Kwa dalili hizi, hakuna Katiba Mpya!

Kwa dalili hizi, hakuna Katiba Mpya!

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Katika hatua za awali za mchakato wa katiba mpya sisi wengine tuliamini kuwa ifikapo mwaka 2015 itapatikana katiba mpya hasa baada ya ule mswaada wa awali kurejeshwa bungeni baada ya kelele za wadau kuwa nyingi. Niliamini hatua ile ingekuwa ndio mwisho wa kufanywa hadaa katika jambo hili nyeti kwa taifa na mustkbali wa vizazi vijavyo. Lakini yaliyotokea hivi karibuni kule Bungeni ni ishara tosha KUWA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA UKO SHAKANI SASA.

TUJIKUMBUSHE HAYA.
1.Katika mswaada wa awali kabisa ulipata upinzani hasa kwa upande wa Zanzibar kutokana na kutokuwa na usawa katika baadhi ya vipengele hasa vilivyohusu wajumbe na uwakilishi katika ngazi za maamuzi( wajumbe wa tume na muundo wa bunge la katiba) na baadhi ya Term of reference- kumbukeni suala la kujadili kuwepo au kutokuwepo muungano lilipigwa marufuku.

2. Tokea awali suala la katiba mpya lilitekwa na wanasiasa na kusahau uwakilishi mpana wa wananchi kwa nini muundo wa bunge la katiba liliwataja wabunge wanaotokana na vyama na wawakilishi kuwa wajumbe wa moja kwa moja na ikasahau kuwa kuna watanzania wengi zaidi ambao hawana vyama na hili suala lilinyamaziwa?

Maelezo hayo yanaaminisha jambo moja tu. HAKUKUWA NA NIA HASA YA KUTENGENEZA KATIBA YA WANANCHI ila ni kujaribu kufanywa hilba kwa kisingizio cha wakati na ukweli ni kwamba huo wakati wenyewe hauheshimiwi.Kwa nini katiba ya wakati iwatenge baadhi ya watu wa wakati wa leo( wananchi wengi wasio na vyama) ?

MWENDELEZO WA HILBA NA KILICHOJIRI

Mara baada ya kutoka rasimu ya awali na kuonekana wazi kuwa inatishia maslahi ya baadhi ya wanasiasa (CCM) chama ambacho ndicho kinaisimamia serikali inayoandaa katiba mpya walianza kucharuka na kuzidi kuuteka mchakato.
Taarifa za wazi za kupinga zilisikika kutoka kila kona mpaka kwa wale ambao walikuwa wamesahaulika waliibuka na sasa ikawa ni kujihami kwa kila hali. Zilivuja taarifa kutoka katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa ilifika mahali wajumbe wa NEC ya CCM walidiriki kuhoji ilikotoka sera ya katiba mpya wakati ile ya CCM 2010-2015 haimo. kuanzia hapo imekuwa ni kuandamwa kwa mwenyekiti wa chama mpaka leo.

Kilichojiri ni kwa makusudi kuharibu hatua muhimu ambayo kwa mwendelezo wa mchakato wa katiba ambapo kwenye nia njema hatukutarajia kutokea- hii ni dalili nyengine kuwa HAKUNA NIA NJEMA YA KUPATIKANA KATIBA. waliofanya hivi ni watu wale wale waliojazana katika hilo bunge tajwa la katiba linalokuja mbeleni, ni wale wale wanaoongoza nchi ni wale wale ambao serikali inayoongozwa na chama chao walileta hoja na mswaadawa katiba mpya.na ndio hawa hawa wanaopinga mapendekezo ya tume.( naona kisutu na mwenye kisutu simwoni) ndivyo ninavyoweza kusema.

Kinachoendelea kwa sasa baada ya bunge kupitisha mswaada wa upande wa chama kimoja kilichoteka bunge, licha ya wapinzani kuchachamaa jamaa hawa wamefanikiwa suala moja kubwa na muhimu la KUPOTEZA MUDA ili kwa maslahi yao uchaguzi ujao ufanyike katika katiba ya sasa maana wanajuwa hata rais akatae kutia saini kwa mfano muda utakuwa umekwenda sana na na kwa hili la katiba kwa sasa ni sawa na kuwa limesimamama. Katika hali hii tayari washenga wa CCM na wanaopinga rasimu ya katiba wanatumia mwanya huo kuonesha kasoro lukuki na hapa kwa mtazamo wangu wanataka kuhalalisha mchakato usiendelee mbele. wametumia wingi wao bungeni kusitisha mchakato usiendelee na hii ndio jeuri ya CCM ikiwa jambo hawalitaki. Wao ni daima tu.

MAWAZO YANGU.
Ikiwa suala la katiba limetokana na utashi wa kweli kwa ajili ya wananchi na tanzania mpya kutoka kwa raisi mwenyewe na timu yake yaserikali basi hili suala litapita vizuri na hayo mengine vijana wa leo wanaliita shengesha tu na ikiwa Mh mwenyewe yumo anacheza na wakati , basi hili limefika mwisho ingawa kuna dalili za kuharimu kila kitu,mali, wakati na hata nafsi za watu ziko hatarini kupotea

SASA tunasubiri Rais wetu akiondoka madarakani kwa aibu mbaya au kwa kuandika HISTORIA YA UKWELI

Uamuzi anao yeye mwenyewe.

Nawasilisha
 
Toka Warioba alipolazimisha ishu ya Tanganyika iwe ndio main issue
nilijua tu hakuna kitakachopita
tutaacha na gesi iende bure bure
 
Bora tusiipate kabisa mpaka ccm itoke madarakani au tuwe na serikali mseto kwanza kubalance mambo.
 
kama tutafanikiwa kuandika katiba kwa kalamu ya kawaida tutamshukuru mungu. ni mara chache sana katiba inaandikwa kwa pen lazima iandikwe kwa damu (wino wa damu) au kwa sasa wemegundua wino mpya wa tindikali. naomba mungu atusaidie tupate katiba kama tuliyoipata mwaka 1961. na nina muombea kwa mungu rais awe na ujasili wa kufanya maamuzi ambayo hayatatuingiza kwenye machafuko yoyote ili tuandike katiba kwa Bic.
 
Wewe upo TZ au umekimbia kichapo cha JWTZ huko Congo. Unasema Warioba kalazimisha? Sikia KATIBA mpya si sera ya CCM hivyo hawajajipanga zaidi ya kutawaliwa na hofu, wao wameandaa waraka kwa vibaraka wao wa mabaraza ya katiba kupinga serikali tatu. Logic ya serikali tatu ni rahisi, ni kwamba hata sasa tunazo ila kwa uficho, kinachotakiwa ni kuweka bayana. Au hujui kuwa saiv tuna mambo ya Muungano, mambo ya Zanzibar na mambo yanayohusu Tanganyika yanayoshughulikiwa na serikali ya Muungano?
Toka Warioba alipolazimisha ishu ya Tanganyika iwe ndio main issue
nilijua tu hakuna kitakachopita
tutaacha na gesi iende bure bure
 
Mchakato wa kupata katiba mpya ni msimamo na ajenda ya kikwete kama rais na sio ccm! Wanaccm wengi wamejipanga kumkwamisha kikwete kuelekea kupata katiba mpya! Msaada pekee wa kikwete ni wapinzani pamoja na Ngo basi!
 
Wanabodi kinachoendelea ndani ya ukumbi wa bunge uliokarabatiwa kwa tsh bilion nane ni kuwatania wananchi.wajumbe hawako serious kuropoka ropoka wiki ya pili imeisha wamefanya jambo moja tu la kumchagua mwenyekiti wa muda na kamati ya kanun


Mambo mengine ni nje na lengo na madhumuni ya mkutano huo.suala la posho sio ajenda lkn hadi limetengenezewa kamati,hawaendani na muda wacku tisini uliopangwa.

Hii ni kuwapotezea watanzania raslimali zao.mimi nadhani serikali iachane na ongezeko la posho wanaloitaji hawa wajumbe..iwalipe walimu madai yao ya muda mrefu ili kukidhi matakwa ya brn.

Nchi hii itakua nchi ya posho hadi lini,watu wakikutana kidogo tu lazma walipane posho?????. hata kwa kazi ambayo ina kujengea heshima ktk jamii yako kua ulikua mmoja wa watu waliotengeneza katiba mpya.

Watu wa namna hii hawatufai,tungekua na rais mkali wajumbe hawa wangelipwa laki moja na kupelekwa kuishi hostel za udom ambako serikali ingewahudumia chakula na usafiri....

Hali hii tukiiacha iendelee watoto wa maskini wataisha kwa kua mfumo wa posho hautawafikia wao wako mbali na mfumo huuu thats why waliopo kwenye mfumo huu wanataka kuurithisha kwa watoto na ndugu zao refer sumari to sioyi,mgimwa to jofrey,makamba to mwezi wa kwanza,kj44 to riz,.....nk..huuu wote ni mfumo posho ndo unasababisha haya yote hakuna kitu kingine hapi.Tuupinge tuupinge tuupinge.
TUNATAKA KATIBA MPYA MSITUZINGUE
NYAMAKONGE
 
Hakika katiba mpya haipatikani na ikipatikana itakuwa yenye viraka mwili mzima na huenda muda nao usitoshe
 
Wakati wajumbe wa bunge la katiba wakilumbana kuhusu posho yao huko Dodoma. Nilikuwa najaribu kuangalia umri wa wengi wa wajumbe wa Bunge hilo naona wengi wao umri wao unaanzia miaka 55-90 na kuendelea mf. Lipumba, Mapalala, Mtikila, Kingunge, Paulo Kimiti,Chipaka Prof. Mahalu etc. na wengine sidhani kama wazee hawa kweli waaelewa changamoto ya Kundi kubwa la vijana ambao ni Asilimia 68 ya watu a taifa hili (kwa mujibu Sensa ya 2012). Binafsi naona mchakato huu ni bora liende tu. VJANA TUSITARAJIE JIPYA
 
halina tija, halina welekeo, halieleweki. mijadala iliyopo pale ni posho, miongozo, utaratibu na laghai nyingi. kwanini mambo haya yasingefanyiwa kazi katika utaratibu wa kawaida halafu pale bungeni iwe sehemu ya mijadala pevu ya katiba??? huu ni upotezaji wa muda, fedha na rasilimali zingine za wananchi maskini wa nchi hii ya tanzania.
 
Ndugu wananchi wenzangu tuvuajo jasho ili kupata mkte wetu wa kila siku tuendelee kupambana na maisha haya magumu yaliyoletwa na hawa wanokula pesa za nchi kwa kuhudhuria vikao vya matusi na ujuha.

Kiufupi ni kuwa Watanzania tumeishaliwa hakuna cha katiba wala nini....hata ikija katiba mpya haiwezi kutupunguzia ugumu wa maisha tulionao walala hoi,zaidi itakuwepo kwa maslahi ya wanaojiita wanasiasa,amka sasa fanya kazi kwa bidii ili familia isilale njaa

maisha yangu binafsi hayategemei katiba ya wanasiasa waliovimbiwa pesa za walipa kodi,nitapigana kuyashinda maisha haya magumu hata pasipo na katiba yoyote ilee.
 
kutokana na kinachoendelea ndani ya bunge ni matumizi mabaya ya fedha za watanzania ambao wapo wengne mpk sasa hawana madawa, shule za maana, vitabu, madawati na bado mpk sasa kuna wilaya hawana magari ya kubebea wagonjwa lakn kuna watu 601(wabunge) wanalipana zaid ya 300,000 kwa kukaa dakika 44 tu nchi hii inaelekea wapi nashauri siku ya ijumaa tuandamane kwenda kwa mkuu wa wilaya kushinikiza bunge livunjwe ili hela iliyobaki ifanyiwe mambo mengne ya maana hata nchi za wenzetu uarabuni walipata haki zao kupitia forumz kama hii hata sisi twaweza kujikomboa tumechoka
 
kutokana na kinachoendelea ndani ya bunge ni matumizi mabaya ya fedha za watanzania ambao wapo wengne mpk sasa hawana madawa, shule za maana, vitabu, madawati na bado mpk sasa kuna wilaya hawana magari ya kubebea wagonjwa lakn kuna watu 601(wabunge) wanalipana zaid ya 300,000 kwa kukaa dakika 44 tu nchi hii inaelekea wapi nashauri siku ya ijumaa tuandamane kwenda kwa mkuu wa wilaya kushinikiza bunge livunjwe ili hela iliyobaki ifanyiwe mambo mengne ya maana hata nchi za wenzetu uarabuni walipata haki zao kupitia forumz kama hii hata sisi twaweza kujikomboa tumechoka

It is a pity kuwa anguko la nchi hii linatokea kwenye mikono ya JK. Ametahadhalishwa several times kuwa yeye ni dhaifu na watu wengi. Sasa udhaifu unaleta anguko la nchi hii. Sidhani kama watu watakubali katiba ya CCM!
 
Ccm wanaleta uhuni .shame on them .nimechukia mpaka nikapata picha mwenyeketi kama vile yuko chooni anakamua Mavi mpaka anatoka jasho ,
 
Watz hawajui kudai haki zao, hapo ukisema maandamano nchi nzima polisi na hata jeshi watamwaga mitaani kupiga watu kutokana na kufuata amri za viongozi wa ccm. Na kwa bahati mbaya watz ndio waoga wa kupindukia hata kwenye haki yao hawathubutu kuwa ngangari. Wanajeshi watapewa hela kidogo kwa ajili ya umaskini wao na tamaa zao za mali watawasaliti wananchi na kukumbatia watawala dhalimu. Maana haiwezekani kile kinachoendelea bungenia wanakiona lakini wako tayari tuendelee kulipa kodi huku ikitumika vibaya na wao wanajaza mandugu zao nyumbani eti wanawasaidia kwani wanakuwa wamepewa pesa za wizi wa kodi za wananchi.
CCM wanachotambia na kucheza na nchi yetu ni kwaajili wanajua watawatumia wanajeshi na polisi kubaki madarakani. Lakini wakumbuke nchi hii ikiingia machafukoni hata hizo hela wanazopewa na mafisadi itakuwa ngumu kuzitumia.
 
wazo zuri, ila ungekuja na jina lako halisi ili tuone dhamira ya dhati toka kwako,,coz watz ni wanafiki sana hasa linapokuja ishu ya msingi kama hii ulilosema,,
hatupaswi kusbr makamabda kama slaa na mbowe kupaza sauti bali tuanze cc na majemedari wetu watuweke ulinzi nyuma yetu kipindi hiki
 
Ishu sio jina ni dhamira mkuu nitaandamana hata mwenyewe wait n u ill see
 
Nimebahatika kusoma michango mingi sana hapa Jamvuni juu ya suala zima la bunge la katiba na mambo mengine yanahusiana na mchakato mzima wa katiba mpya.

Nilichogundua ni kwamba wange wetu hatujaridhishwa na mchakato mzima unavyoenda, Tulikua na matarajio makubwa sana baada ya kuundwa kwa hili Bunge na kupatikana kwa mwenyekiti wa kasi na viwango kama alivyojinadi mzee wangu sitta.

Kutokana na kutoridhika na mwenendo mzima wa hili Jambo hasa baada ya hotuba ya mheshimiwa raisi tumeishia kulalamika kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari.

ooh sijui wanakula kodi zetu bure, ooh raisi amelazimisha matakwa ya ccm ya serikali mbili, ooh sitta anachemka. haya yote yataishia humu kwenye mitandao na itakua ubatili mtupu.

Lets make steps!!! Tuanzishe bunge la wananchi
 
Kabla ya Hotuba ya Rais kikwete Bunge lilionekana kama kuanza kupata suluhu ya kuendesha mambo kwa muafaka zaidi na hali ya utulivu ilianza kujitokeza.

Lakini baada ya Hotuba ya Warioba wanaccm wengi wakaonekana kuhamaki na kumtaka rais badala ya kutoa hotuba ya kufungua Bunge, amjibu Warioba kipengele kwa kipengele. Licha ya wachambuzi wa mambo kumuonya rais kutokufanya hivyo, rais alionekana kukubaliana na maoni ya baadhi wa wanachama wake na kwenda kuijadili hotuba ya warioba na kusisitiza msimamo wa chama chake.

Si hayo tu bali alijaribu kuonesha kuwa CCM wako wengi na wanaweza kuibadilisha rasimu yote na kwamba haiwezekanai watoke wapige kampeni ya nguvu rasimu ishindwe kupita!

Kuanzia hapo wajumbe wa CCM ndani ya Bunge la katiba wakaanza kuvunja ile misingi ya maridhiano kwa kuanza kufanya mambo ya hila na yanayoashiria kutumia uwingi wao kulimiliki Bunge maalumu. Mwenyekiti wa Bunge naye akaonekana kubadili msismamo wake wa kubalance uwakilishi ndani ya kamati mbali mbali za bunge. Yeye mwenyewe alijitapa baada ya rais kuhutubia kwamba atahakikisha anabalance kamati na majadiliano ili makundi mbalimbali yaweze kuwakilishwa.

Gafla amebadilika na kushindwa kutimiza ahadi yake kwa kigezo kwamba CCM ni wengi kwa hiyo lazima wadhibiti maeneo yote kwa sababu ndio hali halisi wanannchi walivyoamua. Kwanza hao CCM waliojazana huko bunge la katiba walichaguliwa na wananchi lini na wapi kwenda kuwawakilisha kwenye bunge la katiba? La pili, mbona tulivyoweka utaratibu wa kubalance gender hatukusema wananchi ndio waliamua kuwachagua wanaume kwa hivyo tuache ilivyo? Je Sitta anamini kabisa bila kubalance kamati zake kuna kitachoendelea? Moja ya hasara za kujaza CCM wengi ni kwamba kila jambo litakoletwa litatiliwa mashaka na upande mwingine.

Cha ajabu basi, ni kwamba badala ya hotuba ya Kikwete kuongeza mshikamano na maridhiano na kutoa dira ya namna ya kuvumiliana imekoleza hisia za uchama na ubabe wa tupo wengi. Na hii ndio maana wengi wakasema Kikwete alikwenda kuvunja bunge maalumu na sio kulizindua. Pinda mwnyewe amedhihirisha hili kwa kuonesha wasiwasi kwamba hakuna uwezekano wa kufikia maridhiano kuendana na hali ilivyo kwa sasa na bunge litaahirishwa!

Lawama zote kwa Kikwete, alionywa hakusikia! Nadhani pia mapigo ya Waznazibar ameanza kuyapata! yangu macho!
 
Back
Top Bottom