Kwa dhati kabisa! Kwanini unapenda kukopa?

Kwa dhati kabisa! Kwanini unapenda kukopa?

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,143
Reaction score
10,859
Mikopo inatesa watu, Mikopo inadhalilisha, Mikopo ina fedhehesha, Mikopo inaleta uadui, Mikopo inavunja amani kwenye familia.

Mikopo ingekuwa dawa basi ingeitwa dawa ambazo huwezi pewa bila maelekezo na usimamizi wa daktari! Mikopo ni utumwa.

Zamani waliokopa wakashindwa kurejesha waligeuzwa watumwa na familia zao kwenda kuwatumikia wakopaji. Mikopo sio Mpango wa Mungu, ni laana..

Embu jiulize, Kwanini lazima ukope?:-

- Unaogopa njaa?
- Unaiga maisha ya mwenzio?
- Una tamaa ya kumiliki kitu au hali fulani?
- Umekosa uvumilivu wa kulala na njaa?
- Unataka kuweka heshima baa, au mtaani kwako, au kwa jirani zako?
- Ni hofu kuwa watoto hawatakula sikukuu vizuri?q
- Au una kopa kwa kuwa mpango wa kisayansi wa kutumia mkopo huo?

Any way, Wanauchumi wanasema "Kopa kwa Maendeleo" Japo hata Nchi inakopa kwa maendeleo lakini hadi sasa tunadaiwa Trilioni 61. Sawa na bajeti ya nchi kwa miaka 2 nanusu!!
 
kuna mtu alinishauri nikope mkopo kwa ajili ya harusi.. na hata ndoa yenyewe nikaiua kabisa... nikamwona mwehu... wadada wajinga sana wakiukuona una kazi na business ya kizushi, umepanga appartment.. una ka ist anafikiri maisha ni marahisi...

anaanza kulazimisha harusi.. na anataka hata ukakope avae shela

hata kama mtu umempenda harusi muache afanye mwenyewe ya uwezo wake.. usimlazimishe

mkopo wowote ambao sio wa biashara ni laana.. epuka kabisa
 
kuna mtu alinishauri nikope mkopo kwa ajili ya harusi.. na hata ndoa yenyewe nikaiua kabisa... nikamwona mwehu... wadada wajinga sana wakiukuona una kazi ya kizushu.. una ka ist anafikiri maisha ni marahisi...

anaanza kulazimisha harusi.. na anataka hata ukakope avae shela

hata kama mtu umempenda harusi muache afanye mwenyewe ya uwezo wake.. usimlazimishe

mkopo wowote ambao sio wa biashara ni laana.. epuka kabisa
Usikubali,kopa kwa mambo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikopo haiepukiki...hasa kwa wafanya biashara, inakuza mtaji.
 
Dah...mikopo mingi hurudishwa pamoja na riba...ili uwe POA lazima ukikopa ujue unaingiza kwenye biashara itakayokupa faida zaidi ya riba....vinginevyo ni ujinga....Kuna mibwege inakopa pesa ya kunywea pombe..

Ukweli machungu[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapokopa hakikisha unatekeleza lengo lililokufanya ukope. Epuka kukopa kununua vitu vya nyumbani, nguo, kutoa mahari au kufanya sherehe. Kopa kwa ajili ya biashara, kununua ardhi, kutatua changamoto fulani kama ugonjwa, kesi nakadhalika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfanyabiashara huwezi kuepuka kukopa maisha! Bila kukopa huwezi kusonga.

Kopa ukiwa na lengo sio kukopa pesa isiyozalisha mf. Kukopa sababu ya
1. Arusi
2. Starehe
3. Mavazi

KOPA UKIWA TENA UMEFANYA UTAFITI KUWA PESA ITARUDI SIO UTEGEMEE AHADI TU ZA KUPATA PESA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom