Kwa hali hii wanawake hawawezi

Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,523
653
kwa matukio yaliyotokea kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa umoja wa wanawake(UWT) nimebadilisha mtazamo wangu kuhusu wanawake kushika uongozi wa nchi hii, nchi yetu haiwezi kuongozwa kwa vijembe na mipasho ya kipashkuna namna ile, hatuwezi kuongozwa na mtu au watu wenye uwezo finyu wa kukabiliana na hata changamoto za maswali tu,je changamoto dhahiri za kiuchumi na mambo mengine yasiotakiwa katika jamii yetu wataweza!!?
Mimi sikuona ubaya wa swali alilouliza shyrose bhanji kwa sophia simba kuwa toka amekuwa kiongozi wa UWT amefanya kitu gani katika kuboresha na kuimarisha chama chake na wanawake kwa ujumla lakini matokeo yake sophia simba mapovu yanamtoka anashindwa kutulia kwa hekima kujibu hoja analeta upashkuna kwenye mambo serious!! halafu fikiria mtu mwenye udhaifu kama huo ndo wanawake wanamchagua kuwa kiongozi wao!! kwa hiyo tu judge uwezo na utendaji wa wanawake kwa kuangalia kiongozi ambae wamemchagua!!? kama kiongozi wao yu hivyo, vipi kuhusu anaowaongoza na waliomchagua!!? inanipa mashaka na sasa mtazamo niliokuwa nao kwa wanawake nimeuweka kwenye mabano mpaka hapo nitakapohakikisha vinginevyo!!

NOTE: I am not being a misogynist or a chauvinist! ni kwamba mtazamo wangu kwa wanawake umebadilika ghafla kwa tukio la uchaguzi wa mwenyekiti wa UWT.
 
Mmmmmmhhhhhhhh! 'kama mmoja ataokoka kwa jina langu, nitawaokoa wote!' i will lead my family, period!
 
Well, nakosa ujasiri wa kubishana na wewe manake hata mie wamenikatisha tamaa.....Labda watupe ushuhuda wale wanaoongozwa nao huko kwenye mawizara.

Ila trust me, bado wapo wanawake wengi tu walio nje ya system ambao wana uwezo wa uongozi katika nyanja zozote (you name it). Ila tatizo linakuja kuwa hawa waliopo wanatumia nguvu nyingi, kifedha n.k ili kuendelea kujiweka hapo walipo. Kama ulivyosikia SS alivyodai kuwa Shyrose asamehewe coz ni mdogo mno kwenye nyanja za siasa (kwa tafsiri yangu), sasa huoni kuwa hao wanaoibuka sasa wataendelea kuzuiwa waliko mpaka waliojirithisha nafasi zao watoke?
 
Sasa wewe unafkiri mwanaume wa shoka ataacha kutoa support kwa mwanamke wa shoka???
Tatizo si wanawake hawawezi!!!! wanaoweza hawapewi nafasi,,,,,tatizo ni mfumo wote wa ccm umejaa rushwa...........
 
Chuma Chakavu mtazamo wako unaweza kuwa sahihi kwa wanawake wa CCM maana ni kweli swali la Shyrose Bhanji lilikuwa la kawaida kabisa na Sophia angeweza kulijibu bila moja kwa moja bila kuanza kwa vijembe lakini mtazamo wako huo hauwezi kuwa sahihi kwa wanawake wote wa Tanzania. Wapo wanawake wenye uwezo. UWT si ya wanawake wote wa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Tukio lile ni la aobu sana lakini haliwasiqulify wanawake wote. Mtu apimwe kwa uwezo wake,if she is capable apewe kama kura zitatosha lakini kusiwe na ghiliba katika zoezi hilo.
 
Chuma Chakavu mtazamo wako unaweza kuwa sahihi kwa wanawake wa CCM maana ni kweli swali la Shyrose Bhanji lilikuwa la kawaida kabisa na Sophia angeweza kulijibu bila moja kwa moja bila kuanza kwa vijembe lakini mtazamo wako huo hauwezi kuwa sahihi kwa wanawake wote wa Tanzania. Wapo wanawake wenye uwezo. UWT si ya wanawake wote wa Tanzania.

Eti mwaJ, wanawake wa CCM hawapaki lipstick na hina au wanavaa boxer?
 
