Kwa hili; CHADEMA hawakutenda Vyema, Walikosea!

Kwa hili; CHADEMA hawakutenda Vyema, Walikosea!

Hivyo vyombo habari vinavyoshabikia wakati hata tukio la mkutano lenyewe havikuripoti inaonekana vipo biased.Kwani kuna sehemu CDM walisema watu watukane,ila mi nahisi hayo matusi yanatokana na hasira walizo nazo wananchi juu ya hawa viongozi.Ila bado tuendelee kuwa kumbusha wajibu wao kama viongozi wa vyombo muhimu kama hawatki kupigiwa simu na wananchi basi waachie nyadhifa zao
 
Vyombo vya habari vya Tanzania ni hatari kwa mustakabali wa amani na demokrasia ya nchi yetu.Ningependa kuwaasa wanahabari wawe makini,Tanzania kwanza mshiko baadaye.Maana machafuko yakitokea hata huo mshiko hautakuwepo.

Siku CCM ikiondelewa madarakani kaka na dada zangu waandishi wa habari mtakuwa upande upi?Je mtawaambia nini watanzania?Kuwa mlitumwa na uongozi mfanye hayo.Chondechonde waandishi tusaidieni watanzania wa kawaida kujua haki zetu za msingi bila kuleta mtafaruku.Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu,kwani kuna siku yaja mtajisuta na matokeo yake kuwa mabaya.
 
unafikiri wangekuwa wema kuna mwanachi angewatukana?

wakae wajitafakar kwa nn hawapendwi
 
Mie nilikuwa na hamu ya kuwasiliana na DADA huyu, Anna Makinda.
Asante CDM
 
Haki haiji kirahisi jamani. Tulianza kutoka nje ya bunge tukafanikwa kiasi, tukaja kulazimisha kuonge hata bila kupewa nafasi nayo ikatusaidia. Sasa tumekuja na kuweuka bungeni i.e tunatunga kibwagizo hapo hapo na kukiimba huku bunge linaendelea. Baada ya hapo tutakuja kivingine kama bado hatutaeleweka. Hiyo ya kumtukana Bibi siyo kali sana kwakuwa yeye mwenyewe anajua watu hawampendi so hata wasipomtukana ni kama katukanwa.
 
Tangu chama cha Demokrasia na maendeleo kifanye mkutano wa kuhamasisha wananchi kuwawajibisha Viongozi/watawala wao, kuna wengine wametumia mwanya huo kufanya ndivyo sivyo. Hali hii imeleta mtafaruku kati ya jamii na baadhi ya asasi pamoja na watawala.

Kwanza niseme wazi kuwa mwananchi kufanya mawasiliano na mtawala wake kwa njia yoyote ile ni haki yake ya msingi, hivyo CDM kugawa namba ya viongozi hao haikuwa dhambi ukizingatia kuwa namba za mawasiliano yao zilikuwa wazi katika mitandao na kwenye ofisi zao hata kabla ya mikutano hiyo ya CHADEMA kufanyika. Hivyo kitu cha msingi hapa ni kulaumu watu waliotumia namba hizo kwa matumizi mengine na si yale ambayo yalikusudiwa.

Makinda na Ndugai kama binadamu wengine wanaweza kukosea katika maamzi yao, na pale walengwa wanapoona kuwa hawajatendewa haki wanayo sababu ya kupaza sauti ya kudai haki yao (Ila si kwa njia ya matusi kama ilivyotokea). Nina imani Viongozi wa CHADEMA waliwatuma watu wakapaze sauti zao au kuwauliza watawala wao kuwa haya mnayoyafanya ndiyo tuliyowatuma?!na si kuwatukana. Sasa kama kuna mtu amefikia hatua ya kutoa lugha za matusi au vitisho vya namna hiyo, sasa hiyo ni kazi ya vyombo vinavyohusika kuwafuatilia wahusika na kuwawajibisha kwa mjibu wa sheria za nchi.

Angalizo: katika suala hili, vyombo navyo vya habari vimejikuta vikitumbukia katika sakata hili na kuanza kulaumu CHADEMA kama vile ndicho kimesema watu wafanye hivyo. Hili suala linafaa kuangaliwa kwa kina ukizingatia kuwa hata vile vyombo ambavyo vimekuwa kipenzi cha wasikilizaji wengi, sasa vinatumiwa kama vyombo vya propaganda kwa watawala na serikali iliyopo madarakani.

TUKUMBUKE KUWA SEHEMU NYINGI ZIMEKUMBWA NA MACHAFUKO KUTOKANA NA SERIKALI TAWALA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUPOTOSHA UKWELI.

TUKUMBUKE KUWA: Maandiko yanasema kuwa atendaye mema hulakiwa kwa ndremo na vifijo, na Yule atendaye maovu huzomewa na hata asipate pa kuficha uso wake.

Tafakari.

Tatizo si matusi,unapomwita mtu chongo ilihali si chongo hilo ni tusi,lakini kama ana chongo basi ana stahili kuitwa chongo.Makinda na mwenzake wanayo yapata kwa sasa ni matokeo ya kujitakia,cha msingi arudi kwa wananchi kama mwajiriwa wao na kuomba msamaha ikibidi ajiuzuru.
 
Namba ya spika au naibu wake na pia za wabunge wengine wote siyo jambo la siri. ukiingia kwenye tovuti ya bunge kuna namba za simu za mikononi za wabunge wote pamoja na anuani zao za barua pepe pamoja na physical address, hivyo hata bila ya kutajiwa katika mkutano huo wa hadhara bado namba hizo siyo siri kwa mwananchi yeyote
 
wala hajatukanwa,angetukanwa angeshafanya uamuzi wa kuachia ngazi
 
mwananchi wa kawaida hajui kanuni za bunge. kanuni za bunge zinahitaji kuzisoma kwa ufafanuzi wa kina hasa daarasani. unaweza dhani lissu ameonewa kumbe mwenyewe ndiyo amepindisha kanuni. kumpeleka spika kwenye mahakama ya umma hali ya kuwa umma hauelewi kanuni ni uhalifu na uvunjifu wa haki za binadamu.

viongozi waliotoa namba baada ya kuwapandisha watu jazba, wana kesi ya kujibu.
 
Hayeni jamani. Ngoja tuone tuelekeapo. Ni vyema tuchunge nyendo zetu kama wapinzani ili zisije zikachelewesha mabadiliko kwa kuibua visa na mikasa isiyo makinika
 
Tusitumie hizo simu kutukana viongozi wa kitaifa, bali tutumie simu kumwonyesha Anna Makinda na Job ndugai kwamba kiti walichokikalia sio mali ya ccm bali ni mali ya umma wa watanzania bila kujali vyama vya siasa.wanachofanya makinda na Ndugai ni kudhoofisha nguvu ya chadema

Makinda aonyeshe matusi aliyotukanwa,hapakuwa na njia nyingine zaidi ya live democracy kwa vile parliamentary democracy imejaa ushabiki wa uccm
 

Kamanda Lema akitaja namba za Spika Makinda baada yakuambiwa na Zitto aliye simama karibu yake.
Katika mkutano wa CHADEMA Temeke juzi aliyetaja namba za simu za Spika na za naibuSpika ni Kamanda Lema ,lakini Zitto ndiye aliyemuambia azitaje ,je Zitto hananamba za Spika ??au alitaka nini kumuambia Lema azitaje namba za Spika??Miminafikiri :
Kwanza-nafikiri kuna jambo hapa ,ZZK bado anaamini ananafasi ndani ya CCM na hataki kwa namna yoyote ile kujenga uadui na Spika nawakuu wa CCM kwani anajua nafasi yake ndani ya CCM itategemea watu hao.
Pili-ZZK aliamini kumwambia Lema azitaje namba hizoatamuingiza Lema kwenye matatizo kwani kama namba hizo zikitumika ndivyo sivyolabda Lema anaweza kuhojiwa au kusumbuliwa na ppolisi
Yapo mengi ya kujiuliza hapa kwa nini ZZK hakutaja hizonamba yeye mwenyewe
Bado naamini ZZK ni mwanachama wa CDM mwenyemapenzi na CCM

si kweli, huwezi kutoa hotuba huku una tablet, ipad au palmtop. Mbona alisoma zingine? Acha upuuzi kaka Minja
 
Ndio jamii yetu ilivyo, umekasahau kale kapuuzi ka 'unawashwawashwa' kaMabumba! Ukimtumia Ndugai ama Makinda ni tusi? Kama tusi mbona hako kaliitoa?
 
