Kwa hili nitawachukia wanawake milele. Na sitowasamehe.

Haha bado wewe, we endelea kugawa k kama karanga afterall huilipii vat
hakuna nini wala nini hapo!

mke hampendi tena si ajabu alilazimishwa au jamaa alimtenda sana wakati wa uchumba sasa kaamua revenge.

lol, eti mume anifume na mie nikubali eti nimelala na mijitu 6? ningemwambia mmoja tu tena mara moja then roho ingenisuta na ningejirekebisha mwenyewe tu kimyakimya.

mke gani huyo tena hajafundwa kabisa, wake waliofundwa huwa hawanogewi na mechi za nje wala hawakubali ukweli labda umfume live kainamishwa.

HAYA MABO YALIKUEPO TANGU ENZI ZA MABIBI BANA, SEMA WAO WALIFUNDWA WAKAFUNDIKA.
 
Ukome kuwavamia viruka njia na utalia hadi arudi masiha ka vipi hamia jangwani ukaishi peke yako ,bila wanawake ungekuwepo duniani?mwangalie sura ka libolo
 
haya ndio madhara ya kupambambazukia mapenzi ukiwa tayari mkubwa.........nani aliyekuambia uoe kabla ya kumchunguza mwenendo wake.............hutakiwi kuwachukia wanawake wote kwani kuna wanawake pia waliofikia level zako za kuumizwa na waume zao so hii ni kwa mtu binafsi siyo wote. Jitahidi utengane naye kwa amani uanze maisha mapya kwani hata kama umeumia kiasi gani ipo siku utasahau tu
 
watch out Mcheza Karate coz kuna msemo usemao dont promise when you a soo happy and dont make decisions when you are so angry,sasa na we nnachoona hapa unamake decisions katika hali ya hasira nyingi jambo amabalo sio zuri mama ni mama nenda uendako kamwe hutampata kama yeye,tafadhali tengua kauli yako kwani hata mama yako akijua maoni yako hayo ataumia kuliko unavyofikiria wewe,ila pole sana kwa maswahibu yaliyokukuta Mungu yupo na usikate tamaa iko siku atakulipia na kuutuliza moyo wako.
wanawake wote ni makatili hata mama.
 
Last edited by a moderator:
wanawake wote ni makatili hata mama.

Afadhali hata ungeongea kuliko kuandika chini kabisa!!!! Hii ni statement mbaya sana kwa binadamu wa aina yoyote kuandika. Huyo mwanamke si umekutana naye akiwa na meno yake 32 mdomoni, mkajidai mnapendana na kufunga ndoa haraka haraka bila kuchunguzana??? Sasa kinachokufanya umseme mama yako ambaye alikuwa na wewe tangu unaumbika TUMBONI KWAKE ni nini? mama yako alikuwa na wewe kabla hata hujajulikana hiki ni kidole, hiki ni kichwa, huu ni ubongo (ambao kwa sasa umeoza kisa mkeo kakusaliti). Haya mambo sio mapya kipindi hiki kijana, yanatokea kila kukicha. Asilimia kubwa sana sasa hivi watu wameachana kwa sababu either ni mwanaume au mwanamke? na bado watu maisha yanasonga mbele na huwasikii wakisema namchukia mama yangu au baba yangu because whether you believe me or not the ONLY person who can understand your suffering right now, is your MOTHER. Kwa sababu kumbuka mlikuwa mwili mmoja wakati uko tumboni. So shut up and be a man!!!!!!!
 
Pole sana. Lkn bado naamini kama wanawake, pia kuna wanaume wakatili na kwamba tu hadithi hazijaandikwa hapa...Na kwa upande mwingine kuna waliyobahatika kuwapata wanawake na wanaume walio wema.

Kumbuka unakufuru kwa kumchukia mama yako.
 
Usimchukie mama yako mkuu,ila la muhimu muombe mungu akupe ujasiri ktk kipindi cha majaribu kama hayo unayopitiia na naamini utayashinda na kusonga mbele.Usiruhusu mtu kukuharibia maisha wakati naaamini kabisa wengi wetu tumeoa watu ambao tumekutana nao ukubwani na kwa mtu kujificha kwa muda especially kama hamkuwa eneo moja ni rahis.
Kumbuka huyo sio ndugu yako na hata ukifa kwa hizo stress yeye atasonga mbele na anaweza olewa na mmoja wapo wa hao mabazazi wake,au nao wanaweza mtema vile vile.
 
wanawake wote ni makatili hata mama.

Yanayokupata yanakustahili,radhi ya mama yako hiyo na ukiendelea kumdharau uta chitiwa mpaka siku unaingia kaburini.
Yaani mwenyewe ukaoe majanga halafu uje utulaumu wanawake wote!
 
Dah!!! Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta. Hiyo ya kuwachukia wanawake wote mpaka mama yako mzazi haihusu kitu. Si kweli kwamba samaki mmoja akioza basi wote wameoza. Kitendo cha mama yako kubeba ujauzito wako kwa miezi tisa na kukulea ukiwa hujitambui hili au lile hadi leo hii umekuwa mtu mzima mwenye akili yake wa kujua baya na zuri ni kitendo ambacho unastahili kukienzi wakati wote wa uhai wako na kumpa mama heshima kubwa sana anayostahili. Machungu ya kutendwa na mkeo yatakapoisha labda unaweza kuamua kupenda tena.

Best King'asti uzi huu hauhitaji kuweka wimbo wowote ule yaliyomkuta ni makubwa sana hasa ukitilia maanani ni ndoa ya miezi mitano tu na bado ana hasira sana asije akaudhika zaidi na kuitumia bastola yake kufanya mauaji.


kabla haujazimia tena....pole baba. Lakini huoni kama unatuonea kutuchukia wote kwa sababu ya mkeo? Muulize vizuri kama ni kwanini alifanya hivyo. Kapime ukimwina uendelee na maisha yako.

Tahadhari...bastola inataka ushujaa baba. Kama ni adui utazinduka umefungwa kamba. Ningekuwa mkeo ungeamka unikute nimekushikia bastola na wewe uniambie wakati tunadate umenicheat mara ngapi.

BAK ama Sikonge plz, wimbo wa majanga umfariji huyu mpendwa.
 
Last edited by a moderator:
kabla haujazimia tena....pole baba. Lakini huoni kama unatuonea kutuchukia wote kwa sababu ya mkeo? Muulize vizuri kama ni kwanini alifanya hivyo. Kapime ukimwina uendelee na maisha yako.

Tahadhari...bastola inataka ushujaa baba. Kama ni adui utazinduka umefungwa kamba. Ningekuwa mkeo ungeamka unikute nimekushikia bastola na wewe uniambie wakati tunadate umenicheat mara ngapi.


BAK ama Sikonge plz, wimbo wa majanga umfariji huyu mpendwa.

We King'asti sasa huyu hata miaka 30 sijui kama kafikisha,yaliyomkuta ndio hayo,hataki kuona mwanamke tena maishani mwake hata mama yake,for that case, sasa akifikisha miaka 40 akaanza kuvaa jeans za kubana na t shirt,utasema anajiendekeza tu.Matatizo yameumbiwa watu na watu wengine ndio sisi.
Pole sana mkuu Mcheza Karate,nyanyuka,jifute vumbi,pangusa machozi songe mbele,kama uliaza na mungu basi malizie nae utakuwa ok
 
Kheee kumbe na wanawake nao huwaga wanachiti?

Halafu iweje umuachie mkeo akuchiti lakini?

Yote yaliyokukuta umejisababishia mwenyewe. Sasa mimi nakushauri uwatafute wote hao aliochiti nao halafu uwapige uwakomeshe waache tabia zao mbaya.
 
Ndio matatizo ya kuoa bila kukaa na Demu ukamjua tabia na kuonja papuchi kama iko Sawa Sawa.....lakini si kulaumu sana, ndio matatizo ya kusoma seminary!
Usidanganyike kuwa ukikaa na demu kabla ya kuoa ndo utajua tabia yake bro.
 
Naandika nikiwa na kilio cha jitimai na majonzi yasiyoisha milele.

Mwezi desemba mwaka jana nimefunga ndoa na mke wangu.

Lakini tangu tufunge ndoa nikawa na mashaka na mwenendo wa mke wangu.

Wiki mbili zilizopita nilipata jambo la ajabu. Mke wangu kaniambukiza ugonjwa wa ngono. Nilipomuuliza akadai kuwa hajui amepataje.

Nikimweleza twende hospitali anakataa. Nimeenda nikatibiwa na naendelea na tiba.

Juzi usiku nikiwa nataka kupata ukweli nikaja nyumbani na kumwomba tuongee chumbani. Nikatumia mbinu ya kijeshi nikatoa bastola yangu ambayo hajawahi kuiona hata siku moja na nikaanza kumsaili.

Mke wangu akanitajia orodha ya wanaume aliotembea nao ktk kipindi hichi cha ndoa ya miezi 5 inatisha. Katembea na wanaume sita tofauti.

Nilijikuta napoteza nguvu na fahamu. Nilipozinduka mke wangu kadai tutengane kwani dhambi aliyonitendea haipaswi kumsamehe.

Kila baada ya kama masaa 3 napoteza fahamu. Ndugu zangu hawana taarifa. Lakini ndugu na wazazi wa mwanamke wanajua kinachoendelea.

Ni ngumu kuamini ktk hali ya kawaida lakini najikuta kila akija mwanamke akija kunijulia hali nataka kuzimia tu na napata hasira.

Sitofika kupenda tena na nawachukia wanawake hata mama yangu mzazi aliyenizaa.

POLE SANA KAKA! Lakin futa kaul ya kuwachukia wanawake wote tatizo lako haukuowa wife material na kinacho waponza wengi ni pale mnapoupinga wimbo wa uzuri sio sura ama uzur wa maumbile,vjana wengi mnavutiwa na muonekano wa nje.
 
Tupendane kwa machale jamani, i mean usimpe m2 100%ya moyo wako ili usije poteza fahamu kama kaka Mkubwa hapa. na hii ki2 :laser: kaka iposiku utai2mia kiukweli.
 
Kwanza Mshukuru Mungu bado uko hai hujajiua wala huyo mkeo hajaichukua hiyo bastola na kujiua yeye au kukuua wewe.

Pili, mtake radhi Mama mzazi na omba msamaha kwa Mungu kw kosa la kumchukia hujui ulitendalo japo najua ni hasira na machungu yaliyokupata.

Kama huwa unasali, nadhani ni kipindi cha kusali sana kuliko wakati wowote.
Lakini umeweza kumiliki bastola muda wote huo na mkeo hajawahi kujua PR yako na wife iko sawa? huenda pakawa na mambo mengi sana ambayo hujayaeleza hapa.

Mwisho wa yote:

Binadamu yeyote anawezafanya kitu chochote wakati wowote bila kujali chochote
 
Back
Top Bottom