MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Kuna mvua usipime mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu kwenye kilimo mkuu, inaonekana ndiyo mara ya kwanza..
Mvua nyingi siyo kipimo cha mavuno kwa mazao...magonjwa yanaongezeka...
Jingine na usilime kutumia kalamu na daftari wala kwa simu...
Eti zile tuma hela ya kupalilia, tuma hela ya mbolea, UTAJUTA..
Mpunga unataka jua pia siyo maji tu...
Unataka dawa sometimes utoe maji uweke mbolea...
Kilimo kinahitaji uwepo ukague baadhi ya shughuli ujihakikishie zimetendeka..
Dakawa, Malinyi, Ifakara, Kilosa, Mvuha safari hii changamoto kwa Morogoro ni mvua zilizopita kiwango...

Kila la heri mkuu, mwaka mzuri ukilima eka 5 gunia 100-110 hukosi, mwaka wenye changamoto waweza kupata gunia 5 za kurudisha mbegu..

Everyday is Saturday........................ :cool:
 
Nimelima hekari tano za mpunga mkoani morogoro wilaya ya malinyi je naweza vuna gunia ngapi wakuu anisaidie kwa alie na uzoefu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na mfumo uliotumia katika kupanda, he umepanda Kisukuma au kutaalam? Kama Kisukuma utapata gunia kati ya 50-60 lakini kama umepanda kitaalam utapata kati ya gunia 125 na 150!
 
Jamani naomba kufahamu ukweli kuhusu Kilimo cha umwagiliaji cha mpunga nimepata taarifa sasa nahitaji kujua zaidi taarifa nilizopata nikwamba.kukodi hekta 1 ni 800,000/=Kulima 100,000/=,kurudia kulima 80000/=, Kupanda 180000, Mbolea 300000, kuvuna na mashine 180000 JUMLA ni kama 1700000.kwa kila hekta na Mavuno yanakisiwa 7.5 tani, Je hapa kuna ukweli naomba kama kuna mzoefu atupe ukweli wa hii skim

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani naomba kufahamu ukweli kuhusu Kilimo cha umwagiliaji cha mpunga nimepata taarifa sasa nahitaji kujua zaidi taarifa nilizopata nikwamba.kukodi hekta 1 ni 800,000/=Kulima 100,000/=,kurudia kulima 80000/=,Kupanda 180000,Mbolea 300000,kuvuna na mashine 180000 JUMLA ni kama 1700000.kwa kila hekta na Mavuno yanakisiwa 7.5 tani, Je hapa kuna ukweli naomba kama kuna mzoefu atupe ukweli wa hii skim

Sent using Jamii Forums mobile app
Cheki hiyo ukiwa na swali uliza.
Pady 1 = ekari 15
Chukua total ya pesa gawia 15 utapata jibu la kiasi cha pesa.
Bado moja kwa wastani ni gunia 250.
 

Attachments

  • RICE%20PADDY%20COST.2.xlsx
    10.9 KB · Views: 43
Unachokodi siyo hecta(eka 2)...uliza vizuri...kwa kawaida ni blocks za eka 15, labda ila inaonekana unashea na mtu, aliyekodi block.

Huwezi lima eka 15, kwa laki 1, na ukazirudia kwa 80K..kaulizie farm manager..

Everyday is Saturday..................... :cool:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom