Kwa anaefahamu vizuri...

luhota

Member
May 16, 2010
27
1
Ni kuhusu jina hili Idd Amin Dadaa. Kama sijakosea hiyo bold. hivi hilo neno dadaa lilitokana na nini? naamini ma great thinkers mtanisaidia kwa hilo..
asanteni sana
 
Uhindini - Dadaa linamaamisha "Babu" na uhindini hukohuko neno "mama" humaanisha - mjomba.
Kwa kiswahili hakuna neno dadaa kuna dada!
Kwa kiganda pia hakuna neno hilo ila inapatikana unubini - ni jina la heshima kwa mtawala ama mtu anaetoka katika koo za machifu.
Na waganda walilitamka na kuliandika kama dada na wakati mwingine dadda! Ila wanubi wao hutamka dadaa na wakiandika hivyo. Na kwa makabila ya Tanzania mathalani unyamwezini neno dada hutamkwa katika salamu na kwingineko mathalani 'panga dada' anasalimiwa mwanamume.. suala la majina na maana zake inategemea na lugha husika. ukichukulia lugha yako ndio iwe ya mwenzako iko siku utarusha ngumi ugenini!
 
Ni hivi; miaka ile ya 1970 wakati Amin alipoipindua serikali ya Obote na Obote kukimbilia Tz. Idi Amin aliichukia nchi yetu sana. Na ktk hilo vijineno vingi sana vilikuwa vikirushwa kati ya watawala hawa wawili, yaani Nyerere na Amin. Chuki hizi zilipelekea vamizi kuu mbili toka Uganda. Katika mojawapo wa vijineno vilikuwa hivi, "Nyerere wewe ni mzuri sana ungelikuwa mwanamke ningelikuoa" Amin huyo. Naye Nyerere alijibu hivi, ' Amin Dada...' Kuanzia hapo tukaanza kumwita kwa jina la Dadaa. Kuna majina mengine kama nduli, joka, nk.
 
me naona hii imekaa vizuri zaidi maana ina connection ya Idd Amini, Nyerere na vita kati ya uganda na tanzania thanx mkuuu
 
Hilo jina lilitokana na propaganda za mwalimu wakati anahalalisha kwenda kumdunda Iddi.Alitaka kuaminisha kuwa jamaa ni mbaya wa yote likiwemo la ushoga ndo maana alimwita dada
 
Back
Top Bottom