Kwa Hili Wanastahili Pongezi----

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Wakati hakuna anayeelewa kwa undani maana halisi ya " kujivua magamba" labda wana CCM wenyewe waliokaribu na CC, kilichowazi ni kuwa CCM imekubali kuwa chama chao kiligubikwa na tuhuma za ufisadi au kulikuwa na ufisadi wa kupanga kweli ndani ya chama.

Hii ni hatua nzuri na ni ukomavu wa kisiasa. Si wengi miongoni mwetu wana ujasiri wa kukiri hadharani mapungufu yao! Ukiondoa wanafiki!

Nadhani hii iwe changamoto kwa vyama na taasisi nyingine kujipima na kukiri makosa yao au mapungufu yao! Huku ni kujiimarisha si kujidhoofisha kama wengi humu wanvyodhani.

Ni wakati sasa Chadema nayo iangalie kwa kina shutuma zinazoelekezwa dhidi yake, hususani Udini, Ukabila,Ukanda na Umangimeza kwenye uongozi wa kitaifa wa chama hicho!

Kufumbia macho hayo ni kukidhoofisha chama chenu, acheni kujidanganya!
 
tuwapongeze vp wakati walikuwa wanakataa kuwa hakuna mafisadi kwao! sasa wamezidiwa tuwapongeze!?
 
Wakati hakuna anayeelewa kwa undani maana halisi ya " kujivua magamba" labda wana CCM wenyewe waliokaribu na CC, kilichowazi ni kuwa CCM imekubali kuwa chama chao kiligubikwa na tuhuma za ufisadi au kulikuwa na ufisadi wa kupanga kweli ndani ya chama.

Hii ni hatua nzuri na ni ukomavu wa kisiasa. Si wengi miongoni mwetu wana ujasiri wa kukiri hadharani mapungufu yao! Ukiondoa wanafiki!

Nadhani hii iwe changamoto kwa vyama na taasisi nyingine kujipima na kukiri makosa yao au mapungufu yao! Huku ni kujiimarisha si kujidhoofisha kama wengi humu wanvyodhani.

Ni wakati sasa Chadema nayo iangalie kwa kina shutuma zinazoelekezwa dhidi yake, hususani Udini, Ukabila,Ukanda na Umangimeza kwenye uongozi wa kitaifa wa chama hicho!

Kufumbia macho hayo ni kukidhoofisha chama chenu, acheni kujidanganya!

Naunga mkono mada hii, na tukiichukulia kwa vitendo italeta matokeo mazuri.Isije ikaishia kwenye jukwaa na maneno matupu. Lakini hata hili la kukiri hadharani ni hatua nzuri.
 
CCM wanastahiki pongezi kwa hatua hii,japo ni mapema lakini kwa kuanzia ni hatua njema,Manake kwa yeyote CCM kama kikundi chenye malengo yake kwa mujibu wa ILANI YAO ya uchaguzi na katiba ya Chama Cha Mapinduzi,na ndani yake ulevi wa kitaasisi [Kushika Hatamu kwa Chama] kutenda jambo hilo kwahitaji moyo,japo ilitakiwa daima kuwe na viongozi wenye kuona mbele, na kuzingatia matakwa ya Wananchi na si ULEVI WA KITAASISI.

Mwanzo Mzuri patachimbika si unajua tena MGONGANO WA KIMASLAHI [CONFLICT OF INTEREST].
 
usidanganyike na ondoka kwenye hilo kapu! CCM wote wachafu, akina EL,RA na change hawatafanywa lolote, labda wauawe tu, maana wao ndio watatoa siri zote za uchafu wa CCM! CCM hawako tayari

CCM ili ijisafishe JK must step down kwanza, ama sivyo acheni kununua na kuwapa watu utajiri kisa eti wanajivua gamba!
 
Ni wakati sasa Chadema nayo iangalie kwa kina shutuma zinazoelekezwa dhidi yake, hususani Udini, Ukabila,Ukanda na Umangimeza kwenye uongozi wa kitaifa wa chama hicho!
Mdini JK anayetoa upendeleo kwenye appointments zake.
Ukabila haupo Chadema.
Mbowe - Mchagga
Arfi- Mfipa
Slaa- Mmbulu\Mbarabaig
Zitto- Mha
Baregu- Mhaya
Rwakatare- Mhaya
Mnyika-
Tumbo- Mngoni
Mtemelwa- Mndengereko
Susan Kiwanga- Mpogoro
Regia Mtema- Mpogoro
Mama Kaihula- Mnyakyusa
Na wengineo wengi. Ukabila unatoka wapi we mpuuzi?
 
hoja ya ukabila na udini hazina mshiko katika nchi na wewe kutoa hii mada bila uchunguzi ni kukurupuka
lakini kujivua gamba ccm pia umefuka moshi mkuu hao watu unaosema wewe ni wajumbe wa HALIMASHAURI KUU YA CCM NA kwa taarifa yako JK alipojaribu kuwachuna ngozi kikao kilimshinda na mambo na mafisadi wakashinda sasa tutoe pongezi kwa lipi?
Wakati hakuna anayeelewa kwa undani maana halisi ya " kujivua magamba" labda wana CCM wenyewe waliokaribu na CC, kilichowazi ni kuwa CCM imekubali kuwa chama chao kiligubikwa na tuhuma za ufisadi au kulikuwa na ufisadi wa kupanga kweli ndani ya chama.

Hii ni hatua nzuri na ni ukomavu wa kisiasa. Si wengi miongoni mwetu wana ujasiri wa kukiri hadharani mapungufu yao! Ukiondoa wanafiki!

Nadhani hii iwe changamoto kwa vyama na taasisi nyingine kujipima na kukiri makosa yao au mapungufu yao! Huku ni kujiimarisha si kujidhoofisha kama wengi humu wanvyodhani.

Ni wakati sasa Chadema nayo iangalie kwa kina shutuma zinazoelekezwa dhidi yake, hususani Udini, Ukabila,Ukanda na Umangimeza kwenye uongozi wa kitaifa wa chama hicho!

Kufumbia macho hayo ni kukidhoofisha chama chenu, acheni kujidanganya!
 
ccm ni watanzania kama chadema, tatizo la ufisadi ni janga la kitaifa nchi nzima imemezwa na ufisadi, zito alitulizwa na pesa hivyo kila mtu anaweza kuwafisadi rais anatakiwa atangaze vita ya ya ufisadi kitaifa walio lihuju taifa wote wafilisiwe na washitakiwe mahakamani.
 
aliyetoa hii thread naona angepost kwenye thread zilzopita maana kila siku kuvua gamba tu sasa ma-mods muwemnasoma thread zinazofanana nakutupa kule.. amini nawaambieni product za msekwa humu ndani kibao
 
hawapaswi kupongezwa-ningewapongeza kama wangewachukulia hatua-ila kuwaacha hivihivi nimezidi kuwaona hawana maslah kwa taifa-huwez kuwa na mwizi na uka-acknowledge kua kweli mwizi unae then humpeleki kwenye vyombo vinavyohusika
 
aliyetoa hii thread naona angepost kwenye thread zilzopita maana kila siku kuvua gamba tu sasa ma-mods muwemnasoma thread zinazofanana nakutupa kule.. amini nawaambieni product za msekwa humu ndani kibao

Na ni mapema sana kuthibitisha kwamba hata Msekwa mwenyewe yumo humu ndani
 
Kwahiyo umetafakarii... Ukaona CCM wamefanya jambo lamaana sana, hadi wastahili pongezi!?.. Embu lete faida za huko kujivua gamba kwa CCM!..
 
Sasa swala la MAGAMBA ambayo hadi leo hata KIPANDE hakijaondoka, utayaletaje kwenye mambo ya CHADEMA?

Nimesoma ujumbe wako na naona ume-WELD WELD mambo hadi kuwa kama huyu Mwana dada.

Last edited by a moderator:
Hii kitu umeandika ni sawa na kuzunguka kichaka wakati njia unaiona,umeanza kwa kuisifia ccm mwishowe ukaangusha tuhuma ss sijui ni hisia zako au umetumwa na Msekwa kuja kutupima humu!,hivi udini unaouzubgumzia(usioonekana miongoni mwa Wtz)na ufisadi wa matrilioni ya walipa kodi kipi zaidi!?Acha hizo chama cha magamba kimekufumba Tena macho kwa kukudanganya kuwa kimejivua gamba wakati wahusika wa ufisadi sio watatu na wamepewa siku 90 waendelee kula bata!?Sasa unawezaje kusema mmejivua gamba bila kuwashitaki watuhumiwa?,au magereza ni kwa ajili ya wanyonge tu????????????tumechoka na porojo za ccm!!!ah
 
Wakati hakuna anayeelewa kwa undani maana halisi ya " kujivua magamba" labda wana CCM wenyewe waliokaribu na CC, kilichowazi ni kuwa CCM imekubali kuwa chama chao kiligubikwa na tuhuma za ufisadi au kulikuwa na ufisadi wa kupanga kweli ndani ya chama.

Hii ni hatua nzuri na ni ukomavu wa kisiasa. Si wengi miongoni mwetu wana ujasiri wa kukiri hadharani mapungufu yao! Ukiondoa wanafiki!

Nadhani hii iwe changamoto kwa vyama na taasisi nyingine kujipima na kukiri makosa yao au mapungufu yao! Huku ni kujiimarisha si kujidhoofisha kama wengi humu wanvyodhani.

Ni wakati sasa Chadema nayo iangalie kwa kina shutuma zinazoelekezwa dhidi yake, hususani Udini, Ukabila,Ukanda na Umangimeza kwenye uongozi wa kitaifa wa chama hicho!

Kufumbia macho hayo ni kukidhoofisha chama chenu, acheni kujidanganya!

ccm oyeee, magamba juuuuuu zaidi
 
Kukiri hakutoshi, tunataka hatua zichukuliwe za kuwashtaki wahusika wote, na fedha zote zilizoibwa zirudishwe hazina.
 
Back
Top Bottom