Wenzangu WanaJF,

Nikiwa mnazi mkubwa wa mabadiliko yasiyoogopa gharama yoyote, naomba niwe kinyume na hili walilolifanya viongozi wa Chadema katika maandamano ya juzi kwa kile walichokiita kumshinikiza Anna Makinda Angoke kwenye kiti.

Kwa ujumla kila kitu kilifanyika vyema kabisa, hata kutoa namba za Anna Makinda kwa wananchi na dunia nzima bado ilikuwa sahihi. Viongozi wa Chadema, Zitto na Lema, walizisoma namba za Makinda waziwazi bila hata kificho. Hilo bado sioni kama lilikuwa tatizo.

Tatizo kubwa nilionalo ni kwamba, viongozi hawa hawakuwapa elimu wananchi kama namba zile zilikuwa zina umuhimu gani hasa. Wananchi hawakuelimishwa kuwa namba zile zilikuwa za kutuma maoni kwa Anna Makinda, maoni ya busara na yasiyo na matusi.

Katika hali ya namna ile, wananchi wataanza kumtukana Spika Makinda, bila hata kujua kama ni kiongozi mkubwa wa nchi. Wananchi wangetakiwa waelimishwe umuhimu wa kumhitaji Anna Makinda ajiuzulu lakini kwa lugha yenye staha na maneno ya hoja.

Ni wazi kuwa, kwa mfumo wa mawasiliano wa nchi yetu, bado wengi waliweza kutumia kadi za simu zisizosajiliwa na kumvurumishia Spika matusi (kama gazeti moja lilivyokwisha kuripoti).

Yawezekana bado hajatukanwa, ila yawezekana akatukanwa pia. Sharti tukubaliane kuwa watu hawakuelimishwa kuwa kuna madhara (repercussions) iwapo watamtumia jumbe za matusi. Ikiwa jumbe alizokwisha kutumiwa (au atakazotumiwa) zitakuwa zina matusi, hili litahafifisha hoja ya msingi ya Chadema kutaka kumng'oa Makinda (jambo ambalo mimi binafsi nisingependa litokee).

Kwa Chadema kutowaelimisha wananchi namna bora ya kumwandikia Makinda/Ndugai ujumbe, hili ni kosa; na matusi yote atakayotukanwa Makinda (maana kweli watu wamemchukia) itakuwa ni lawama kwa Chadema. Kwa kweli, bila ushabiki, kwa hili Chadema walikosea.

PEOPLES POWER!!

Ulitaka viongozi wa CDM wafanye semina elekezi ya siku 3 ndio uonekuwa hawakukosea. Kumbuka kauli ya viongozi wa CDM iliwataka wananchi kumtumia sms au kupiga simu ili kumshinikiza spika ajihuzuru hawakuwataka wananchi kumtukana Spika.
 
mwananchi wa kawaida hajui kanuni za bunge. kanuni za bunge zinahitaji kuzisoma kwa ufafanuzi wa kina hasa daarasani. unaweza dhani lissu ameonewa kumbe mwenyewe ndiyo amepindisha kanuni. kumpeleka spika kwenye mahakama ya umma hali ya kuwa umma hauelewi kanuni ni uhalifu na uvunjifu wa haki za binadamu.

viongozi waliotoa namba baada ya kuwapandisha watu jazba, wana kesi ya kujibu.

Fafanua amepindisha kanuni ipi?
 
Ni kweli hatuna uhakika kama Anna Makinda ametukanwa, but ninachokiona ni nanna tu anatakaaa wananchi wamuonee huruma yule mama ni mchawi wa maaendeleo ya democrasia ya nchi yetu anataka tuishi kama miaka ya 1950 kama vipi atuoneshe hizo sms nasi tujiridhishe pia anastahili kutukanwa.
 
Back
Top Bottom