Kwa hali hii ya utoaji mimba kiholela, p2 zimegoma au zimezira

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,184
11,607
Kwa kipindi sasa jambo hili la utoaji mimba kiholela limeshamiri na limeanza kuzoeleka na kuonekana la kawaida kabisa mtaani. Utaskia tu mtaani wakiongea, aah pisi fulani kafinya bana, si unaona kachuja, hajui mimba ni ya nani na mshkaji aliyembambikia kamakazia sio yake na kwakuwa pisi bado inatamani kula maisha imeamua kuifinya mapemaaa!

Pisi yenyewe kwa madaha kama yote, inawaambia wenzie, masuala ya kunuka maziwa na mikojo bado sana ndio kwanza nina miaka 28 tu, nakula maisha kwanza.

Pisi kali hazitaki kabisa hiyo kitu mimba ibadili hali zao. Pisi inakongoroka wiki mbili tatu baada ya hapo inarejea kwenye fomu hatari mtaa unashangaa kulikoni.

Sasa najiuliza dawa za kuzuia ujauzito zimegoma, zimezira au zimesahau kufahya kazi yake?
au wahusika wamechoka kuzitumia?

Wapendwa vitendo hivyo si vya kiungwana kwa afya na zawadi ya uhai na maisha aliowajalia Mungu. Vitendo hivyo vina majuto baadae.

Mahangaiko yake ya baadae huambatana na mateso sana, kutafuta waganga na sehemu za maombezi kila mahali ili kupatiwa mtoto, kumbe ulishajiharibu na kujifungia kupata mtoto kwa matendo yako na makusudi yako ukiwa msichana mrembo.

Mungu akusaidie kuepuka roho hiyo.
 
Ni kujisahau kutumia, P2 bado imara sanaaa,

Suala la mateso lipo pande zote, ukizaa na baba asiye eleweka, ukazaa huna uwezo kiuchumi na kihisia, mateso yake ni makali kuliko kushinda kwa mwamposa
Ohh kumbe.

Maana naona mateso na mahangaiko ni mengi japo pia nina matatizo yangu, nawaonea huruma hawa ndugu zangu.

Naona mtaani anateseka na baadae huko kwa waganga na maombi anateseka pia.

Natafakari kushauri namna ya kujinasua kwenya hii kasumba.
 
Back
Top Bottom