amba.nkya
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 446
- 131
Habari wanaJF
Ni dhahiri kwamba mkuu wa nchi akitamka jambo lolote jamii huamini na kulichukulia jambo hilo kwa uzito wa kipekee. Rais JK akiwa kwenye mjadala wa Kigoda cha Mwl. Nyerere, UDSM wiki hii alisema watalaam wa kilimo hawana uzalendo kwa nchi yao kwa kutofanya utafititi wa kutosha kwenye kilimo kama inavyofanyika kwenye sekta nyingine.
Akitolewa mfano kwa nia ya kujenga hoja yake, amesema mbegu nyingi zinaagizwa kutoka nchi za nje ambazo zimefanyiwa utafiti kwenye mazingira tofauti na kutokabiliana na hali ya hewa nchini Tanzania na kuathiri uzalishaji wa mazao yatokanayo na mbegu hizo, na hivyo kuleta hasara kubwa kwa watanzania.
Kwa kauli hii ya Rais JK amepotosha jamii kutokana na ukweli kwamba kuna tafiti nyingi sana zinafanyika kwenye kilimo tena kwa gharama kubwa lakini Serikali yenyewe inapuuza matokeo na ushauri wa tafiti hizo kiasi cha kuwakatisha tama watafiti wa kilimo.
Tatizo la Serikali inathamini sana watalaam kutoka nje tena kwa gharama kubwa wakati tuna wanatanzania wazuri waliobobea kwenye Nyanja mbalimbali za utalaam lakini wanadharauliwa na kubezwa.
Nawasilisha .