Kwa hali hii ya Mkuranga,Kibiti na Rufiji...Ni muda muafaka kwa Waziri Mwigulu Nchemba kuachia ngazi

Kama haija lala iko wapi watu wanakufa kila siku kwa namna ileile kila siku.au wako macho kuwatafuta watu wanao wakosoa na kupingana na itikadi zao ila kwa hili kama wapo macho basi wamezidiwa akili,kitu ambacho ni ngumu kuamini.
huwezi kunielewa
 
Una uhakika gani kuwa hawajawahi kulalamika?
Mkuu, sina haja ya kutoa povu la ubishi. Nilikuwa naelezea kile nachokijua na kukiamini sio lazima na wewe uwe upande wangu.

Kikubwa ni kwamba mimi sio mshabiki wa mauaji wala si mtu nayefuata mkumbo wa mawazo ya wengine.
 
Ni wakati sahihi kwa Waziri wa Mambo ya ndani,ndugu Lameck Mwigulu Nchemba kuachia ngazi na kuwaachia wengine nafasi hiyo.

Mauwaji ya Kibiti na Rufiji kwa ujumla wake,na katika mfufululizo usio na woga unaobeba maisha na damu za raia kikatiri,ni ajabu kuona Waziri mwenye dhamana,aliyefunga safari kwenda mpaka Kibiti,akatema nyongo na "mikwara" mingi akiwa bado yupo ofisini.

Kuachia ngazi sio kushindwa,kuachia kiti sio udhaifu,kuwapisha wengine sio dhambi.Ni dhana ya uwajibikaji wa kawaida katika ofisi za umma na jamii ya wastarabu.

Kwa namna Mwigulu alivyowaahidi watu wa Kibiti na Rufiji yote,kwa namna ziara yake alivyopambwa kwa mbwembwe na matamko ya vitisho kwa "wauwaji" ni wazi kuwa kwa sasa Mwigulu alipaswa kuwa na cheo cha ubunge tu na uwaziri awe ameukabidhi kwa aliyemteua ili ijazwe na mtu mwingine.

RPC wa Pwani katumia mbinu zote,lakini amezidiwa,mpaka sasa askari wake kadhaa wanashinda ndani kwa kuogopa kuwafuata ahela wenzao.Hata msafara wa RPC katika miji ya Kibiti na Rufiji unatembea kwa wasiwasi kama mgambo mwenye rungu na sime.RPC na Mwigulu wangekaa pembeni ili kuleta wengine wenye mikakati mipya.

Huu ni mtazamo,ni mtazamo katika kuelekea kupata kisa hasa cha kwa nini ndugu zetu wanatolewa roho kikatiri huko Kibiti.

Hili la dhuluma ya polisi na viongozi wa vijiji kwa wananchi kwa kipindi kirefu,lisiachwe likapita kimyakimya.Dhurma inauma,dhurma hujenga chuki kwa muda mrefu,dhuluma hupandikiza roho ya kisasi isiyo na mwisho.

Beria(barrier) nyingi za mazao ya msituni kama mkaa,kuni na mbao ilikuwa katika maeneo haya.Wananchi wengi wa maeneo haya walitopea katika hali ya kudhurumiwa mali zao na polisi pamoja na viongozi wa kiserikali ambao walikuwa na madaraka ya kufanya hivyo.Wengi waligeuka masikini kwa mitaji yao kupokwa na wengine kuzikimbia familia zao sababu ya mitaji yao kutolewa kama rushwa kwa viongozi wa vijiji,vitongoji na wilaya kwa msaada wa polisi.

Kuanzia maafisa wa misitu,polisi wa barabarani na polisi wa kawaida na viongozi wa vijiji na vitongoji waliokuwa na uwezo wa kuidhinisha vibali vya mazao ya misitu walicheza na dhuluma hii.Ukikutana na mtu wa Kibiti aliye mjini,atakwambia udhulumaji wa aina hii ulisubiri muda tu.Watu walishachoka sana.Hii iwe moja ya "hypothesis" ya kuona kiini cha mgogoro wa Mkuranga,Rufiji na Kibiti.

Watu walishapanga kwa muda mrefu,wakawa hawana mtetezi,wakamua kwa pamoja....Ukiweka Ugoko,Wao wanaweka chuma!!
ili iweje muuane kibiti wajiudhulu watu wa singida akili za panya hizi.
 
Kama police wamezidiwa basi wapeleke jeshi kukomesha haya mauwaji

Na hicho kinachodaiwa kwenye barua ya hao wauwaji wafanyie kazi.

Dhuluma haijawahi kumuacha mtu salama
 
Umeingia chaka kwa kuunganisha wakata mkaa na kuni na mauaji ya kibiti, unasaidia kuwaficha wauwaji, ukifuatilia mauaji haya yanavyofanyika kwa ustadi wa hali ya juu na kwa series bila woga hujiulizi ni mwanakijiji gani anauwezo wa kupanga mauaji kama haya na wakafanikiwa kwa kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom