ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Jamani nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini wanaume huwa tunapenda sana, kila jambo baya linalohusiana na mapenzi, kuwazushia wanawake kuwa ndio chimbuko la matatizo. Kwa mfano utakuta mtu anafanya mapenzi na wanawake wengi lakini mwisho wa siku, yeye kama mwanaume anaona ni sawa kwake kufanya hivyo lakini kwa mwanamke anaona sio sahihi.
Kwa bahati mbaya sana hao wanaume ambao ndio mabingwa ktk kushawishi wanawake kufanya mapenzi ndio wanaokuwa mstari wa mbele sana kutangaza ubaya wa wanawake wanaotmbea nao. Wengi huwa wanapenda kuorodhesha idadi ya wanaume ambao mwanamke ametembea nao ili kuhalalisha kile anachokielezea.
Binafsi naomba tujiulize swali moja kabla ya kwenda mbali sana. Hivi umeshawahi kujiuliza au kupiga hesabu ya idadi ya wanawake ambao wewe kama mwanaume umeshawahi kutembea nao? Ni wangapi wako hai au wameshatangulia mbele za haki? je unajua huko waliko wameshakuongelea mabaya mangapi mbele za Mwenyezi Mungu, na je unajua adhabu inayokungojea kutokana na wewe kwa nmna moja au nyingine umepelekea kuwasababishia kukosa kuolewa? Na je umeshawahi kupiga hesabu kamili kujua idadi ya wanawake uliotembea nao tokea yule wa kwanza hadi ambaye pengine uko naye kitandani muda huu unaposoma thread hii?
Ukishajiuliza hayo maswali hapo juu na kupata majibu yake, jiulize swali hili la mwisho: Vipi kama hicho 'kitendea kazi' chako ndo kingekuwa kama sabuni, unadhani kwa idadi ya iliyowapitia, leo hii ungeendelea kuwa nacho? Jibu utakalolitoa kwa swali hili la mwisho likufundishe kujua kwamba kila mtu ana makosa na sio sahihi kuwasema wanawake tu kila mara wakati sisi wenyewe ndio washawishi wakubwa ktk mapenzi!!!