Kwa hili dk ndalichako ajivue gamba tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili dk ndalichako ajivue gamba tu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by thatha, Mar 2, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  HII NI MAKALA KATIKA GAZETI LA ANNUR LA LEO, UK 4


  KWA HILI DK NDALICHAKO ANAHUSIKA

  Nimeisoma makala katika gazeti la annur la februari 24 yenye kichwa cha habari " mchawi wa Zanzibar sio Joyce Ndalichako". Mwandishi wa makala hayo ambae alijitambulisha kama mwandishi maalum amejaribu kuonyesha mambo mengi yanahusu kushuka kwa elimu Zanzibar na kubwa zaidi amedai kwamba wanafunzi wa Zanzibar hawapaswi kumlaumu katibu mtendaji wa baraza la mitihani (NECTA) kwa matokeo ya shule zao.

  Binafsi nakubaliana na baadhi ya hoja ya hoja za mwandishi wa makala hayo hasa katika swala zima la kuporomoka kwa maadili ya vijana, watoto hata wazazi kwa ujumla, lakini pia la mfumo wa elimu wa visiwani unahitaji ufanyiwe utafiti (research), kwa mfano hapo miaka ya nyuma wanafunzi wanaofanya vizuri darasa la saba na kuchaguluwa kujiunga na shule maalum (michepuo) walikuwa wakifanya vizuri sana katika mtihani wa kidato cha nne cha sita,Lakini sasa licha ya kuwa hivyo lakini imepungua kwa kiasi kikubwa.
  Kwa mtazamo wa harakaharaka, wanafunzi wengi sasa wanaofanya vizuri ni wanafunzi wanaotoka shule za mjini Unguja, hizi ni shule za serekali kama Lumumba, Benbella, Kiponda , shule ya Ufundi Mikunguni ambayo mwkaa huu imekubwa na fagio la NECTA na shule ya Biashara Mombasa. Kwa upande wa shule za watu binafsi (private)au mashirika ni ni shule kama SOS, sunny Medrasa ,shule ya wanawake Al ihsani , high view na Lauret ambazo mwaka huu nazo zimekumbana an fyagio la Chuma la NECTA.
  Kwa upande wa kisiwa cha Pemba shule zinazoleta afueni ni shule ya Utaani ya Wete ,shule ya ya Ufundi Kengejana shule maarufu ya Fidel-Castro iliopo chake Chake .
  Hii ni changamoto kubwa kwa wazazi , serekali na wanafunzi kwa ujumla, hapa unatakiwa ufanyike Utafiti wa kina kwanini hali hii inazidi kuongezeka siku hadi siku huku wazee wakitumia gharama kubwa ya kuwasomesha watoto wao kwa matumaini ya kujikomboa kielimu.
  Lakini juu ya matokeo ya 2011 kwa upande wa Zanzibar, hapa ni wazi Dk Ndalichako anahusika, sijawahi kuona matokeo ya kushangaza ya mtihani wa taifa yakitolowa kama ilivyotokea haya ya 2011 hapa Tanzania ,nimetembelea nchi nyingi na pia kusikiliza vyombo vingi vya habari vya kimatifa lakini sijasikia popote pale baraza la mitihani lilitumia mkokoto wake kupata matokeo ya mtihani wa taifa kama ulivyotumika 2011.nimesoma darasa la kwanza hadi kumaliza shahada ya pili ya masmo yangu sijabahatika kuona Chuo au taasisi yoyote nchini imetoa matokeo ya mtihani kama ilivyofanya NECTA.
  , Wanafunzi 52 wa chumba kimoja wanafutiwa matokeo na anabaki mmoja!, wanafunzi 150 wa shule moja wanafutiwa wanabaki 10 tena hao waaliobaki wanaambulia daraja la nne!,shule moja inafutiwa, shule ya jirani haiguswi hata kidogo !huku Katibu mtendaji wa NECTA anatamka kwamba NECTA ni chombo makini katika utendaji wake!Upi utendaji ulioutuka wa NECTA hapa, ni kuwafutia watoto huku baraza hilo likishtumiwa
  na kila mdau kwamba kimeshindwa kusimamia mitihani kwa umakini?
  Ukiskiliza mijadala mingi kwenye mitandao utagundua wasiokuwa waislam wanasema waislam hawana uwezo wa kusoma ndio maana shule za Zanzibar na za waislam matokeo yao sio mazuri. Lakini tujiuliza?Lakni tujiulize jee waislam hawasomi katika mitihani ya NECTA tu?mbona mitihani ya NACTE (Baraza la vyuo vya ufundi) hufanya vizuri sana? Mbona wanabaohataika kuingia vyuo vikuu na daraja la Tatu la NECTA hufanya vizuri ? Jee Chuo kikuu cha waislam Morogoro kinaendeshwa na wasiokuwa waislam? mbona vyuo vikuu vya Zanzibar navyo vimejaa waislam na Wazanzibar huku wengine wakikosa nafasi? Mbona idadi kubwa ya wakufunzi wa vyuo hivyo vya Zanzibar ni waislam na vinaendeshwa kwa uwezo mkubwa pengine hata hivi vyuo vikuu vya madhehebu ya dini?
  Nilipata kuongea na wanafunzi waliofanya mtihani 2011, waliofutiwa na waliobahatika kupenya kwenye tundu la NECTA. Wengi wamefikia hatua ya kuwataka walimu sasa watumie njia ya kuwafundisha wanafunzi wao jinsi ya kuujibu mtihani uliovuja ili majibu yasilengane kati ya mwanafunzi na mwanafunzi, wanaamini NECTA haiwezi tena kufanya mtihani uwe salama. Jee hali ikifikia hivi, nini tutegemee taifa letu kielimu?
  .Uaminifu kuanzia baraza la mitihani hadi kumfikia mwanafunzi wanataka uchunguzwe kwa makini, Baraza la mitihani linatakiwa litupiwe jicho kali na wabunge , wanaharakati na hata vyombo vya habari, vyenginevyo tutegemee maafa makubwa ya elimu kwa vijana wetu, sio kwa upande wa Zanzibar hata Tanzania bara. Ni vigumu kupatikana mtihani Zanzibar usivuke bahari.
  Inaonekana NECTA haipo tayari tena kubeba lawama juu ya yale wanayoyatenda wenyewe na kuwabebesha mzigo huu wanafunzi na wazee jambo ambalo ni hatari kwa taifa letu. NECTA inaonekana haitaki kukiri kwamba baadhi ya watendaji wa baraza hilo sio waaminifu katika swala la kutunza mitihani, haitaki kukiri kwamba njia wanazotumia kuitunza nz kuisambaza mitihani inakasoro, wanachofanya sasa ni kuwachukulia hatua kali wanafunzi wanaohisi tu wamedanganya kwenye chumba cha mtihani huku kuvuja mitihani sio tena ajenda yao, pengine wanahisi wakijiingiza kwenye matamko ya uvujaji wa mitihani wengi wataziacha ofisi hizi za umma kutokana na matamko yatayofuata ya wanaharakati na vyombo vya habari, sasa wanasema "liache liende tu zikija karatai zao za majibu mkononi mwetu tutawaadhibu ili tulinde Unga wetu" hata wakipiga kelele hazitozidi za wabunge na wanaharakati. Hii ndio NECTA iliopewa jukumu la kusimamia maisha ya watoto wetu .
  Tukumbuke baadhi ya wabunge waliwahi kulituhumu baraza hili kwamba haliwezi kuutunza mtihani, kwa hivyo baadhi ya watendji wake waondoshe hasa Dk Ndalichako , haya ndio matunda ya baraza hilo kwa watoto wetu ya kufutiwa matokeo huku uzembe ukianzia kwenye baraza. Hii ni hatari kwa taifa changa kama letu ambapo njia pekee ya kumkomboa mtoto ni elimu.mwanafunzi anaeshtumiwa tu amekopi adhabu yake miaka mitatu kutofanya mtihani, jee kijana huyu mdogo aliebeshwa zigo la NECTA afanye nini? Lakini kwa bahati mbaya sijawahi kumsikia afisa yoyote wa NECTA akipewa adhabu ya kutokana uvujai wa mitihani, wapo an wanaendelea kupeta huku watoto ndio muhanga wa uzembe wa NECTA. Sote tunajua mtihani ni swala nyeti, ndio maana vyumba vyote vya kuhifadhia mitihani kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu vinaulinzi mkali, komputa inayotumika kuchpiwa mtihani haitakiwi iguswa na asiehusika .
  Shule nyingi za Zanzibar zimefutiwa matokeo, shule ya Kiislam Unguja kati ya 52, ni 1 tu alesalimika, Shule ya kiislam pemba wao wote wamesambaratika, Hamani, Sufa, High view, Lauret , Jangombe, regeza mwendo na nyengine nyingi zimekubwa na sakatata. Hili tujiuilize kwanini iwe 2011 na isiwe 2010, 2009 au hata 2007?
  Hoja kubwa ya Dk Ndalichako kwamba walimu an wasimamizi wamehusika kwa kiasi kikubwa, swali la kujiuliz, hivi nani anateu wasimamizi hawa?
  Hawa si ndio wasimamizi wanaoaminika na NECTA na kufanya vizuri kila mwaka? Iweje 2011 wabadilike an waungane na wanafunzi kuihujumu NECTA?lakini hata huo ushahidi wa NECTA kuwafutia wanafunzi wameupata wapi? Hawa si ndio waliokusanya na kuupeleka NECTA?au tuseme maofisa wa NECTA walifunga kambi Zanzibar?au tuamini NECTA waliafnya maamuzi haya wakiwa juu ya meza bila ya ushahidi makini?
  Lakini pia hoja ya pili kwamba wanafunzi wakipeana vikratasi kwenye chumba mtihani. Hapa tunatakiwa tujiulize, chumba(bwawa) chenye wanafunzi 100 wakipena karatasi chumba hicho kitakuwa hali gani? Sio fujo, kelele za peleka hapa niletee hiyo? Jee usalama wa mitihani ulikuwa wapi tena hapo? Hawa waliosalimika walikaa vyumba vya pekee yao?polisi waliopewa ulinzi wa vyumba vya mtihani walikuwa likizo?
  Pia hoja kwamba majibu ya wanafunzi yanalingana katika shule moja nayo ni hoja inayohatiji ufafanuzi zaidi, ni vigumu kama majibu haya hayakuandaliwa nje ya chumba tena siku moja kabla ya mtihani, haya sio majibu ya ndani ya chumba kwa masaa matatu.
  Juhudi za pamoja zinatakiwa ili kuwakomboa watoto wetu kielimu, njia pekee ni kuangalia upya utendaji wa NECTA.

  mwandishi amejitambulisha ni
  Juma Said

  Mob 0652 013301
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  dk ndalichao huyu mama sijui hii phd kaipata vipi?
   
 3. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nawaomba watanzania wenzangu mpate kutambua NECTA ni chombo makini sana na kwa hakika hakina maamuzi ya kukurupuka...
  Kwa miaka miwili mfululizo(2010,2011),matokeo ya kidato cha nne yamekuwa mabaya sana(nina Imani haijawahi kutokea)..kwa miaka hiyo miwili tu.Tanzania imetengeneza Division Zero zaidi ya 300,000.Hapo tu ilibidi tujiulize,nini shida!!na hiyo inadhihirisha kuna tatizo...kama tatizo lipo kamwe haliwezi kuwa la NECTA au wizara peke yao..Je sisi kama wazazi au walezi tuna nafasi gani ya kubadili matokeo haya?wengi wetu hatuna muda hata wa kujua kama mtoto anaenda shule na pia kujua maendeleo yake kitaaluma(tupo busy na maisha.)
  Pia kumekuwa na wimbi la shule binafsi ambazo ziko tayari hata kununua mitihani na kutafuta majibu na kuwapa wanafunzi wake ili shule ipate matokeo mazuri na kupata jina ili miaka inayofuata BIASHARA IWE NZURI,watanzania hatujui haya?
  Kuna mwaka fulani(kati ya 2002-2004)..shule ya Saint **** ilifutiwa matokeo yake kwa vitendo kama hivyo....bila shaka wengi mnafahamu...
  Pia tufahamu NECTA haina Ubaguzi wowote wa kidini na kamwe haijawahi kutokea(nina imani hiyo)..hivyo waliofutiwa matokeo yao si kwa sababu ya DINI zao ila ni kwa sababu ya vitendo vyao vibaya(mtoa na mpokea rushwa wote wana makosa)...
  Pia kama mlimsikiliza vizuri Dr.Ndalichako siku akitangaza matokeo ya Mwaka 2011..alisema wazi kabisa..anashughulikia matatizo haya kwa pande zote..yani kwa wanafunzi na baadhi ya walimu ambao shule zao zimefutiwa matokeo..pia anatafuta ushauri elekezi toka ofisi ya jaji mkuu ili kuweka mambo haya sawa.

  Binafsi nina imani na kazi ya NECTA na ninawapa Pongezi sana na nina waambia wasirudi nyuma,kwa yeyote yule mwizi wa Mitihani adhabu yake ni hiyo ya kufutiwa hadi na wengine mtakapo tia akili.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hii makala imeenda shule sana
   
 5. Najuta Kukufahamu

  Najuta Kukufahamu Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani humjui Joyce vizuri..huyu mama ni kichwa vibaya sana..tofauti na hilo li rais lenu bogus..sema system nzima ya utendaji wa kazi ndio inayo muangusha lakini she's the best!! trust me!!
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kwa sababu anatoa div 1 kwa makanisa? au uzuri wake uko wapi? ufafanue kidogo
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hpa ndalichako kachemka
   
 8. +255

  +255 JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Kwanza tungejua kazi hasa ya NECTA ni nini af ndo tuje tumlaumu Ndalichako!
  Mi nadhani ubovu wa elimu na kufeli wanafunzi unasababishwa na Wizara ya Elimu yenyewe na sio NECTA!
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  sijawahi kuona matokeo ya kushangaza ya mtihani wa taifa yakitolowa kama ilivyotokea haya ya 2011 hapa Tanzania ,nimetembelea nchi nyingi na pia kusikiliza vyombo vingi vya habari vya kimatifa lakini sijasikia popote pale baraza la mitihani lilitumia mkokoto wake kupata matokeo ya mtihani wa taifa kama ulivyotumika 2011.nimesoma darasa la kwanza hadi kumaliza shahada ya pili ya masmo yangu sijabahatika kuona Chuo au taasisi yoyote nchini imetoa matokeo ya mtihani kama ilivyofanya NECTA.
  , Wanafunzi 52 wa chumba kimoja wanafutiwa matokeo na anabaki mmoja!, wanafunzi 150 wa shule moja wanafutiwa wanabaki 10 tena hao waaliobaki wanaambulia daraja la nne!,shule moja inafutiwa, shule ya jirani haiguswi hata kidogo
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hii thread imekaa kidini zaidi ..haina mashiko..
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Dk ndalichako anachuki binafsi
   
 12. +255

  +255 JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Ila huwa kuna nafasi ya kukata rufaa, Je imetumika?!
  Zanzibar wana Wizara yao ya Elimu kwa nini hawana Baraza lao la Elimu au na elimu na swala la muungano?
   
 13. Imany John

  Imany John Verified User

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Wacha unazi wewe!
  Mbona feza wametoa div 1?
  Au wataka kusema hata mtoto wa raisi dini yake ndo tatizo?
  Wacha upuuzi,al-qaem seminary ni yawakristo?
  Mbona wanafaulisha watoto.
  Kiziwi ni kiziwi,hasikii wala hajui kuongea.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  sijabahatika kuona Baraza la mitihani duniani likitoa matokeo ya ajabu kama haya. 100 kati ya 111 wanafutiwa wanabaki 10?
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mkuu hoja zako zingehitaji utafiti zaidi:

  Mkuu kila wakati kuna mambo mapya yanatokea, na si lazima experience yako isaidie katika kila tukio. Namna mbaya ya kujenga hoja eti: "sijawahi kuona popote"
  Mkuu chunguza vizuri chanzo cha mijadala iliyojikita katika udini. Mara nyingi huanzishwa na watu wanaolalamika kuonewa kwa vigezo vya kidini, na karibu mara zote, bila ushahidi bali kuwa na hisia tu. Hoja hizi zinapokuja hujibiwa kwa hoja za kupinga dhana hizo. Binafsi naamnini kuwa uwezo wa mtu kitaaluma hautokani na dini yake, bali kutokana na kipaji alichojaliwa na Mwenyezi Mungu na Mazingira. Mazingira ni pamoja na malezi ya nyumbani na vipaumbele anavyopewa na jamii inayomzunguka ambavyo vitamfanya awe na nidhamu na bidiii katika kujifunza.

  Ndio maana watu wa dini zote tu wana uwezo wa kufanya vizuri, iwapo wamejaliwa vipaji, na wamejilea katika ari ya kutaka kufanikiwa kitaaluma, na wanafanya juhudi kubwa kutafuta mafanikio hayo.

  Tusiwajengee watoto mazingira ambayo hata wakishindwa kuna hoja za kujisamehe, tutawafubaza na hawatajaribu kufanya vizuri. Tuwasisitizie kuwa hakuna njia ya mkato katika kupata mafanikio yoyote yale, na hapa tunaongelea mafanikio ya kielimu.

  Baraza la Mitihani la Taifa linafanya kazi kwa umakini sana.

  Inapotokea kuna suala lolote la udanganyifu katika mitihani ambao unaweza kupelekea kufutiwa matokeo au kufungiwa kituo, huwa hawakurupuki.
  1. Wanafungua faili, na wanalipeleka kwa wataalamu wa upelelezi wa makosa ya kughushi na udanganyigu. (Polisi Makao makuu)
  2. Kitengo hiki kinafanya uchunguzi na kikikamilisha uchunguzi wake kinashauri Baraza kama kuna udanganyifu au la.
  3. Baraza linachukua hatua.
  4. Baraza linatunza mafaili ya upelelezi kama ushahidi kwa watakaodhani haki haikutendeka.

  Vielelezo hivyo na mafaili vipo, na endapo Shule yoyote au kikundi chochote kinadhani kina sababu za kutosha za kupinga hatua za baraza, kuna utaratibu unaoweza kufanyika wa hata wao kwenda pale na kuoneshwa ushahidi huo.

  Tume nyingi tu zimeshaundwa kushughulikia malalamiko kadhaa yaliyokwisha tolewa kuhusu utendaji wa baraza, lakini zote zimetoka zimeridhika na utendaji huo.

  Hivi karibuni, Wanasiasa na wanaharakati wa Zanzibar walikaribishwa na Baraza kujionea udanganyifu uliofanywa na watoto wa Sekondari za Zanzibar ambao ulipelekea kufutwa kwa matokeo ya wanafunzi 1200. Wanasiasa hao na wanaharakati walitoka wameridhika, kama inavyoonesha kauli hii ambayo Waziri wa Elimu wa Zanzibar aliitoa kwenye Baraza la Wawakilishi: Kumbuka Waziri wa Elimu wa Zanzibar ni Muislamu na anawakilisha maslahi ya Wazanzibar ambao walikuwa na jazba sana baada ya matokeo hayo kufutwa.

  SMZ yakubali wanafunzi 1,200 wafutiwe matokeo
  Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 4th April 2012


  HabariLeo | SMZ yakubali wanafunzi 1,200 wafutiwe matokeo


  SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imekubaliana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kwa hatua yake ya kuwafutia matokeo ya mitihani ya kidato cha nne wanafunzi 1,200 kutoka Zanzibar baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwa kushirikiana na wasimamizi wa mitihani.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdalla Shaaban alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe waliopitisha Muswada wa Kuanzishwa kwa Bodi ya kufanya tathimini ya vipimo vya elimu Zanzibar.

  Shaaban alisema SMZ iliwasiliana na NECTA kuhusu kuwepo kwa taarifa za kuvuja kwa mitihani pamoja na wanafunzi wengi wa Zanzibar kufutiwa mitihani yao ya kidato cha nne waliofanya mwaka jana.

  "Tulifanya mawasiliano na kupeleka mjumbe wetu huko, lakini baada ya utafiti ilibainika kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu mkubwa wa mitihani yao baada ya kupata vielelezo mbalimbali," alisema Shaaban.

  Alisema hata hivyo SMZ imeunda chombo kuchunguza suala hilo la kufutiwa kwa wanafunzi wa Zanzibar mitihani ya kidato cha nne, lakini taarifa za awali pamoja na uthibitisho wake unaonesha kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu ambao ni kinyume cha maadili ya mitihani.

  Alisema hivi sasa wanafunzi wengi wanakabiliwa na dhana potofu ya kusubiri kununua mitihani ya taifa ya kidato cha nne na sita na kuacha kusoma kwa bidii.

  Aidha, Shaaban aliwataka wazazi nao kuacha kabisa tabia ya kushawishiwa na watoto wao kununua mitihani ya taifa, kwani kufanya hivyo madhara yake ni makubwa ikiwemo kufutiwa mitihani ya taifa.

  Akijibu hoja za wajumbe, Shaaban alisema SMZ haina mpango wa kujiondoa katika Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwani chombo hicho kipo kwa mujibu wa sheria kikiwa ni taasisi ya Muungano.

  "Hatuna mpango wa kujiondoa katika chombo cha NECTA......tumeunda Bodi ya kuangalia tathimini ya vipimo vya elimu, lakini haina maana kwamba tunajiondoa katika Baraza la Mitihani la Taifa," alisema.

  Wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi waliochangia muswada huo waliitaka Zanzibar kujiondoa NECTA baada ya kuwepo tuhuma za kufutiwa mitihani yao taifa kidato cha nne wanafunzi wengi kutoka Zanzibar.


  Hata wewe unaweza kwenda na wawakilishi wako ujiridhishe kuwa haki imetendeka.

  Mitihani haivuji siku hizi kama ilivyokuwa zamani kabla ya Dr. Ndalichako kuongoza Baraza. Kinachofanyika ni Walimu kuchukua karatasi wakati wa mtihani na kusaidia wanafunzi, na ndio maana inatokea katika shule chache. Uchunguzi umefanyika na ushahidi wa polisi upo, pia wahusika walihojiwa wakakiri, na walimu wasio waaminifu wamechukuliwa hatua.

  Hii lazima tumpe credit Dr. Ndalichako, udanganyifu wa zamani wa mitihani kuuzwa mitaani haupo tena, imebaki ni udanganyifu kwenye vituo na vyumba vya mitihani.
  Tume imeundwa, imefanya uchunguzi na imeridhika kuwa kila aliyefutiwa matokeo hakuonewa. Tume ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunge wa bara na Zanzibar, maafisa elimu, viongozi wa dini, walimu na wazazi.

  Namnukuu tena waziri wa Elimu wa Zanzibar:
  "Tulifanya mawasiliano na kupeleka mjumbe wetu huko, lakini baada ya utafiti ilibainika kwamba wanafunzi wamefanya udanganyifu mkubwa wa mitihani yao baada ya kupata vielelezo mbalimbali," alisema Shaaban.


  What?
  Kazi ya NECTA ni nini, si ni kupima jinsi wanafunzi walivyoelewa. Kazi inafanyika mashuleni, na hamasa inatoka kwenye familia.

  Njia ya kujikomboa kielimu ni kwanza kukubali kwamba kuna tatizo katika mfumo wetu wa elimu. Kufanyia kazi hayo matatizo hasa katika mashule yetu. Wanafunzi wakijifunza vizuri, NECTA haitawanyima haki yao.

  Mtoa hoja anatarajia kuwa NECTA wanapasika wafaulishe wanafunzi hata kama hakuna walichoandika.

  Tusidekeze watoto wetu, bali tuwasisitizie kuwa Juhudi ni shina na Maendeleo.

  Of course NECTA kama binadamu nao wajitahidi kuboresha mapungufu yao, nami naona wanajitahidi.
   
 16. K

  Kijamba Koti Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni upumbavu,mnataka ajivue gamba kwa misingi ipi?
   
Loading...