Kwa hilo Nagu kachemka!

Inabidi Chadema waweke mkazo wakakomboe jimbo la Mery Nagu maana ni moja ya majimbo mepesi sana kukomboa
 
Wivu tuuu unawasumbua mwaacheni mama yetu!!

unakumbuka siku wanajadili kuboresha hospitali zetu huyu mama alisimama akaanza kusema mimi mwanangu ni dr yuko muhimbili, yaani akaingiza hoja isiyo na maana kabisa. Sawa yupo lakini umuhimu wake nini kama hana vifaa vya kufanyia kazi? Ata kama unampenda kwa kauli anazotoa huyu mama ni ishara tosha kwamba kuna watu hawatakiwi kuongea mbele ya kadamnasi. Amefichua madudu ambayo siku zote tumekuwa tukiyasema bila uhakika,leo katuthibitishia kwamba wao ni kikwazo kwa maendeleo ya watanzania. I hate these type of women ambao hawana uchungu na wanawake wenzao wakihangaika kutafuta maji just because wao wanakula na kusaza.
 
Hili mbona ni zuri tu - huyu mama ni honest; kawaambia watu ukweli na sasa watu wa Arumeru wanatakiwa wachague kupiga magoti mbele ya altare ya CCM au kukataa wakijua kabisa matokeo yake. Binafsi ningemshukuru huyu mama angalau kwa kuwaambia wananchi kuwa chaguo liko vipi; aidha waendelee kuwa watumwa kwa sababu watapewa masufuria ya minovu ya hapa na pale huko minyororo imewashika au watakataa kuitwa watuma na kuvunja minyororo yao.

Asante Nagu!
 
Mary Nagu ajitenge na siasa za visasi. Mimi nilidhani angeongelea madai ya kughushi shahada ya udakatari. Kwa maana hiyo anathibitisha anavyotia walakini kwenye udaktari wake wenye kutia shaka hadi akanushe na kujibu madai kuwa alighushi. Laiti tungekuwa na serikali inayochunguza na kupima maneno na matendo ya watendaji wake. Nagu angekuwa historia sawa na akina Haji Mponda na Lucy Nkya.
 
Mary Nagu ajitenge na siasa za visasi. Mimi nilidhani angeongelea madai ya kughushi shahada ya udakatari. Kwa maana hiyo anathibitisha anavyotia walakini kwenye udaktari wake wenye kutia shaka hadi akanushe na kujibu madai kuwa alighushi. Laiti tungekuwa na serikali inayochunguza na kupima maneno na matendo ya watendaji wake. Nagu angekuwa historia sawa na akina Haji Mponda na Lucy Nkya.
 
BARAZA LA MAWAZIRI
(serikali ya JK)
1. Wassira
2. Merry Nagu
3.

GWANKAJA GWAKILINGO 20:40 Yesterday
By Ngoiva:
BARAZA LA MAWAZIRI
(serikali ya JK)
1. Wassira
2. Merry Nagu
3.
Ngereja

4.malima
5.rukuvi
6.nyarandu(mh yara wanipiga na leso waniumiza)
7.membe
 
Hii ni kinyume na sheria mpya ya uchaguzi anatakiwa kufunguliwa mashtaka haraka sana!!
 
Wivu tuuu unawasumbua mwaacheni mama yetu!!
Huyu mama ni mbuge wa jibo langu la hanang' lkn ananikera kwa kauli zake kama hizo, sijui kwann kapewa uwaziri, KWA MBUNGE WA AINA HII WANAHANANG' TUANGALIE UPE.
 
Ni ukweli usiyo fichika sasa CCM kazi kwisha, kama ata watendaji wa Serekali wanaongea wazi kwamba watakwamisha miradi ya maendeleo kama wapinzani wakichukua jimbo, ujue wamekosa sera za kuzungumza na wameamua liwalo liwe, but wajue kwamba wanatangaza vita ambayo ikianza wenyewe watakua wakwanza ku exit.
Uyu mama ajue nae tutaanza kumshushia mvua ya kashfa zake, Pls Mama Nagu tunakweshimu sana naomba tafadhali ukae kimya usije umbuka apa.

