Kwa imani yako (marejeo)

Kwa imani yako (marejeo)

micka jac

Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
49
Reaction score
20
Habari za asubuhi, mnamo tarehe 8 niliandika thread ya kutaka kusaidiwa ada ya mtihani. Wapo walionipa maneno makali yenye kuumiza na pia wapo walionishauri vyema na hata hivyo wapo pia walioahidi kunisaidia lakini imekuwa kimya mpaka leo hii ikiwa usajili unafungwa rasmi mwisho wa mwezi huu. Kiukweli nimekuwa nikijaribu kujishughlisha ktk shughuli tofauti lakini bado sijaweza fanikiwa kwakuwa hali na mzunguko wa pesa umekuwa mgumu. Sikati tamaa kwa kuendelea kujipa matumaini kwakuwa siku hazifanani, labda leo yaweza ikawa bahati kwangu. Ila kiukweli bado sijajua nini hatma yangu mpaka hii leo!! Napenda niwatakie asubuhi njema kaka na dada zangu, mwenyezi mungu awajaalie ya kher na awaepushie yote ya shari. Love all
 
tatizo siku hizi uaminifu umekuwa mdogo sana hasa humu kwenye mitandao.....
 
Yah..uaminifu ni ishu...unaweza kudhan unamsaidia mtu mhitaj kumbe looh anatafta mb za kuperuzi jf....

By the way usikate tamaa jaribu kwa watu wako wa karibu na pia kuna wasamaria umu wanaweza kufanya lolote
 
tatizo siku hizi uaminifu umekuwa mdogo sana hasa humu kwenye mitandao.....

Kweli kabisa waweza kudhani unasaidia kumbe unajikaanga. Bt wenye uwezo msaidien jaman Mungu atawatetea
 
Mie sio mhuni wa kusema nadanganya ili nipate hela za kutumia tu. La hasha, hili jambo ni serious kabisa. Ninashida kweli mwenzenu. Nimejaribu kwa baadhi ya watu wa karibu lakini wapi! Wanaahidi ila mwisho wa siku mtu anakwambia sijapata. Inanibidi niikubali ile hali kwakuwa ni matakwa yake kunisaidia au la. Kiukweli naumia na kuumia kwa hili. Nashindwa kuattend shule kwasababu ule uhuru sina. Naomba sana kwa yeyote. Sitaweza kuingia internet tena kwasababu sina simu huwa naazima. Ila namba za simu za mtu wa karibu ambaye niko naye ni hizi 0654 929 003. Ahsante
 
Hujasema unadaiwa sh ngapi unafanya mitihani gani unasoma shule gani kwani msaada sio lazima upewekononi mtu anaweza kwenda kulipa tu na akakutaharifu hela imelipwa nenda shule funguka
 
Hujasema unadaiwa sh ngapi unafanya mitihani gani unasoma shule gani kwani msaada sio lazima upewekononi mtu anaweza kwenda kulipa tu na akakutaharifu hela imelipwa nenda shule funguka

Ni ada ya mtihan na inatakiwa ikalipwe ofisi za posta. Inatakiwa iambatanishwe na refference number ambazo ninazo mimi.
 
mi siamini kbs mitandao, dirty games nyingi.mtu anapiga fake thread zake na comments unaweza ukahisi kweli mtu kumbe.......
 
mi siamini kbs mitandao, dirty games nyingi.mtu anapiga fake thread zake na comments unaweza ukahisi kweli mtu kumbe.......

Nilichokisema au nilichokiandika kina ukweli. La kwa atakayetaka kufika mpaka shule akutane na mkuu nafikir ataamini. Nilisimama kwa mda kutokana na kutolipa ada lakin ikamjaa huruma baba wa watu na kuniruhusu niendelee kwenda ila pesa ya mtihani aliniambia niongee na ndugu zangu. Siwezi kudanganya hata kidogo!! Siwezi
 
tumsaidieni ni mhitaji kweli mimi nimeahidi kumsaidia japo sijatimiza ahadi yangu lakini nitafanya
 
nimezitoa hapo hadhara, labda kwa anayezitaka kwa moyo thabiti wa kutaka kweli kunilipia anipm mi nitamtumia.
 
Sio kama siwezi kuweka ref no hapa bali nahofia usalama wake. Katika ulipaji wa mitihani kuna hatua tofautitofauti. Licha ya hivyo inatakiwa mlipaji wa mtihani aambatanishe form ya mtihani wa form two, pamoja na ref no.

1. Unaenda na ref no unalipa.
2. Unarudi na risiti uliyopewa posta mpaka shuleni.
3. Unasajili masomo unayofanyia mtihani.
4. Unasubiri form ndan ya siku moja au mbili kutokana na mzunguko au kama ukibahatika kutokuwa na foleni waweza pata siku hiyohiyo.
5. Unarudisha tena form katika ofisi za posta kwaajili ya kupelekwa baraza la mitihani necta.
 
Back
Top Bottom