Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,357
- 100,372
Nawapongeza baadhi ya Wana CCM walioguswa na kutoweka kwa Ndugu Saanane, naamini sio kwamba ni kwa sababu wanamfahamu pengine lah ila kwasababu Ben ni binadamu kama Wewe na Mimi.
Hata hivyo nimeshangazwa na kuumizwa na asilimia kubwa sana ya baadhi ya Wafuasi, Makada na Wapenzi wa CCM wakifurahia au kuonyesha kufurahia kutoweka kwa Binadamu mwenzao. Nichukue fursa hii kwamba hakuna MTU mwenye damu ya chama, dini ya chama wala uhai wa chama. Sisi wote tunabaki kuwa ndugu, Leo hii tukifurahia baya la Ben kisa tu sio "mwenzetu" kesho tutafutwa machozi na nani??? Ben ni mdhambi kiasi gani cha kustahili dhihaka hizi za Wafuasi hawa???
Yamemkuta Ben Leo, hatujui yuko hai ama lah! Vyovyote vile lazima tusikubali au kuruhusu itikadi na mapenzi yetu ya vyama yatufikishe hapa. Wanetu watarithi nini? Chuki? Ubaguzi? Kamwe hatutabaki Salama, siasa zitapita Bali maisha yetu na undugu wetu utabaki hata baada ya vizazi na vizazi.
Naomba labda kwa namna ile ile ambayo tulilaani wale walioshangilia mauaji ya Polisi wetu kipindi kile hivyo hivyo tulaani na wana CCM hawa wachache wa mitandaonj Wanaona ni sawa kwa Ben kutoweashwa.
Kama yametokea kwa Ben na tukachekelea usisahau kuwa yanaweza kutokea kwako au kwangu pia. Ben ana ndugu, ana Marafiki, ana majirani ana damu na mwili kama wako na wangu. Ya Mungu mengi, nani anaifahamu kesho yake??
Kama Wewe unafanya hayo kwakua Uko chini ya mwamvuli wa chama Fulani basi jua wazi kuwa hayo hayo yatakuja kukupata au kuwapata ndugu zako hata baada ya Wewe kuondoka. Maumivu na vidonda hivi tunavyowasababishia wengine basi Mungu ni mwaminifu sana na hajawahi kushindwa, atalipa muda ukifika.
Tunakuombea Ben huko uliko!¡