Kwa hali hii ya Mkuranga,Kibiti na Rufiji...Ni muda muafaka kwa Waziri Mwigulu Nchemba kuachia ngazi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,704
2,000
Ni wakati sahihi kwa Waziri wa Mambo ya ndani,ndugu Lameck Mwigulu Nchemba kuachia ngazi na kuwaachia wengine nafasi hiyo.

Mauwaji ya Kibiti na Rufiji kwa ujumla wake,na katika mfufululizo usio na woga unaobeba maisha na damu za raia kikatiri,ni ajabu kuona Waziri mwenye dhamana,aliyefunga safari kwenda mpaka Kibiti,akatema nyongo na "mikwara" mingi akiwa bado yupo ofisini.

Kuachia ngazi sio kushindwa,kuachia kiti sio udhaifu,kuwapisha wengine sio dhambi.Ni dhana ya uwajibikaji wa kawaida katika ofisi za umma na jamii ya wastarabu.

Kwa namna Mwigulu alivyowaahidi watu wa Kibiti na Rufiji yote,kwa namna ziara yake alivyopambwa kwa mbwembwe na matamko ya vitisho kwa "wauwaji" ni wazi kuwa kwa sasa Mwigulu alipaswa kuwa na cheo cha ubunge tu na uwaziri awe ameukabidhi kwa aliyemteua ili ijazwe na mtu mwingine.

RPC wa Pwani katumia mbinu zote,lakini amezidiwa,mpaka sasa askari wake kadhaa wanashinda ndani kwa kuogopa kuwafuata ahela wenzao.Hata msafara wa RPC katika miji ya Kibiti na Rufiji unatembea kwa wasiwasi kama mgambo mwenye rungu na sime.RPC na Mwigulu wangekaa pembeni ili kuleta wengine wenye mikakati mipya.

Huu ni mtazamo,ni mtazamo katika kuelekea kupata kisa hasa cha kwa nini ndugu zetu wanatolewa roho kikatiri huko Kibiti.

Hili la dhuluma ya polisi na viongozi wa vijiji kwa wananchi kwa kipindi kirefu,lisiachwe likapita kimyakimya.Dhurma inauma,dhurma hujenga chuki kwa muda mrefu,dhuluma hupandikiza roho ya kisasi isiyo na mwisho.

Beria(barrier) nyingi za mazao ya msituni kama mkaa,kuni na mbao ilikuwa katika maeneo haya.Wananchi wengi wa maeneo haya walitopea katika hali ya kudhurumiwa mali zao na polisi pamoja na viongozi wa kiserikali ambao walikuwa na madaraka ya kufanya hivyo.Wengi waligeuka masikini kwa mitaji yao kupokwa na wengine kuzikimbia familia zao sababu ya mitaji yao kutolewa kama rushwa kwa viongozi wa vijiji,vitongoji na wilaya kwa msaada wa polisi.

Kuanzia maafisa wa misitu,polisi wa barabarani na polisi wa kawaida na viongozi wa vijiji na vitongoji waliokuwa na uwezo wa kuidhinisha vibali vya mazao ya misitu walicheza na dhuluma hii.Ukikutana na mtu wa Kibiti aliye mjini,atakwambia udhulumaji wa aina hii ulisubiri muda tu.Watu walishachoka sana.Hii iwe moja ya "hypothesis" ya kuona kiini cha mgogoro wa Mkuranga,Rufiji na Kibiti.

Watu walishapanga kwa muda mrefu,wakawa hawana mtetezi,wakamua kwa pamoja....Ukiweka Ugoko,Wao wanaweka chuma!!
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,833
2,000
Mh. mambo ya ndani hapamfai. Natamani angekuwa fedha na mipango.
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,905

Hili la dhurma ya polisi na viongozi wa vijiji kwa wananchi kwa kipindi kirefu,lisiachwe likapita kimyakimya.Dhurma inauma,dhurma hujenga chuki kwa muda mrefu,dhurma hupandikiza roho ya kisasi isiyo na mwisho.

Beria(barrier) nyingi za mazao ya msituni kama mkaa,kuni na mbao ilikuwa katika maeneo haya.Wananchi wengi wa maeneo haya walitopea katika hali ya kudhurumiwa mali zao na polisi pamoja na viongozi wa kiserikali ambao walikuwa na madaraka ya kufanya hivyo.Wengi waligeuka masikini kwa mitaji yao kupokwa na wengine kuzikimbia familia zao sababu ya mitaji yao kutolewa kama rushwa kwa viongozi wa vijiji,vitongoji na wilaya kwa msaada wa polisi.

Kuanzia maafisa wa misitu,polisi wa barabarani na polisi wa kawaida na viongozi wa vijiji na vitongoji waliokuwa na uwezo wa kuidhinisha vibali vya mazao ya misitu walicheza na dhurma hii.Ukikutana na mtu wa Kibiti aliye mjini,atakwambia udhurumaji wa aina hii ulisubiri muda tu.Watu walishachoka sana.Hii iwe moja ya "hypothesis" ya kuona kiini cha mgogoro wa Mkuranga,Rufiji na Kibiti.

Watu walishapanga kwa muda mrefu,wakawa hawana mtetezi,wakamua kwa pamoja....Ukiweka Ugoko,Wao wanaweka chuma!!
Yuko Busy na Mimba za Mashuleni kwa sasa
 
ancillary

JF-Expert Member
May 30, 2017
599
1,000
ndugu kama ungemuona Mwigulu siku ya kuapishwa Nyakolo sorro,sura yake ilikuwa dhahiri imejaa hofu ,naamini hivi karibuni kuna kitu tutasikia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,722
2,000
Lengo la kwanza la Waziri yeyote wa mambo ya ndani chini ya ccm ni kudhibiti vyama vya upinzani nchini , hicho ndio kigezo kikuu katika kuteuliwa kwake , fuatilia utendaji wa Mwigulu kuanzia kesi ya ugaidi wa Lwakatare hadi mauaji ya Arusha kwenye mkutano wa chadema.

Kulinda raia si kipaumbele cha uwaziri huu , ukitaka kujiridhisha fuatilia kilichomuondoa Mangu , Huyu hakuondolewa kwa sababu ya mauaji ya kibiti , yako yaliyomuondoa .
 
Mdf

Senior Member
May 16, 2017
129
250
Mh. mambo ya ndani hapamfai. Natamani angekuwa fedha na mipango.
Alikuwa anajiita field mashal kwa sababu ya kuwabambikizia kina Lwakatare kesi za kipuuzi .Kapewa kazi ya ukamanda anapiga domo.Hajui wenzake wako serious.Hata huko fedha na mipango hakumfai kote ni nafasi za kazi siyo mipasho na kupiga domo,watu wanakufa yeye anashinda kuchimba mikwara.labda wampe ukatibu mkuu wa CCM huko ataweza ndo kwenye kupiga domo.
 
Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,181
2,000
Tatizo maswala ya kiusalama wanayatolea majibu mepesi utadhani wanao kufa si binadamu
Kuhusu kujiudhulu ni viongozi wachache sana barani afrika wente kuthubutu kwani wengi wanaamimini siyo utamaduni wetu, pia tatizo la mwigulu ni kuoenda a siasa chafu tokea yuko uvccm vikevile yete ni mtuhumiwa wa mambo mengi ya kisiasa na tuhuma zimetolewa na wabunge wa upinzani ndani na nje ya bunge.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,109
2,000
Muda wote nimekuwa nikifikiri mwenyewe na kudhani kwamba changamoto linalokumbana nazo jeshii letu la Polisi huko kibiti linatokana na "UKOSEFU WA UDHOEFU WA KUKABILIANA NAZO".t

Hivyo nikawa naamini kwamba kwa sababu sio changamoto ngeni duniani, kwa haraka Jeshi letu linaweza kuazima mbinu japo za muda mfupi ili kupunguza kiwango cha madhara wakati likatafuta jawabu la kudumu.

Lakini sasa naona kuna udhembe mkubwa sana. Haiwezekani mpaka leo hawa jamaa wanazifikia targets zao na kukamilisha uovu wao bila hata kukumbana na pingamizi la askari wetu.

Hawa wajinga hawajawahi kubadirisha targets, wanaua ASKALI WETU na VIONGOZI WA SERIKALI YETU, Jeshi la Polisi limeshindwa hata kuwapa ulinzi hawa watu?
 
Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,970
2,000
Ni wakati sahihi kwa Waziri wa Mambo ya ndani,ndugu Lameck Mwigulu Nchemba kuachia ngazi na kuwaachia wengine nafasi hiyo.

Mauwaji ya Kibiti na Rufiji kwa ujumla wake,na katika mfufululizo usio na woga unaobeba maisha na damu za raia kikatiri,ni ajabu kuona Waziri mwenye dhamana,aliyefunga safari kwenda mpaka Kibiti,akatema nyongo na "mikwara" mingi akiwa bado yupo ofisini.

