Wewe Ray Jay kweli ni mtu wa Mtwara au umeamua kufanya Sarakasi na taulo mchana kweupe?,CCM sasa ndiyo inaadhirika ,kwani haukuona jana pale ,Viongozi walivyozomewa?,kama kusoma haukusoma je hata Picha kaka?.
NAFARIJIKA...!
Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa
Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!
Viongozi wa chama kutoa maagizo kwa viongozi wa serikali! Labda tusubiri utekelezaji wa maagizo! Hata Nape alitoa maagizo nyufa za majengo kule UDOM zizibwe!... Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara...
Mimi si mtu wa Mtwara bali ni mtu wa Nachingwea wilaya iliyopo mkoa wa Lindi, lakini matatizo ama kero hizo za Mtwara juu ya korosho hazina tofauti na huku kwetu, lakini si tu kuwa matatizo yetu yanafanana lakini pia aina ya watu wake tunafafa, ninayo haki lakini pia wajibu wa kuyazungumza yale yanayowahusu watu wa kusini, haya ni yetu...!
Viongozi wa chama kutoa maagizo kwa viongozi wa serikali! Labda tusubiri utekelezaji wa maagizo! Hata Nape alitoa maagizo nyufa za majengo kule UDOM zizibwe!
Kwa hiyo hapa unatuambia kwamba viongozi wa serikali ya CCM ( kama vile mawaziri na wakuu wa Mkoa) hawafai kuongoza nchi hii kwa kuwa wanasubiri kukumbushwa vitu vilivyomo kwenye ilani ya chama, ambayo nakala zake wanazo maofisini! Na kwa kuwa hawafai, basi tuchague chama kingine ambacho serikali yake haihitaji kukumbushwa mambo yaliyo bayana!... kulegalega nafasi ya kiongozi wa chama ni kukumbusha kwa kuyataja maagizo hayo kwa waziri ama kiongozi husika chini ya wizara fulani juu ya utekelezaji wa agizo hilo ambalo lipo kwenye ilani ya Chama