Mimi (jina nahifadhi) nafanya kazi na Kampuni moja hapa Posta inayojishughulisha na ushauri yaani Consultancy in Risk Management na naeleza na kufafanua kama ifuatavyo:-
1. Kwamba, kitaaluma mimi ni mwanasheria hivyo nina uelewa wa kutosha wa utaratibu au mienendo (procedures) kwenye maswala haya ninayoyaandika.
2. Katika nafasi yangu kama nilipata kubaini kwamba wateja wa huduma ya Airtel Money wanaibiwa pesa kutoka kwenye akauti zao kwa kiwango kikubwa pasipo wao kujua kutokana na sababu ambazo tulizijua baada ya kufanya uchunguzi wa kina.
3. Tulianzisha uchunguzi wa chini kwa chini na kubaini kwamba tatizo lipo kwenye mfumo wa kulinda namba ya siri (PIN) ya mteja kwa maana kwamba kwa kawaida akauti ya mteja inatakiwa ifunge endapo mtu akikosea namba ya siri mfululizo zaidi ya mara tatu katika mitandao mingine lakini mara sita kwa akauti ya Airtel Money cha ajabu ni kwamba akaunti hiyo ya Airtel ilikuwa inafungua badala ya kufunga.
4. Tulibaini pia kwamba wezi wanatumia fursa hii kuwaibia wateja wa Airtel Money kwa kukosea makusudi namba ya siri ya mteja mara sita kisha akaunti inaruhusu kuweka namba ya siri mpya na kutoa pesa bila mhusika kujua.
5. Kwamba mnamo tarehe 7/5/2018 tuliwasilisha matokeo ya awali ya uchunguzi kwa Mkurugenzi wa Airtel Tanzania kama mtoa huduma ili waweze kuzuia uwizi huu chini ya kifungu cha 45 cha Cyber Crime Act, 2015 na kifungu cha 4(1) (a) na (b) cha Whistleblower and Witness Protection Act, 2015.
6. Baada ya siku tatu toka nilipowajulisha nilirudi tena kwao maana niliangalia nikaona hakuna marekebisho walofanya kisha walisema kwamba wanafanya uchunguzi wa ndani kwamba inawezekana kuna njama kati ya watumishi wao na watu wa nje ili kuwaibia wateja.
7. Lakini badala ya Airtel kuondoa tatizo baada ya kupokea taarifa hizi wao wamepamba tatizo ili ionekane nzuri kana kwamba wameiweka makusudi. Walichokifanya ni kwamba wamerekebisha mfumo wao kiasi kwamba kama akaunti ina hela kuanzia shilingi moja basi akaunti itafunga lakini kama haina salio lolote basi akaunti itareset ukikosea namba mara sita.
8. Baada ya zaidi ya wiki tatu walinipigia simu kunieleza kwamba waliweka huo mfumo makusudi ili kuwawezesha watu wa vijijini kurudisha namba zao za siri wakizisahau bila kusumbuka kwenda ofisini. Jibu hili nimepewa juzi ambapo ni baada ya zaidi ya wiki tatu toka nilipowapa barua na licha ya ahadi za hapa na pale kwamba wanafanya marekebisho.
9. Wamerekebisha pia kwamba kama ukireset namba ya siri kwa njia hii ya kukosea namba makusudi, kama una uwezo wa kukopa Timiza basi utazuiwa kukopa mpaka baada ya saa 24 tokea pale ulipofanya reset hii kinyume na maumbile.
10. Licha ya marekebisho haya tatizo bado liko pale pale kwa maana kwamba kama akaunti yako haina salio mtu yeyote anaweza kukosea namba yako ya siri mara sita kisha anaweka namba aipendayo yeye kisha mwenye namba ndo atakuwa hajui namba yake ya siri na kisha kusubiri baada ya saa 24 na anaweza kukopa kwenye Timiza kupitia akauti yako bila wewe kujua.
11. Licha ya Timiza miamala ya pesa pia ni faragha na sheria inaweka wazi hilo hivyo hata kama akaunti haina kitu ni kinyume cha sheria kwa mtoa huduma kuruhusu makusudi udukuzi na uingiliaji kutoka nje kwenye miamala ya mteja na ina madhara makubwa sana hasa kwa wanandoa ambapo mmoja anapoangalia miamala ya mwandani wake kisha anakuta pesa ilitumwa kwa mchepuko kwa mfano madhara yake yako wazi hayahitaji maelezo ya ziada.
12. Akauti ya Airtel Money pia inaweza kutumika kuvutia pesa kutoka benki hivyo mtu bado anaweza kuvuta pesa ya mteja kutoka benki hivyo huu utaratibu wa Airtel wa makusudi kama walivyosema inarahisisha uwezekano wa kuvuta pesa ya mteja kupitia akauti ya Airtel Money.
13. Sikushangazwa na jibu hili maana Airtel walikuwa wanatafuta jinsi ya kupamba tatizo ili ionekane wako sawa na hivyo kuficha udhaifu wao mkubwa ilopelekea watu wengi kuibiwa bila wao kujua, badala yake limeleta maswali zaidi ya majibu, nimewaomba wanipe haya majibu kwa njia ya maandishi ila wamegoma an nimewauliza maswali kama ifuatavyo lakini wamegoma kunijibu:
A. Kwanza kureset namba ya siri ukisahau huhitajiki kwenda ofisini bali unapiga simu huduma kwa wateja ambao watakuuliza maswali kisha wanareset akaunti yako kisha unaweka namba mpya, sasa hao watu wa vijijini hawawezi kupiga simu ambayo pia ni bure?
B. Hao watu wa vikijijini wanajuaje hii huduma wakati imegubikwa na upotoshwaji kiasi kwamba meseji ya mrejesho inaonya kwamba akaunti itafunga ukikosea zaidi ya mara tano lakini mwisho wa siku inareset?
C. Kwa nini ujumbe mrejesho usioneshe kwamba namba ya siri itareset ukikosea mara kadhaa kama akaunti haina hela kwa nini inamislead?
D. Hata wakirekebisha kwa kufunga akaunti yenye hela je, namba ya siri ya akauti ambayo haina hela haipaswi kulindwa inaruhusiwa kuchezewa na yeyote?
E. Kwa nini utaratibu huu wa kubadilisha namba ya siri unakiuka utaratibu wa kawaida ambao pia upo kwenye menu ya Airtel Money ambapo mteja anapaswa kuweka namba ya siri ya zamani kabla ya kuruhusiwa kuweka namba mpya?
F. Kama lengo ni kuwasaidia watu wa vijijini wabadili namba zao za siri kienyeji ni kwa nini isiwekwe huko vijijini kwenyewe kwa nini ipo mpaka mjini?
G. Kama jibu lilikuwa ni rahisi hivi walikuwa wanafanya uchunguzi wa nini na walishindwa nini kunibu siku ile ile nimewapa barua?
14. Pia kuna maidhaifu yao mengine inayopelekea pesa za kampuni kuibiwa ambayo mpaka sasa naziandikia kitabu lakini udhaifu huu namba ya siri unapelekea kuibiwa pesa za mteja na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kulikuwa promotion na miradi kama (1) Hakatwi Mtu Hapa (2) Hatoki Mtu Hapa (3) Timiza Loan Facility (4) Timiza Wakala Loan ambayo ilibidi isitishwe kabla ya muda au kufanyiwa marekebisho makubwa ndipo ikaendelea. Kwa mfano vocha ya BURE PARK kama mtaikumbuka ilibidi iranguliwe na Airtel yenyewe kutoka sokoni kutokana na hasara kubwa iliyopata kampuni kutokana na madhaifu ya vocha hizo na hiyo ilipelekea bei ya hizo vocha kupanda kutoka bei halisi ya 1500 mpaka zaidi ya 50,000. Vocha hizi zilikuwa almasi kwa mawakala ila hii siyo mada ya leo.
Hitimisho
15. Nahisi kuna kitu hapa zaidi ya kuficha madhaifu ya kuambiwa ukweli hivyo ndani ya siku chache zijazo nitafungua kesi mahakamani kuishaki Airtel kwa kiuka haki mbali mbali za mlaji pia mteja yeyote anaruhusiwa kujitokeza kuungana nami katika kesi hii kwa (1) Kuhatarisha usalama wa pesa za mteja (2) Kuhatarisha taarifa za siri za miamala ya mteja kinyume cha sheria (3) Kutuma ujumbe wa kupotosha makusudi kwamba akauti itafunga ukikosea namba ya siri mara kadhaa huku ikijua siyo kweli (4) Kubagua wateja makusudi kwa kufunga akauti zenye kiasi fulani cha pesa na kureset akaunti ambazo halina salio. (5) Kuvunja mkataba wa usiri kati ya mtoa huduma na mteja kwa kuruhusu mtu yeyote kubadili namba yangu ya siri na hivyo kuweza kufanya chochote na akauti yangu. Lakini pia mnaruhusiwa kuchangia nini kifanyike kukomesha tatizo lisiendelee ili wengine wasiibiwe hasa tukijikita kwenye mada ya kufungua kesi ya pamoja.