Wale wanaodai serikali mbili naona maji yamefika shingoni na wamezidiwa hoja kwa kila namna yeyote ile. Hakuna hata mtu mmoja namsikia akitoa hoja ya maana ya serikali mbili na ninaona wanaotaka serikali tatu wanakuja na hoja kali zenye mafunzo, mishiko na wanaonekana kama wanasema ukweli zaidi. Cha kushangaza wa serikali mbili walikuwa hawajajiandaa kabisa kwenye agenda.