Last edited by a moderator:
Chuma Chakavu mtazamo wako unaweza kuwa sahihi kwa wanawake wa CCM maana ni kweli swali la Shyrose Bhanji lilikuwa la kawaida kabisa na Sophia angeweza kulijibu bila moja kwa moja bila kuanza kwa vijembe lakini mtazamo wako huo hauwezi kuwa sahihi kwa wanawake wote wa Tanzania. Wapo wanawake wenye uwezo. UWT si ya wanawake wote wa Tanzania.

OK uko sawa! lakini wewe huoni ni hatari kwa kundi kubwa kama hilo kuwa na kiongozi wa namna ile? ni kweli si wanawake wote wako hivyo ila kwa kupitia UWT taswira ya uwezo wa wanawake kiuongozi imedhalilishwa kwenye macho ya wanajamii wengine!
 
Last edited by a moderator:
tukio lile ni la aobu sana lakini haliwasiqulify wanawake wote. Mtu apimwe kwa uwezo wake,if she is capable apewe kama kura zitatosha lakini kusiwe na ghiliba katika zoezi hilo.

je yawezekana mtu mwenye akili achague kuongozwa na mtu mpumbavu!! Na ikiwa mtu mwerevu anaongozwa na mjinga utamwelewa vipi?!!
 
Heshima kwako mzee CC
Mimi sikubaliani na mtazamo wako kwani ninahisi umefikia maamuzi hayo kwa kuangalia uchaguzi wa uwt pekee.
Jumuiya hiyo siyo kigezo cha kufikia kuamua hivyo. zipo jumuiya nyingi za akina mama aidha za kisiasa au za kijamii ambazo wanawake wengi wamejitokeza kama majasiri [wakati mwingine zaidi yetu]
Hata huko ndani ya uwt siyo wote wako hivyo.
lakini pia uelewe sisi hatuna utamaduni wa kukubali kushindwa hata chaguzi za mwenyekiti wa mtaa kilio ni rushwa.
Kama kweli rushwa ipo kwa kiasi hicho maana yake tatizo ni la jamii nzima iko hivyo. kwa maoni yangu mtu anaweza kutumia udhaifu wa umasikini wa mtu kwa kumpa rushwa lakini hiyo haiondoi utu wa mtu kuamua kutompigia huyo aliyetoa rushwa.
 
OK uko sawa! lakini wewe huoni ni hatari kwa kundi kubwa kama hilo kuwa na kiongozi wa namna ile? ni kweli si wanawake wote wako hivyo ila kwa kupitia UWT taswira ya uwezo wa wanawake kiuongozi imedhalilishwa kwenye macho ya wanajamii wengine!

Hatari si kwa UWT tu. Wewe huoni hatari ya kundi kubwa la watanzania kuongozwa na viongozi wa namna ya hawa tulionao sasa? Nina maanisha kuwa hata kwa ngazi ya kitaifa tunaongozwa na viongozi wa caliber hiyo hiyo tu. Hivyo usiwashangae wanawake wa CCM.
 
kwa hao wanawake wachache wa ccm kutoweza haimaanishi kuwa wanawake wengine hawawezi.
mimi naweza hata nisipowezeshwa.
 
UWT si ya wanawake wote wa Tanzania.
mwaJ fafanua kirefu cha UWT = Umoja wa Wanawake Tanzania.
Hii ni tofauti na UVCCM ambayo ni Umoja wa Vijana wa CCM

Kaa ufikiri tena.

Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
mwaJ fafanua kirefu cha UWT = Umoja wa Wanawake Tanzania.
Hii ni tofauti na UVCCM ambayo ni Umoja wa Vijana wa CCM

Kaa ufikiri tena.

Bazazi!
Bazazi mbona unaleta tafsiri rahisi rahisi hivyo? Kuwepo kwa neno Tanzania haina maana ya kuwa kila mwanamke ni mwanachama wa huo umoja. Ina maana kweli hujui kuwa hiyo ni moja ya jumuiya za chama cha mapinduzi? Unadhani unaweza kutoka utokako na card yako ya CUF au CHADEMA ukaenda kugombea uongozi au hata kupiga kura UWT? Aaaaaaaaaaaa Bazazi hufanani hiyo reasoning uliyoitoa hapo labda kama ulikuwa unatania.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom