Hi members, nitaanza kwa kujitambulisha hapa chini kabla ya kwenda kwenye mada kamili.
Jina: Free ideas(Not official)
Umri:29yrs
Elimu:Shahada
Kabila:Kanda ya ziwa
Familia: Married with 2 kids
Kiufupi nimesoma 0-A level hapa Tanzania kisha nikaenda nje ya nchi(Europe) kuchukua Bachala.
Binafsi kuna hali inanitokea hua mpaka mwenyewe nashindwa kujielewa kama ni kwangu tu ama hata kwa watu wengine, lakini kila nikijaribu kumsimulia mtu kuhusu yanayonitokea hua ananishangaa na kuona kwamba mimi sio mtu wa kawaida.
Nitaeleza japo kwa ufupi hapa chini kuhusu hali hiyo.
.
.
2. Napenda sana kukaa mwenyewe na hua nikiwa mwenyewe najikuta naongeaongea na wakati mwingine kucheka mwenyewe.Pia mama yangu aliponizaa anasema kwanza hakusikia uchungu wa uzazi kabisa.Pia nilipozaliwa tu nilicheka badala ya kulia kama watoto wengine.Nikiwa na miaka 3 nikikua na uwezo wa kusoma bila kukosea.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
6. Mwaka mmoja kabla ya babu wa Loliondo nikiwa nje ya nchi nilimwambia jamaa yangu kwamba mwakani kuna mtu ataibuka maarufu kwa kusema anatibu ukimwi tanzania na atapata watu wengi.Kweli ikawa jamaa yangu mpaka leo anaamini mimi ni ndugu yake huyo babu na kwamba nilijua paln zake.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
13. Sipendi kabisa habari za Dini na maswala yamuhusuyo mungu(mimi ni Atheist) na hua najickia vibaya sana kujadili maswala hayo.Ninaamini hakuna mungu.Pia sina ushabiki wa vitu vinavyopendwa na watu wengi mfano mpira ama siasa.
.
.
14. Napenda kukaa sana vijijini (japo kwa sasa niko mjini sababu ya kazi)na kufanya kazi huko, sipendi kuajiliwa na wala sifurahii kabisa kulipwa mshahara na mtu mwingine.Napenda pia kuzunguka zunguka sehemu zenye mito ama maji yanayotiririka na kuyaangalia huku nikijiongelea mwenyewe.
.
.
15. Kuna mwaka flani nilikua kijijini eneo la mto akili ikanituma niangalie juu ghafla kikashuka kitu kizito sana kutoka angani kama jiwe kubwa, baada ya kutua chini ghafla kitu kile kikageuka ndege mzuri na sijawahi kuona ndege wa aina kama ile tena mpaka leo.Ndege yule aliruka ruka kunizunguka kisha akapaa kurrudi angani vertically. Cha ajabu sikuogopa kabisa hali ile.
.
.
.
17. Tangu niwe na akili timamu sijawahi kutoa chozi kwa maana ya kulia.Hata misibani nikienda hua naona ni hali ya kawaida na napenda sana kuishika maiti hasa kichwani.Wakati mwingine hua naomba nioshe maiti iliradi niishike kichwa tu kisha nami najishika kichwa halafu naondoka msibani.
.
.
18. Napenda harufu mbaya sana.Nikipita mahali kuna mzoga naweza kumaliza nusu saa hapo navuta harufu mpaka tumbo hua linajaa.Nikimuona mtu analia ama yuko kwenye huzuni mimi hua nafsi inafarijika na napenda kumwangalia huku natabasamu.
.
.
.
.....Free ideas.......