KWAAJILI YAKO MAIMUNA 🥹[emoji120]
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 13
MAWASILIANO: 0783642467
SONGA NAYO.......
Rajabu alitumia muda mrefu sana kumtuliza Nagma na kweli akatulia
Upande wa pili shoga yetu maimuna kazurula mitaa yote kila mwanaume wake aliyeenda alimkata akiwa ameshachoka na kukata tamaa alikumbuka na kuamua kurudi kwa mama rukia
"Makubwa......"
Alizungumza mama rukia baada ya kumuona maimuna
"Shikamoo mama....."
"Eeeh wacha weeeh na cheo nimepewa, nambie maimuna "
"[emoji4] nimekukumbuka sana, nikakumbuka na ndugu zangu nimekuja kuwaona "
"We umenikumbuka mimi au ? Ebu subili kwanza umenikumbuka na hayo mabegi yako au ??"
"[emoji23] mama rukia bhana "
Alijichekesha maimuna uku akiangalia uku na uku alitumia muda mwingi kuangalia nyumba yao iliyobomolewa ambayo kwa muda huo mafundi walikuwa bize na kichimba msingi wa Ramani mpya
"Kaka rajabu na shyna wako wapi au wametoka ??"
"We wale ndugu zako ??"
Yaani ma rukia alikuwa na majibu ya hapo kwa hapo
"Acha hizo mama rukia nimechoka ujue, nikaribishe basi, niweze kuzungumza na ndugu zangu "
"Mtoto huna haya wewe wala hujui vibaya, yaani kwa yule ambaye umemsema na kumtukana ukampa matusi yote, nikuambie kitu maimuna kati matusi yote tusi ambalo silisahau ni wewe kuniambia kuwa Nina mahusiano na Rajabu sikutaka kusema yote haya lakini pia niseme tu kuwa wewe kuwa yatima yaani kuwa mtu ambaye haujui ndugu zako upo upo tu unastahili kabisa na kama ndugu wapo bora wasijitokeze "
"Mama rukia mbona unaniambia maneno mazito sana ?? [emoji17] ata mimi ni binti sijapishana sana na mabinti zako sikupenda kuwa hivi mimi napenda sana kuwa na ndugu zangu, napenda sana kujua mama yangu,.kwanza kabisa naomba niambie ndugu zangu wako wapi ??"
"Ata me sijui wako wapi na wanaishi wapi wnaafanya nini sijui kwakweli "
"Unamaanisha hapa hawapo ??"
"Me mwenyeewe nina chumba na sebule ulitaka niwaweke wapi ? Kwanza unanipotezea muda ondoka "
Maimuna akapiga magoti akilia sana akiitaji msamaha na msaada kutoka kwa Mama rukia maana mpaka alipofikia hakuwa na msaada wa watu wengine....
Kelele za maimuna ziliwashtua majilani, walimzunguka maimuna ambaye aliendelea kulia na kuomba huruma ya mama rukia lakini mama rukia alikataa kabisa mpaka pale mwenyekiti alipomuomba mama rukia kumpokea tena maimuna.
Siku mbili zilipita ikiwa ni majila ya saa 1 usiku Nagma akiwa amekaa na familia yake mpya muda huo walishapata chakula cha usiku hivyo walikaa kuangalia TV wakipoteza poteza muda lily muda wote alikuwa kwenye mikono ya shyna yaani hakutaka kumuacha ata dakika....
"Weeh lily ebu muache antie sasa kaaaah muda wote uko mikononi "
"Muache bhana da nagma....."
"Nimekumbuka "
Alizungumza rajabu na kila mtu alimgeukia akisubili asungumze
"Shyna....."
"Abeeh kaka "
"Ata sijui naanzia wapi lakini naomba niende moja kwa moja, lily ni antie yako "
"Si ndio mbona ananiita antie tangu siku ya kwanza "
"Sijamaanisha hivyo namaanisha kuwa lily ni mtoto wangu mimi na wewe ni shangazi wa ukweli kabisa "
"Ahahahaha thubutu "
Shyna ni mimi kabisa aligoma kukubali
"Kwa ubishi sikushangai kwakuwa umezaliwa nao, najua unajiuliza kama lily ni mtoto wangu kwanini sikumleta kwa mama enzi za uhai wake, kiukweli nimejua juzi tu kuwa lily ni mtoto wangu, unajua nini siku ya kwanza nilihisi kuwa Nagma amechanganyikiwa lakini alikuwa na akili timamu huyu sio Nagma kaka unavyojua huyu anaitwa shenaya....."
"Subili kwanza, kaka naogopa natetemeka shenaya ni mwanamke wako ambaye aliwai kufariki ? Nakumbuka uli......"
"Najua unachanganyikiwa lakini nimeshajua ukweli nakuambia kila kitu mdogo wangu "
"Rajabu acha nitamwambia kila kitu....."
Alijibu Nagma kisha akakaa vizuri na kuanza kutoa hostoria ya nini kilitokea uko nyuma....
"Mimi ndo shenaya kama mnavyojua since familia yangu imekuwa ni yenye pesa mingi na mambo mengine tumekuwa tukikumbwa na na matatizo mengi sana aswaah ya chuki tulichukiwa mno, na adui zetu ni wale wafanybiashara wakubwa ambao walikuwa wakijumuika na baba katika plan zao za kuchukua kila kitu chetu kwanza kabisa walipanga kunimaliza mimi kwakuwa ndiye mrithi pekee wa mali za familia 🥹 nakumbuka nilishawai kunusulika kunywa sumu kwenye juice akiniwekea kwenye juice kwa kulipwa na watu hao lakini Mungu mkubwa sikunywa nilijua hayo nikiwa marekani, mara ya pili ilikuaa ni kipindi kile ambacho rajabu ulipambana na wale waliotaka kuniteka ndio maana nashindwa kukusahau [emoji24] mara ya tatu ndio ile tindikali ambayo iliharibu uso wangu [emoji17] na sehemu kubwa ya shingo yangu, niliwaishwa hospital na kwakuwa pesa zipo baba yangu akafanya utaratibu nikaamishwa nchi kimya kimya na taarifa za kifo changu kuzagaa, najua Rajabu uliumia sana, nilifanyiwa surgery na ilienda powa nikapatiwa sura mpya ambayo mnaiona sasa, imechukua muda sana kuwa hivi kipindi kile ambacho nilikuwa nimemwagia tindikali ndio kipindi ambacho nilikuwa na ujauzito [emoji4] rajabu alishatoa jina kwa binti yake, tulipanga mengi sana na rajabu "
Nagma akaanza kulia kwa sauti
"Kinachoniuma ata mama mkwe hakuwai kunijua hakuwai kumuona mjukuu wake shyna wifi yangu uwezi amini mtoto wangu nimekuja kumuona akiwa na mwaka mmoja na miezi 8 yaani nilijifungua kwa upasuaji tena kabla ya muda 🥹 hii yote kwaajili ya matibabu makubwa niliyokuwa nikiendelea nayo, nilipokuwa sawa nilibadilishwa Uraia na ata jina uwezi amini wazazi wangu wanaiogopa nchi yao kwa sasa ata mimi naogopa lakini hakuna mtu wa kunijua nashukuru ilo na nilirudi kwaajili ya kumkutanisha lily na baba yake lakini pia kumtafuta mtu nimpendaye, najua unawaza kwanini nilikuaa nikiishi na mtu mwingine, nimeishi nae tu lakini bado nilikuwa nikikutafuta tangu nimeishi na huyu mwanaume ni mateso tu.....
Basi shyna alimsogelea na kuanza kumbembeleza wifi yake
"Hujui tu natamani kulipiza kisasi kwani nawakumbuka waliofanya hivi, nakumbuka sura ya mtu ambaye alinimwagia tindikali 🥹 na namuona kila kona, lakini nani atanielewa nani atajua kuwa mimi ni shenaya familia yangu kila siku inaniambia niondoke lakini naondokaje nishapata familia yangu sidanganyi moyo wangu una kidonda kikubwa "
Lily alikua akilia tu baada ya kumuona mama yake analia
"Njoo mwanangu "
Rajabu alitaka kumbeba lily lakini lily alikataa rajabu aliumia mno lakini alielewa ilo...
"Nimekumbuka "
"Nini tena ??"
Alizungumza nagma na rajabu akauliza
"Kwakuaa familia yangu imekamilika sina budi kumchkua Raya aje kuishi na sisi hapa nyumbani "
"Raya ??
Rajabu alishtuka sana maana jina ilo alipaswa kupatiwa lily lakini leo anatajwa mtu mwingine ambaye hakuwa akimjua
"Ndio Raya ni mtoto wa maimuna namaanisha mtoto binti aliyeokotwa na mama yako 🥹 sijui kama mtanielewa nachanganyikiwa kabisa....."
Ata me mwandishi nachanganyikiwa bhana [emoji23][emoji1544].
ITAENDELEA