Kwa Ajili ya Wanaume tu!!!!!!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,974
1,640
Jamani nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini wanaume huwa tunapenda sana, kila jambo baya linalohusiana na mapenzi, kuwazushia wanawake kuwa ndio chimbuko la matatizo. Kwa mfano utakuta mtu anafanya mapenzi na wanawake wengi lakini mwisho wa siku, yeye kama mwanaume anaona ni sawa kwake kufanya hivyo lakini kwa mwanamke anaona sio sahihi.

Kwa bahati mbaya sana hao wanaume ambao ndio mabingwa ktk kushawishi wanawake kufanya mapenzi ndio wanaokuwa mstari wa mbele sana kutangaza ubaya wa wanawake wanaotmbea nao. Wengi huwa wanapenda kuorodhesha idadi ya wanaume ambao mwanamke ametembea nao ili kuhalalisha kile anachokielezea.

Binafsi naomba tujiulize swali moja kabla ya kwenda mbali sana. Hivi umeshawahi kujiuliza au kupiga hesabu ya idadi ya wanawake ambao wewe kama mwanaume umeshawahi kutembea nao? Ni wangapi wako hai au wameshatangulia mbele za haki? je unajua huko waliko wameshakuongelea mabaya mangapi mbele za Mwenyezi Mungu, na je unajua adhabu inayokungojea kutokana na wewe kwa nmna moja au nyingine umepelekea kuwasababishia kukosa kuolewa? Na je umeshawahi kupiga hesabu kamili kujua idadi ya wanawake uliotembea nao tokea yule wa kwanza hadi ambaye pengine uko naye kitandani muda huu unaposoma thread hii?

Ukishajiuliza hayo maswali hapo juu na kupata majibu yake, jiulize swali hili la mwisho: Vipi kama hicho 'kitendea kazi' chako ndo kingekuwa kama sabuni, unadhani kwa idadi ya iliyowapitia, leo hii ungeendelea kuwa nacho? Jibu utakalolitoa kwa swali hili la mwisho likufundishe kujua kwamba kila mtu ana makosa na sio sahihi kuwasema wanawake tu kila mara wakati sisi wenyewe ndio washawishi wakubwa ktk mapenzi!!!
 

fau60.

Member
Sep 14, 2011
17
2
kaka ushashkwa maskio nin.? dah.. na aliekuska kama co mmbenga bas hakiwii kuwa mtoto wa mganga, coz n ajab.
 

King’asti

Platinum Member
Nov 26, 2009
27,800
24,544
ndyoko,unamuona na huyu? anadhani umekula limbwata. hivi kwa nini mko hivyo wanaume?
(ukimaliza hii wafungulie uzi wanawake wanaoendaga kuchungulia jandoni)
kaka ushashkwa maskio nin.? dah.. na aliekuska kama co mmbenga bas hakiwii kuwa mtoto wa mganga, coz n ajab.
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,904
Sorry wajamen, najua ni kwa ajili ya wanaume tu lkn nimeshindwa kuvumilia,asante sana Mkuu Ndyoko, mungu akubariki sana wewe na kizazi chako chote kwa kuweka huo uzi hapo ili hawa wanaume wasome na kujitambua na kubadilika kwa wale ambao hawakulijua hili,amen.
 

Msikilizaji

Member
Nov 6, 2008
51
8
Kaka Ndyoko naona you have come to your senses maana wanao enda kinondoni kufata madada poa ni wale wale wakaka
 

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,747
6,553
ata wazazi wakiona mtoto wao wakiume anakaakaa nyumban wanatilia shaka uwezo wake ktk kusaka mabinti.mwanaume kujishughulisha.
 

Ndetirima

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
981
727
Wanaume siku zote ni wababe. Mungu alimuumba mtu Mume wa kwanza halafu baadae akamfanyia msaidizi kwa kutumia ubavu wake Adam ndiyo maana hadi leo ubabe upo na utaendelea kuwepo. Kama Mungu angemuumba Mtu Mke kwanza ingekuwa kinyume chake tungekuwa tunaolewa, tunatongozwa na mambo mengine mengi ingawa kutongozwa na kuolewa wanaume ipo siku hizi lakini sio sana.
 

Qulfayaqul

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
480
84
Mimi huwa siwasemi vibaya sanasana huwa nawapenda sana wale kina dada ambao hawana complication, sio demu unatongoza miezi kibao utafikiri unachimba dhahabu, halafu ukipata siku moja tu umekinai, kama kizuri kizuri tu asikwambie mtu, hata kama kinatumika sana. Ni mtazamo tu.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom