Kuzuru Tz

frakerg

Member
Jan 15, 2014
15
4
Habari za mchana wanajamvi?

Uzi huu ni wa pili katika hili jukwaa nikitafuta ushauri kuhusu suala hili. Akhsante kwa walionishauri katika uzi wa kwanza. https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/917117-kuzuru-dar.html Kwa kifupi mimi ni Mkenya mzawa wa jiji la Nairobi na nimepanga mikakati ya kuzuru TZ kulingana na udadisi nilioufanya katika mitandao ya kompyuta. Hii itakuwa mara yangu ya kwanza kuzuru Tz. Mpangilio wangu wa ziara hii hi kama ifuatavyo

27 Dec: Nitazuru na nilale Moshi

28 Dec: Nitazuru na nilale Arusha

29 Dec: Nitazuru na nilale Dodoma

30 Dec: Nitazuru na nilale Dar es Salaam

31 Dec & 1st Jan: Nitazuru nilale siku mbili Zanzibar

2nd Jan: Nitakuwa Tanga beach: Nitafika jioni nipumzike kwa beach Kisha niamkie safari ya kurudi Mombasa

Ist Jan: Nitarejea Nairobi.

Hii hapa ni ramani ya hii safari.

http://www.JamiiForums.com.com/index.php?attachments/mkufuu-tour-png.24842/

Nitasafiri kwa motokaa. Mafuta yatakayotumika ni ya takriban shillingi elfu kumi na tano (Ksh 15,000 au ukipenda Tshs 131,000) Sina uhakika yatatosha. Sijui bei ya petroli TZ ni shiringi ngapi hapa kenya ni Ksh 90.4 au tshs 1880 kwa lita moja.

Lengo kuu la hii safari ni kujivinjari na kujiunga na watanzania kwa kuadhimisha mwaka mpya 2016. Kama uonavyo kwa ratiba niliyoichapisha, mkesha wa mwaka mpya 2016 nitakuwa Zanzibar natumai usiku wa tarehe mosi 2016 nitakuwa pale forodhani Zanzibar nikila pizza ya zanzibari.

Ningependa sana kupata ushauri kuhusu mahala pazuri pa kujivinjari katika safari hii. Akhsante.


Ps: Nimetafuta ushauri pia katika jukwaa letu la kenya (JamiiForums.com.com) katika uzi huu hapa http://www.JamiiForums.com.com/index.php?threads/kuzuru-tz-ii.14814/


 
Nakutakia matembezi/tour nzuri tz.Uwe mwangalifu, wakora wa Nairobi wapo pia kwenye miji
mikubwa tz.Fanya editing kwenye ratiba sehemu ya mwisho. Huwezi kula xmas na mwaka mpya tz halafu urudi Nairobi tarehe 3/12!
 
Nakutakia matembezi/tour nzuri tz.Uwe mwangalifu, wakora wa Nairobi wapo pia kwenye miji
mikubwa tz.Fanya editing kwenye ratiba sehemu ya mwisho. Huwezi kula xmas na mwaka mpya tz halafu urudi Nairobi tarehe 3/12!
Akhsante Mkuu...Nimekosoa. Ningependa kujua utaratibu unaofuatwa kuingia Zanzibar kwa wageni wasiokuwa watanzania kutoka upande wa Dar.
 
Back
Top Bottom