Kwa hiki mlichonifanyia Airtel, lazima niwapeleke Mahakamani

MNYWABUJU

JF-Expert Member
Sep 6, 2018
260
327
Habari wana jamvi , kama mada hapo juu mimi ni mtumiaji wa mitandao mingine, lakin juzi kati niliamua kusajili line ya airtel kwa matumizi ya airtel money, ni wiki ya pili niliweka fedha katika account yangu kwaajili ya kununua umeme na kifurushi cha mb cha sh 1000.

Lakini sikupata kifurushi ,na pia hela yangu ikakatwa ,bila kupata kifurushi, nimeshawasiliana na huduma kwa wateja, lakini wananipanga tu zaidi ya mara sita.

Kilichoniudhi saa hizi, nikiwapigia simu wanakata, nafikilia kuwapeleka Mahakamani mpaka wiki hii wasipo,nilejeshea salio langu au wanipe kifurushi.
 
We jamaa karibu AIRTEL inawezekana hujui menu so

mimi ni mteja wa kudumu tangu enzi za Celtel na sijajutia kama hiyo mitandao mingine, nina line zao kwa ajili ya kupokelea simu tu.
Yaani kiongozi ,wamekata hela yangu afu kifurushi sijakipata
 
Huo mtandao ni wa hovyo sana wanajifanya the smartphone network lakini wapi ukiweka kifurushi cha data kuna namna wanaminya speed yani picha ya kb80 unaweza ipakua kwa dakika nzima.

1 Vodacom
2 Hallotel
3 Tigo
4 Zantel
5 airtel
 
Huo mtandao ni wa hovyo sana wanajifanya the smartphone network lakini wapi ukiweka kifurushi cha data kuna namna wanaminya speed yani picha ya kb80 unaweza ipakua kwa dakika nzima.

1 Vodacom
2 Hallotel
3 Tigo
4 Zantel
5 airtel
TTCL ???
 
Elfu moja lazima iwe na sh. 20 zamani ilikuwa sh.11, ila airtel ukinunua umeme hawarudshi SMS ya kujulisha kiasi kilicho tumika na kilichobaki, na nilishawahi uliza kwenye ofisi lakini sijawahi pata jibu
 
Back
Top Bottom