Hivi jamani mimi natatizwa sana na utendaji kazi wa Bunge letu tukufu.
Wakati Zito anatoa hoja ya Kuundwa Kamati ya Bunge juu ya buzwagi, wote tunafahamu walivyokuwa wanapondwa na yaliyojitokeza hadi kufungiwa kwake.
Ni kwa nini sasa hoja ya Richmond iliyotolewa na Mwana CCM imeungwa mkono na wote wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga na kuponda?
Je, ni kwa sababu imetolewa na mwanaCCM au ina mantiki kuliko ile ya Buzwagi?
Je, imefanyika hivyo baada ya wao kuona rais kaunda tume waliyokataa kuiunda?
Kulikoni?
Kuna shule kidogo unatakiwa kupatiwa;
1. Hoja ya kuundwa kamati ya Richmond ni hoja ya Bunge, kwa kuwa kamati ile ya Uchumi na Biashara ilikasimiwa madaraka na Bunge kuangalia mambo yote yanayohusu maeneo hayo... na ikaleta mapendekezo bungeni kwamba hawakuelewa jambo la Richmond na riport ya PPA na ya PCCB zinahitaji kuangaliwa zaidi kwa makini...
Hoja hii si ya Shelukindo!!! na wala si ya Mbunge wa CCM, kumbuka kwenye Kamati za Bunge zote zinawabunge wa Upinzani.
2. Hoja ya Buzwaji haijaundiwa tume wala kamati hata mpaka leo!!! ila unaweza kusema issue ya Buzwaji imesaidia kuweka mazingira ya kuunda
Tume ile ya Madini aliyounda rais hivi karibuni.
3. Nakumbuka hoja ya Richmond kuundiwa kamati haikuwahi kutolewa bungeni, ila kuna mizengwe ilifanyika mpaka hoja haikupelekwa bungeni.
4. Ni kweli kuna-issue ya wengi wape,,, maana ndio hivyo tena demokrasia pale bunge ni ya kura (waonunga mkono semeni ndiyooo, wasiounga semeni sio) sasa CCM wakisema ndio, mambo ndio hivyo tena, well, demokrasia yetu ni changa but we are improving slowly.
5. Zile kamati za Kudumu za Bunge zina nguvu kubwa sana kuliko mswada binafsi wa mbunge mmoja mmoja... but in short hakuna mbunge wa CCM ambaye ameleta mswada binafsi kwenye haya mambo mawili.