Kwa haya ya Mwanza, kuna bomu linatengenezwa

Kwa haya ya Mwanza, kuna bomu linatengenezwa

Ccm kwisha habari yao! watu wanafuata fiesta! ama nene!!
 
kwa Akili yako mtoa uzi hivi hawa wote wanao onekana star tv unaweza kuwalipa? muache ujinga bana hata kama ni ushabiki tuweke pembeni bana!!!!

Mbona mnasema Lowssa anaye jaza watu mara tano zaidi ya hao wa Magufuli kuwa anawalipa !

Kama kwa hao wachache wa Magufuli unaona haiwezekani, Inakuwaje kwa maelfu ya Lowassa?

Acheni huo u double standard.
 
Mm nasema cku ya kupga kura hakuna lorry litakalombeba mpga kura
 
Nimemsikiliza hotuba yake karibia yote alikua akiongelea barabara madaraja na ferry tu...mara sasa unaweza kutoka mtwara hadi mwanza kwa tax. Jamaa bado hajui wajibu wake kama raisi...!
 
Haikwepeki. Lowasa ndiye Rais kwa mahaba ya Watz. Bwana Pombe na chama changu CCM tukubali kutokubalika. Enzi imeisha.
 
CCM Mbele kwa mbele.

Nnasikia teja leo madawa yalimzidi akashindwa kuhutubia Tunduma.

Halafu watu walivyo wajinga, eti mzee wa viroba kasimama kusema kuwa mitambo ya kupaza sauti inawakorofisha kajisahahu kuwa anaongea kupitia mitambo hiyo hiyo inayowakorofisha- Majanga!
 
CCM Mbele kwa mbele.

Nnasikia teja leo madawa yalimzidi akashindwa kuhutubia Tunduma.

Halafu watu walivyo wajinga, eti mzee wa viroba kasimama kusema kuwa mitambo ya kupaza sauti inawakorofisha kajisahahu kuwa anaongea kupitia mitambo hiyo hiyo inayowakorofisha- Majanga!

Haingi akilini mtu kukuelewa kwamba kipaza sauti kibovu wakati unakitumia tena kwenye umati mkubwa hivyo. Waongo na wanafiki.

Ushauri wa bure kwa wanachama na washabiki wa UKAWA - TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Hbari za leo Great Thinkers. Leo nimebahatika kuwa jijini Mwanza katika pilika zangu za kutafuta kamuhogo. Bahati nzuri leo pia mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mh. John Pombe Magufuli yupo jijini kwa ajili ya kujinadi.

Wakati na ingia jijini Mwanza nikitokea Musoma , nilipofika Kisesa kuingia mjini nimekutana na makundi ya akina mama wamejikusanya kwenye vituo wakisubiri usafiri wa kuelekea kwenye Rally. Shamrashamra hizo zilikua zina zidi kila ninaposogelea mjini kati. Nilipofika mzunguko wa Nyerere niliamua kupitia barbara ya Pamba ili nishike barabara ya Kenyata...kwenye kituo cha Mafuta pale mkabala na stendi ya kwenda Igombe zilikuwepo bodaboda kama mia hivi zote zinapeperusha bendera za ccm kuulizia nikaambiwa kila bodaboda ilikuwa inawekewa mafuta lita 5, halafu unalamba elfu5 na kuwekewa bendera .

Pale Nyamagana daladala zilikuwa zinashusha watu halafu wanawezeshwa kwa Tshirts na buku tano kila mmoja.. Ilipofika saa nane wakatoka humo kwa maandamano, ukiziangalia hizo sura ambazo wengi ni wakina mama wengi unajuwa wamesombwa kutoka vijijini. Kuuulizia pale jamaa wakasema mbona shule zote za sekondari za serikali wameamuriwa na afisa elimu kupeleka watoto kwenye mkutano wa JPM wakiwa na nguo za kirai

Maswali
Kama ccm ni chama kikongwe kwanini kinanunua watu kwenda kwenye mkutano wao?
Kwanini iwalazimishe wanafunzi kwenda kwenye mkutano wao wa kampeni?
Pamoja na jopo la wasanii 60 kwanini hawajiamini?
Sio kwamba hapo wnataka kuwin psychology ya watu kuwa wao bado wako popular?

kampeni za gharama zote hizo ni kwa manufaa ya nani?
You do this because politics is, above allelse, “a business.” – Melania Trump (wife of Mr. Donald J.Trump (GOP presidential candidate)
 
Back
Top Bottom