Kwa hali hii wanaoitetea CCM hadharani wana ujasiri gani?

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Kwa mambo yanavyoendelea sasa hivi hakuna ubishi kuwa CCM imeshakufa kinachosubiriwa ni mazishi tuu. Ushaidi wa hili ni haya yafuatayo:
  1. Hakiko tena kwa maslai ya Watanzania kwa kuwa hali ilivyongumu kwa watu wengi, wao wanapiga msumari kwenye kidonda wanataka kuongeza posho za Wabunge tena bila haya kwa kisingizi cha hali ngumu kwao wabunge.
  2. Badala ya kuboresha maisha ya Watanzania wao wanafikiria nani rais 2015, na kwa hali halisi wale waliowachafu ndio wanaonekana kuwa watashinda na kupeperusha bendera ya CCM 2015 wakidhani kuwa watanzania still ni mabwege hawana tena uwezo wa kusoma alama za nyakati wapo gizani.
  3. Hakuna tena dalili ya kuweza kutekeleza walichowaahidi Watanzania katika kampeni za rais wao katika uchaguzia uliopita hata theluthi moja YA AHADI kutokana na kuaraganyika kwa uchumi kwa sasa tazama ahadi za mgombea urais wao:
AHADI ZA MGOMBEA URAIS WA CCM 2010
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Kuna siku kwenye daladala nilijifanya kuitetea CCM nakwambia konda akanibembeleza nishuke manake abiria wengi walikuwa wameudhika na kitendo changu cha kuitetea CCM -HII ILITOKEA KITUNDA DSM
 
CCM ni janga la kitaifa, haikubaliki, ni mwendawazimu tu anayeweza kuipenda CCM kama hayumo kwenye mfumo wa ulaji wa CCM.
 
Wengine tunasubiri tu tuone huyo Sharobalo kama ataliweza hilo fuko la misumari, maana ni yeye mwenyewe ndo kalishindilia.
 
nimewahi kuandika hapa kuwa, ukiwa mfusi wa ccm lazima uwe chizi , mwizi au unafaidika na hao wezi.
kinyume cha hayo hakuna mwenye akili timamu anaweza kushabikia ccm. so naunga mkono hoja 100%.
 
CCM ni janga la kitaifa, haikubaliki, ni mwendawazimu tu anayeweza kuipenda CCM kama hayumo kwenye mfumo wa ulaji wa CCM.

85% uko sahihi mkuu, CCM ni kundi flani la wahuni wachache waliojitoa akili na kujifanya hawaelewi hali ilivyo mbaya huku tunakoishi watu wa kima cha chini!
Nachukia ccm na wote wanaisapoti pumbavu kbs punguwani hawa!
 
70.Kuongeza posho za wabunge ili kutunisha akiba yao kwa ajili ya hongo ya pilau kwa wapigakura wao mwaka 2015<hiyo imetekelezwa>.
 
Hakuna wanachokosea katika hilo, hebu fikiria kama kazi yako inayokuweka hapa mjini ni mwizi utaacha kuitetea?
 
Hizo ndiyo siasa za Africa..... huishia baada ya kampeni, siyo CCM, CUF, CDM, NCCR.. wote sawa tu.

Kama gombea atawaambia nitawafanyia hiki, kwanini msimuulize atatumia mbinu gani?

Au fedha zitatoka wapi?.. maanake sisi watanzania wenyewe hatulipi kodi za kutosha kuendesha serikali yetu ya mabwanyenye
.
Hata ukiangalia Bajeti mbadala za wapinzani, ni upuuzi mtupu . Hazimake sense yeyote.

Bilioni mia tano za posho ambazo Mnyika alizungumzia kwenye ilani ya Uchaguzi ya CDM ili zitumike kulipia elimu bure, haziwi reflected in Bajeti mbadala wala mapokezi yao ya posho na matumizi yao ya ruzuku.
Wizi tu!, hamna lolote!

why sell shares and not this? - YouTube
 
Yaani hiki chama ni aibu tupu ni kichaka cha maovu,wengi wanaingia kwenye chama kuficha maovu yao.Mwanza diwani mmoja mwenye utajiri wa kutisha ambao si wake.kwa kutumia uwezo wa chama, pesa na vyombo vya maamuzi kupora nyumba ya watu kisa wenye nyumba hawataki kuwauzia kupisha ujenzi wa mahotel yao ya kitalii.Hawa watu wanakipaka matope chama
 
Ninakubaliana na ninyi kwa mawazo yenu na hii ndiyo "demokrasia" tatizo ni namna ninyi mnavyowachukulia watu wengine wenye mtazamo tofauti na wa kwenu "kulazimisha wote waamini ninyi mpo sahihi".
 
al sahaf aliwah kusema kama wao.wanapingana na ukweli.pia imetengenezwa hofu kuwa ukiji-detach wanakumaliza
 
Back
Top Bottom