CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,065
Mimi nilidhani tumepata uongozi ambao utaonyesha mabadiliko ukilinganisha na uhuni ule wa akina Mkoba, lakini nimeshangaa sana kuona TUCTA hii ya sasa huku inakoelekea...
TUCTA imepanga kuonana na Rais eti kuwaombea msamaha waliokutwa na vyeti feki wasamehewe... najiuliza wafanyakazi nchi wamepata mkosi gani kila mara wanapochagua uongozi!
mimi nilidhani mngemuunga mkono Mheshimiwa Rais zoezi hili likaenda kwa haraka ili mambo mengine yaendelee..
1. Hivi TUCTA mnajua kuna watu walipandishwa madaraja na wakashushwa na hela zao hawakulipwa hadi leo kwa kisingizio hiki cha vyeti? leo hii badala mpiganie watu walipwe madai yao mnaenda eti kuwaombea msamaha watu wenye vyeti feki?
2. TUCTA mnajua ile nyongeza ya mshahara ya mwezi julai mwaka jana haikutolewa kwa kisingizio cha vyeti na uhakiki? badala mje na majibu nyongeza hiyo inatolewa lini kabla ya mwezi wa saba mnatuletea ujanja ujanja hapa?
3. Rais amesema atatoa nyongeza ya kawaida iliyokuwa imesimamishwa, TUCTA mnatakiwa kutupa majibu je nyongeza hiyo itajumlishwa tangu julai mwezi wa jana au inaanza julai mwaka huu?
Serikali imeweka wazi kuwa kama kuna mtu ameonewa basi njia za kufwata na wapi waende zipo, TUCTA fanyeni mambo ya msingi, kumbuka hadi leo kesi ya makato ya loan board 15% bado iko mahakamani na nyie mmekaa kimya.
TUCTA acheni kutafuta kiki za kijinga.. mnaboa