Ana PHD feki aliyoipata chuo feki nchini Marekani kwa Thesis aliyoandikiwa na watoto wa Masters UD!
 
Anaiga za Sumaye aliposema maneno yanahofanana nahayo Enzi zilee kule Moshi. Tunaongozwa na WATU wasiotambua kwamba uongozi ni dhamana unayopewa na wananchi hivyo huwezi kuwatisha waliokupa dhamana hiyo. Wakuu hivi ni kweli jamii yetu inashindwa kujisafisha na uozo wa WATU hawa?
 
Huyo Mama ni wa kupuuza tu, wana Arumeru wasidanganywe, wakitaka kuona kuwa ni heri wachague CDM ili Nassari asimamie maendeleo jimboni mwao, wamuulize Zitto Kabwe, kwenye majimbo manane kabla ya uchaguzi uliop[ita, Upinzani ulikuwa na jimbo moja kwa Mh. Zitto tu mengine yote yalikuwa CCM, lakinindani ya kipindi hicho Zitto ameweza kufanya mambo ambayo hadi sasa ameandika historia, imetengenezwa barabara ya lami nzuri sana, kiasi kwamba baadhi ya wazee wanasema hata wakifa kwa sasa, roho zao zimesuzika kuona cement/lami inamwagwa barabarani.
Hivyo ujinga huo wa kina Nagu ni mbinu zilkizopitwa na wakati
 
Siamini kua katamka hivo wazi kabisa kweny TV... Labda kama ana Kichaa....

Asha amesema na mradi anaodai ni wa EPZ (EXPORT PROCESSING ZONE) kama ule wa mabibo,lakini hivi hao wameru wanakitu gani cha kukosa ikiwa shida wanazo kila siku.
 
Kama CCM tumeshindwa kuongoza nchi ni bora tupumzike na kujipanga upya. Haya ndiyo tunapandikiza chuki zisizo za msingi kwa jeuri ya uongozi. Kulishakuwa na malalamiko hapo awali kwamba majimbo ya upinzani yananyimwa maendeleo, sasa imedhiirika ni kweli. Picha hii imebainika tangu Mrema alipochukua Temeke, jimbo lilikuwa haliendelezwi chochote. Pia tunakumbuka jinsi mradi wa barabara na maji ilivyotelekezwa Rombo kabla ya Mramba kurudi Jimboni. Sasa tunaweza kusema kwanini UBUNGO hakuna Maji ingawa yanapita hapo kwenda MASAKI, OSTERBAY nk. Hii ni dhambi kubwa sana ya kufanya mchezo na kodi za watu.
 
Nimeisikia ile, huyu mama ni popopo kweli, nado sasa katoa siri ya serikali hii, ni kweli maendeleo ya majimbo ya upinzani yako nyuma sana na miradi haiendi huko, Huyu mama kweli amechemsha na kwa kuwa rais ni goi goi basi hakuna atakacho sema.Chadema walitolee tamko haraka sana.
 
Wivu tuuu unawasumbua mwaacheni mama yetu!!



Unafikiria kwa kutumia makalio ama..Aliyoyasema ni akilia au matope..CCM imetawala toka uhuru Arumeru, faida yake ni ipi? Kero ni zile zile na matatizo ni yale yale..We real need changes
 
Wapinzani wasipo lichukulia hili swala kwa mapana na marefu yake basi watakuwa hawajawatendea haki watanzania na kweli watu wataanza kupata wasiwasi juu ya kuchagua wapinzani. Nadhani hii ilikuwa ni fursa ya wapinzani ku-shine kwa kutumia hii kauli ya huyu mama aliyepotoka. Ni kauli ambayo wapinzani wakiivalia njuga majukwaani inaweza ikawapa faida kubwa kwa public na hata kutungwa sheria ya namna ya kugawa maendeleo bila upendeleo. Wapinzani mkiliacha hili lipita mtakuwa mmeikosa bahati ya ku-shine.
 
Kwani huko ambako CCM walichaguliwa(ikiwemo Hanang ambako huyu dada ni mbunge) wamefanya maendeleo gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom