Kwa hili, Nimeshindwa kumuelewa Rais Magufuli

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
756
743
Rais wetu ni "Dkt" ; udoctor wake sio wa kubahatisha coz ameenda shule vya kutosha.

Huwa namuelewa sana Rais wetu kwa namna anavyopanga hoja zake kwa mantiki (logic).

Ila kwenye hili Swala la Bunge Simuelewi.

Rais anasema Majipu yatumbuliwe hadharani, jambo ambalo linaonyesha anataka mambo yaende kwa uwazi.

Sasa iweje ashindwe kutuonyesha Bunge moja kwa moja kama ilivyozoeleka?

Rais na Serikali kwa ujumla inaogopa nini?
 
Akionyesha bunge kuna mambo mengi hatavumilia kuambiwa ukweli, ukimwangalia sana Magufuli anachofanya ni kuhakikisha yatangazwe mazuri tu anayoyafanya lakini mabaya ya serikali yake hataki yatangazwe ili kurudisha imani kwa wananchi ili CCM ipendwe, lakini kwa ulimwengu huu wa digital ni sawa na kuchota maji ya bahari kwa tenga kwenda kujaza ziwa victoria
 
Akionyesha bunge kuna mambo mengi hatavumilia kuambiwa ukweli, ukimwangalia sana maghufuli anachofanya ni kuhakikisha yatangazwe mazuri tu anayoyafanya lakini mabaya ya serikali yake hataki yatangazwe ili kurudisha imani kwa wananchi ili ccm ipendwe, lakini kwa ulimwengu huu wa digital ni sawa na kuchota maji ya bahari kwa tenga kwenda kujaza ziwa victoria
anapenda kuimbiwa sifa tu,akikosea hataki kung'ongwa
Anacholaumu ni kitendo cha maghufuli kuficha yanayoendelea bungeni
uko sahihi
 
Bung/sisiem linamuogopa Magufuli maana mijadala kama escrow au epa ikijitokeza awamu yake anaweza kufukuza hata mawaziri nane. Hivyo kwa kuwa bunge ni muhimili unajitegemea wanajaribu kuweka mazingira ya kuzuia kuvuma kwa mijadala itakayojitokeza.
 
ukitaka kujua kiwango cha kuelimika cha rais wa Tz na uwezo wa kujenga hoja fuatlilia anavyojibu hoja na maswali tata..
 
Show ya bunge kutoonyeshwa Live inasimamiwa na Waziri wa habari..au huyo waziri na yeye ni mhimili mwingine unaojitegemea nje ya serikali na bunge?
Hapo ndo kuna contradiction ya kikatiba, na ndipo huwa naichukia CCM kwa kukataa katiba ya warioba, ili tuendelee hatuhitaji wabunge kuwa mawaziri
 
Rais wetu ni "Dkt" ; udoctor wake sio wa kubahatisha coz ameenda shule vya kutosha.
Huwa namuelewa sana Rais wetu kwa namna anavyopanga hoja zake kwa mantiki (logic).
Ila kwenye hili Swala la Bunge Simuelewi.
Rais anasema Majipu yatumbuliwe hadharani, jambo ambalo linaonyesha anataka mambo yaende kwa uwazi. Sasa iweje ashindwe kutuonyesha Bunge moja kwa moja kama ilivyozoeleka?

Rais na Serikali kwa ujumla inaogopa nini?
Anaogopa kutumbuliwa bungeni
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Akionyesha bunge kuna mambo mengi hatavumilia kuambiwa ukweli, ukimwangalia sana maghufuli anachofanya ni kuhakikisha yatangazwe mazuri tu anayoyafanya lakini mabaya ya serikali yake hataki yatangazwe ili kurudisha imani kwa wananchi ili ccm ipendwe, lakini kwa ulimwengu huu wa digital ni sawa na kuchota maji ya bahari kwa tenga kwenda kujaza ziwa victoria

Mkuu nilikuwa najaribu kutengeneza sentesi hii lakini nikawa sipati maneno mazuri ya kuweka. Ila kwa hii post yako ni kwamba umeweka kisu kwenye mfupa.

cc: lizaboni, msemajiukweli, motochini, mzee mwanakijiji,
 
Bunge na serikali ni mihimili miwili isiyoingiliana mambo yake ila inategemeana, sijaelewa mkuu unaulaumu muhimili upi.
Mkuu, kwani aliyezuia bunge lisiwe live ni BUNGE lenyewe au SERIKALI!? Mi ninavyo kumbuka ni NAPE ndiye alikua wa kwanza kuzuia hilo na kuonesha kua hili jambo lina Baraka za baraza Zima la mawaziri mhe rais alitupia neon siku ile alipokutana na MAJAJI; Umesahau mkuu?
 
Back
Top Bottom