Kwa kasi hii maendeleo lazima

Kwa kasi hii maendeleo lazima

Vitambulisho oyeee! Wamachinga oyee! mamantilie oyee! wahudumu wa bar oyeee! Tuko pamoja. Tuvichangamkie hivyo vitambulisho maana elfu 20 kwa mwaka si kitu! Isitoshe hakuna Taifa lililo endelea duniani kwa wananchi wake kutokupenda kulipa kodi. Lipa kodi kwa maendeleo!
 
JF ndo sehemu inaweza pata ukweli na uhalisia pekee wa nchi hii.Kila mtu ana uhuru wa kuandika na kushare hisia zake.Ya 2016 hatimaye yametimia kama ilivyo.
Ukitaka kujua na wehu pia wamo humu humu soma juu kuna post jamaa anamuambia afute huu uzi wake hajui kinachoendelea.
 
nao ni wengi sana.Hao wao hawasomi ujumbe wa ndani na kutafakari,yeye anasoma title tu anaingia kucoment
Ukitaka kujua na wehu pia wamo humu humu soma juu kuna post jamaa anamuambia afute huu uzi wake hajui kinachoendelea.
 
^Hahahaa naona Baba britanicca anampa umbea wote wa nchi hii mwanaye..!mie sichukui kitambulisho chenu aisee..nitachukua siku nikute hosp kuna dawa walai septrin
 
manengelo chukua kitambulisho haha


Pelekeni kwanza madawa hosp...!alafu mimba yangu ya mwisho eti nilichajiwa kadi ya kupimia mimba..nikitoa 2000..niliudhika balaa...!malizeni mambo ya muhimu nitachukua....tafuta boss yyt wa TRA ukae naye akueleze jins wanavyopata shida kwenye ukisanyaji..makusanyo yamedoroa dorooo..yamefubaa km uso wa Mwita Waitara😏
 
Katika Pita pita za pale Viunga Fulani nikakutana na mtu muhimu kwenye Habari za nchi kaniambia yafuatayo

Kila mwananchi lazima alipe kodi. Kuna mfumo wa kuleta utaratibu kama wa nchi Soviet zamani, kila mwananchi alipewa kitambulisho, kuanzia wafanya biashara wadogo wadogo, walilipa Russian rube kadhaa,

Nimesikia
1.Machinga wote kusajiliwa nchi nzima kupewa vitambulisho, kila mkoa utapewa target, na wilaya kila kitambulisho itakuwa 5,000

2.Mama liishe wote
3.Boda Boda wote
4.Wenye maduka madogo madogo
5.Wafugaji
6.Wakulima
7.wafanya kazi wadogo wadogo

Hela hiyo itasaidia sana kwenye kuyatatua Matatizo kuliko kuomba omba nje,

Watanzania wapo 50,000,000 Wenye uwezo wa kuzalisha ni, 20,000,000
Hivyo 20,000,000 times 5,000 ni 100,000,000,000 kwa Mwezi, ni hatari

Britannica
mkuu ulisema kitambulisho kinauzwa bei gani??

Je bado tuendelee kuamini kuwa maendeleo ni lazima kwa mwenendo huu ??
 
Back
Top Bottom