Kwa haya ya Trump, ina maana Obama aliharibu mbaya!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kwa mambo anayofanya sasa hivi, D.Trump akiwa na siku chache tu madarakani, kwa kumbukumbu zangu sijawahi kuyashuhudia tangu nimeanza kujua na kufwatilia Siasa za USA!
Jamaa ametumia excutive order mpaka sasa hivi kusimamisha mambo aliyopitisha Obama karibia 10 hivi, na haya ndo aliyokampenia na kushinda hivyo ina maana basi Obama alikuwa ameharibu sana kupita kiasi, kwa maana sijawahi kuona, Raisi wa USA ambaye hata wiki moja hajamaliza kusimamisha mambo mengi alio yakuta ktk kwa mtangulizi wake!

Msemaji Mkuu wa Raisi wa USA Sean Spicer!
Sean-Spicer-Holds-Daily-Press-Briefing-At-The-White-House.jpg

Donald J. Trump (@realDonaldTrump) | Twitter
 
Hilo linajulikana lkn siyo kwa spidi hii ya Trump, Maraisi wengi huja na mipango yao na hubadilisha mambo lkn huchukuwa muda, D.Trump siku ya kwanza tu amesimamisha mambo ya Obama mengi tu, hii sijawahi kuona!

Ndio maana nimesema kila mtu ana vipau mbele vyake.
 
Na hiyo ndio tofauti ya mwanasiasa na mtu wa vitendo. Trump anaamini kwenye actions zaidi kuliko maneno matupu.

Kama ahadi zake ndio zimempatia urais inabidi atekeleze, miaka minne sio mingi atakabiliwa na kampeni punde.
 
Kila zama na kitabu chake kwani mwenyekiti wenu si kasi yake ni ya kuvuruga ya aliyepita ili kuonesha hakufanya kitu?
 
Hilo linajulikana lkn siyo kwa spidi hii ya Trump, Maraisi wengi huja na mipango yao na hubadilisha mambo lkn huchukuwa muda, D.Trump siku ya kwanza tu amesimamisha mambo ya Obama mengi tu, hii sijawahi kuona!

Kwa mambo anayofanya sasa hivi, D.Trump akiwa na siku chache tu madarakani, kwa kumbukumbu zangu sijawahi kuyashuhudia tangu nimeanza kujua na kufwatilia Siasa za USA!
Jamaa ametumia excutive order mpaka sasa hivi kusimamisha mambo aliyopitisha Obama karibia 10 hivi, na haya ndo aliyokampenia na kushinda hivyo ina maana basi Obama alikuwa ameharibu sana kupita kiasi, kwa maana sijawahi kuona, Raisi wa USA ambaye hata wiki moja hajamaliza kusimamisha mambo mengi alio yakuta ktk kwa mtangulizi wake!

Msemaji Mkuu wa Raisi wa USA Sean Spicer!
Sean-Spicer-Holds-Daily-Press-Briefing-At-The-White-House.jpg

Donald J. Trump (@realDonaldTrump) | Twitter
Umeshindwa nini kuona na kuhisi kuwa shida yaweza kuwa kwa Trump?
Inabidi utafakari sana kabla hujafuta mambo yote hayo ya mtangulizi wako haswa kama, kwa system ya Marekani hayajapigwa pini na Senate.
 
Hilo linajulikana lkn siyo kwa spidi hii ya Trump, Maraisi wengi huja na mipango yao na hubadilisha mambo lkn huchukuwa muda, D.Trump siku ya kwanza tu amesimamisha mambo ya Obama mengi tu, hii sijawahi kuona!
Hujawahi ona kivipi hata hapa Ukawa wangechukua ungestaajabu ya Musa....
 
Umeshindwa nini kuona na kuhisi kuwa shida yaweza kuwa kwa Trump?
Inabidi utafakari sana kabla hujafuta mambo yote hayo ya mtangulizi wako haswa kama, kwa system ya Marekani hayajapigwa pini na Senate.

Lakini yote aliyoyafanya mpka sasa ndiyo aliyoyaahidi kwenye Kampeni zake, hivyo ina maana amechaguliwa ili ayafanye anayoyafanya, na alikuwa anasema akiingia siku ya kwanza atafanya abc, na ndivyo inavyotokea, sasa iweje usema shida iko kwa Trump?!
 
Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa huyu Obama mambo mengi alikuwa anayafanya kwa Executive Orders.

Obama alipoteza control ya senate (Senators).... Sasa akawa anajifanyia mambo yake wa orders tu...

Trumps anachofanya ni sahihi kabisa...kutengua yale mambo yote ambayo hayana Senate (Senators) approvals
 
Back
Top Bottom