Elections 2010 Kwa hali na Mali Tusaidie Ktk Kesi za Uchaguzi za CHADEMA

mudushi

Senior Member
Oct 19, 2010
151
86
Ndugu wapenzi na washabiki wa Mabadiliko na Maendeleo, sote tunajua kabisa kuwa kuna sehemu CHADEMA imezulumiwa ushindi ktk baadhi ya Majimbo. mfano mzuri ni SEGEREA, BKB TWN, TRM, Kilombero, Mvomero n.k.
Wito wangu kwa wapenda maendeleo ni kuwa aliye mwanasheria atoe mchango wa jinsi gani ya kuendesha kesi na hata atoe mchango wa fedha na wale ambao si wanasheria watoe mchango wa hali na mali.

SOTE TUTASHINDA KWA PAMOJA - CHADEMA
 
......pamoja na Shinyanga Mjini.

Inachekesha na kushangaza pia kwani, Msimazi wa uchaguzi kamtangaza mgombea wa CCM kuwa ni mshindi kwa tofauti ya KURA 1 (moja) na baada ya hapo msimamizi huyo hajaonekana tena Shy na hajulikani yuko wapi. Hatujui kama kahamishwa, kaachakazi au ..... ila Serikali wanalijua hili.

Ukweli Chama kiwasaidie wagombea hao wa Chadema walioshindwa ili waitafute haki yao Mahakamani.
 
Domhome umenena. Chama ni watu, watu ndo sisi. Basi sote tusaidie haki yetu isipotee
 
Pia majimbo ya:
Sumbawanga Mjini
Mbeya Vijijini
Musoma Vijijini (Mbunge aliyekuwepo Mkono ambaye yupo kwenye "list of shame" alimuonga mgombea wa CHADEMA akajitoa)
 
KAragwe nako Mgombea wa CCM alitangazwa chini ya mtutu wa Bunduki kuwa na mshindi na kupelekwa uwanja wa ndege kwa safari ya DAr ambako ana makazi yake ya kudumu. Shame!!
 
Back
Top Bottom