Kuachia ngazi sio kushindwa,kuachia kiti sio udhaifu,kuwapisha wengine sio dhambi.Ni dhana ya uwajibikaji wa kawaida katika ofisi za umma na jamii ya wastarabu.

Kwa namna Mwigulu alivyowaahidi watu wa Kibiti na Rufiji yote,kwa namna ziara yake alivyopambwa kwa mbwembwe na matamko ya vitisho kwa "wauwaji" ni wazi kuwa kwa sasa Mwigulu alipaswa kuwa na cheo cha ubunge tu na uwaziri awe ameukabidhi kwa aliyemteua ili ijazwe na mtu mwingine.

RPC wa Pwani katumia mbinu zote,lakini amezidiwa,mpaka sasa askari wake kadhaa wanashinda ndani kwa kuogopa kuwafuata ahela wenzao.Hata msafara wa RPC katika miji ya Kibiti na Rufiji unatembea kwa wasiwasi kama mgambo mwenye rungu na sime.RPC na Mwigulu wangekaa pembeni ili kuleta wengine wenye mikakati mipya.

Huu ni mtazamo,ni mtazamo katika kuelekea kupata kisa hasa cha kwa nini ndugu zetu wanatolewa roho kikatiri huko Kibiti.

Hili la dhurma ya polisi na viongozi wa vijiji kwa wananchi kwa kipindi kirefu,lisiachwe likapita kimyakimya.Dhurma inauma,dhurma hujenga chuki kwa muda mrefu,dhurma hupandikiza roho ya kisasi isiyo na mwisho.

Beria(barrier) nyingi za mazao ya msituni kama mkaa,kuni na mbao ilikuwa katika maeneo haya.Wananchi wengi wa maeneo haya walitopea katika hali ya kudhurumiwa mali zao na polisi pamoja na viongozi wa kiserikali ambao walikuwa na madaraka ya kufanya hivyo.Wengi waligeuka masikini kwa mitaji yao kupokwa na wengine kuzikimbia familia zao sababu ya mitaji yao kutolewa kama rushwa kwa viongozi wa vijiji,vitongoji na wilaya kwa msaada wa polisi.

Kuanzia maafisa wa misitu,polisi wa barabarani na polisi wa kawaida na viongozi wa vijiji na vitongoji waliokuwa na uwezo wa kuidhinisha vibali vya mazao ya misitu walicheza na dhurma hii.Ukikutana na mtu wa Kibiti aliye mjini,atakwambia udhurumaji wa aina hii ulisubiri muda tu.Watu walishachoka sana.Hii iwe moja ya "hypothesis" ya kuona kiini cha mgogoro wa Mkuranga,Rufiji na Kibiti.

Watu walishapanga kwa muda mrefu,wakawa hawana mtetezi,wakamua kwa pamoja....Ukiweka Ugoko,Wao wanaweka chuma!!
Umenena vyema.
Inasemekana huko ukikutwa na mbao zitaifishwa na mapolisi wana uza ukifata fata mbao zako unakula shaba.
vijana wengi wamepigwa shaba...na kutupwa misituni.
tumekaa tunajidanganya kumbe tatizo ni mauaji ya raia wenzetu yalio fanywa muda mrefu.
vijana wengine waliuliwa na hutupwa mto rufiji kuliwa na mamba.
mwanzoni wa mwaka huu maiti 5 zilitupwa mto rufiji....hawa ni vijana wa kibiti...na Nchemba alilichukulia kama wamekufa panya....serikali haikujali sababu walofanya ni polisi wake.
watu wameteswa sana kibiti..
hakuna siasa wala dini .hii ni dhulma na sote tukawaacha raia wezetu bila ya msaada...
sasa kinacho fanyika ni kisasi ...
only tume ya kiraia itaweza kuleta ukweli. Polisi wanajua wao ndo chanzo wataficha tu.
tuombe bunge ba spika aache ushabiki wa kijinga aunde tume huru ya bunge ipewe ulinzi na JWTZ wakajichimbie kibiti kupata ukweli.
na ikithibitika polisi wana husika na uvunjaji haki za raia wachukuliwe hatua.
bila hivo binadamu ni mbaya kuliko mnyama...kisasi kitatumaliza
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,823
2,000
Ni wakati sahihi kwa Waziri wa Mambo ya ndani,ndugu Lameck Mwigulu Nchemba kuachia ngazi na kuwaachia wengine nafasi hiyo.

Mauwaji ya Kibiti na Rufiji kwa ujumla wake,na katika mfufululizo usio na woga unaobeba maisha na damu za raia kikatiri,ni ajabu kuona Waziri mwenye dhamana,aliyefunga safari kwenda mpaka Kibiti,akatema nyongo na "mikwara" mingi akiwa bado yupo ofisini.

Kuachia ngazi sio kushindwa,kuachia kiti sio udhaifu,kuwapisha wengine sio dhambi.Ni dhana ya uwajibikaji wa kawaida katika ofisi za umma na jamii ya wastarabu.

Kwa namna Mwigulu alivyowaahidi watu wa Kibiti na Rufiji yote,kwa namna ziara yake alivyopambwa kwa mbwembwe na matamko ya vitisho kwa "wauwaji" ni wazi kuwa kwa sasa Mwigulu alipaswa kuwa na cheo cha ubunge tu na uwaziri awe ameukabidhi kwa aliyemteua ili ijazwe na mtu mwingine.

RPC wa Pwani katumia mbinu zote,lakini amezidiwa,mpaka sasa askari wake kadhaa wanashinda ndani kwa kuogopa kuwafuata ahela wenzao.Hata msafara wa RPC katika miji ya Kibiti na Rufiji unatembea kwa wasiwasi kama mgambo mwenye rungu na sime.RPC na Mwigulu wangekaa pembeni ili kuleta wengine wenye mikakati mipya.

Huu ni mtazamo,ni mtazamo katika kuelekea kupata kisa hasa cha kwa nini ndugu zetu wanatolewa roho kikatiri huko Kibiti.

Hili la dhuluma ya polisi na viongozi wa vijiji kwa wananchi kwa kipindi kirefu,lisiachwe likapita kimyakimya.Dhurma inauma,dhurma hujenga chuki kwa muda mrefu,dhuluma hupandikiza roho ya kisasi isiyo na mwisho.

Beria(barrier) nyingi za mazao ya msituni kama mkaa,kuni na mbao ilikuwa katika maeneo haya.Wananchi wengi wa maeneo haya walitopea katika hali ya kudhurumiwa mali zao na polisi pamoja na viongozi wa kiserikali ambao walikuwa na madaraka ya kufanya hivyo.Wengi waligeuka masikini kwa mitaji yao kupokwa na wengine kuzikimbia familia zao sababu ya mitaji yao kutolewa kama rushwa kwa viongozi wa vijiji,vitongoji na wilaya kwa msaada wa polisi.

Kuanzia maafisa wa misitu,polisi wa barabarani na polisi wa kawaida na viongozi wa vijiji na vitongoji waliokuwa na uwezo wa kuidhinisha vibali vya mazao ya misitu walicheza na dhuluma hii.Ukikutana na mtu wa Kibiti aliye mjini,atakwambia udhulumaji wa aina hii ulisubiri muda tu.Watu walishachoka sana.Hii iwe moja ya "hypothesis" ya kuona kiini cha mgogoro wa Mkuranga,Rufiji na Kibiti.

Watu walishapanga kwa muda mrefu,wakawa hawana mtetezi,wakamua kwa pamoja....Ukiweka Ugoko,Wao wanaweka chuma!!
mkuu J. POMBE uliyemteua kukusaidia mambo ya ndani umekosea hawezi kazi mpumzishe tafuta mwengine au mpe yule kijana wako wa ARUSHA atakusaidia kwa kiwango fulani japo hata weza kumaliza
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,836
2,000
MAUAJI YA JANA NI AIBU TUPU.WAUAJI WAMEINGIA KIJIJINI ,HAKUNA HATA POLISI,WALA MAWASILIANO NA POLISI . HAIWEZEKANI WAUAJI WATEMBEE NYUMBA TATU TENA ZA KIJIJINI BILA KUONEKANA. MAANA NYUMBA ZIPO MBALIMBALI.

Polisi bila ushirikiano wa raia hawawezi kumkamata hata kipofu akivamia kijijini.

Wanakijiji wameshahakikishiwa na wauaji kwamba wao siyo walengwa wa hayo mauaji hivyo wala haiwanyimi usingizi lakini wauaji lazima wanajulikana na ukizingatia kuna uhasama kati ya viongozi wa vijiji/polisi/mgambo na wananchi kutokana na sababu mbalimbali ndiyo kabisa wala hawajishughulishi.
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,683
2,000
  • Hivi maafisa misitu wapo kibiti pekee?
  • Vizuizi vya barabarani vipo kibiti pekee?
  • Na ukidhulumiwa ndo ukaue wenzako kama mbu?
Hao wauaji tayari wamesha wa fool na hoja ya dhuluma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom