Kwa hapa Posta jijini Dar duka gani la dawa bei rahisi

Kwa hapa Posta jijini Dar duka gani la dawa bei rahisi

Gobole Lenye Risasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,438
Reaction score
23,492
Wadau nina tatizo ambalo madaktari wameniandikia kununua supplements mbalimbali. ambazo natakiwa kutumia kwa muda mrefu kidogo pamoja na aina flani ya chakula.

Sasa ningependa kujua duka gani ambalo kwa hapa posta wanauza dawa kwa bei ya ku tufikiria na sisi walala hoi. kazini nipo posta nami ningependa nipate duka ambalo ntaweza kufika kirahisi huku huku posta.
 
Ni bora uende mtaa wa Kipata / Nyamwezi na Swahili Kariakoo kwenye maduka ya Madawa kwa jumla unaweza kupata unafuu fulani.
 
aiseeee.... kariakoo ni moja ya sehemu nisizozipenda kabisa hapa dar. miaka yangu yooooooote ni sehemu ambayo sipapend kabisa.labda nijaribu kwenda safari hii kwa maelezo yako. bahati mbaya naifaham mitaa miwili tu kariakoo. mtaa wa msimbazi,mtaa wa uhuru basi. hii uliyotaja nikitokea mnazi mmoja naingilia wapi?
Ni bora uende mtaa wa Kipata / Nyamwezi na Swahili Kariakoo kwenye maduka ya Madawa kwa jumla unaweza kupata unafuu fulani.
 
Ukitoka Mnazi mmoja unaenda mpaka Mtaa wa Kongo. Upande wako wa kushoto kuna mtaa wa kwanza Kipata. Huo ndio mtaa wenye maduka mengi ya Dawa kwa bei ya jumla.
1540879353453.png
 
Back
Top Bottom