Kuzungushwa malipo

Kuzungushwa malipo

understanding

Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
75
Reaction score
34
Tunaomba kujulisha umma tena kwa masikitiko makubwa kwamba centre ya utamaduni ya kifaransa ijulikanayo kama alliancefrancaise, na British council waingereza wanawanyanyasa na kuwadhulumu watanzania.

Tunaomba ifahamike kuwa, centre hizo zilifanya tamasha kubwa la muziki mwezi wa sita viwanja vya posta mwenge, walihitaji huduma mbalimbali kutoka kwa suppliers na waliwa contact na suppliers walihakikisha wanatoa huduma.

La kushangaza ni kwamba, hadi sasa, hakuna malipo yaliyofanyika mbali na wao kufahamu kwamba huduma zote hutolewa kwa wakati na sasa ni miezi miwili tangu shughuli kufanyika. Tumekuwa tukipata ahadi hewa kila siku na la kushangaza wahusika wote wameenda likizo huku wakijua hawafanya malipo na kuacha ofisi zao bila majibu.

Tumefanya jitihada za kuwaona wadhamini wao wakuu kwa wakati tofauti, SBC na Fastjet na kuwaambiwa kuwa tamasha hilo lilidhaminiwa na wao na walishakamilisha udhamini wao siku nyingi. pia tulifika kiwanja cha posta hapo na kuambiwa hata walinzi pia hawakumaliziwa sehemu ya malipo yao japo walifanya kazi tena ya ziada.

Tunaomba kusaidiwa na wahusika na vyombo husika kwani huu ni unyanyasaji na sio haki hata kidogo.
 
Kama mna mikataba halali ya hiyo kazi nashauri muipeleke kwenye vyombo husika walishughulikie

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hekimatele @

All said in a deep tone with authority character!!!
Understanding@fuata hii maneno

Itachukua muda ila mtalipwa,kufanya kazi na taasisi ni kama kuweka hela benki HAIPOTEI,umejaribu pia kuwaandikia kupitia balozi zao????Tricky hapa ni kiwa ubalozi utawashurutisha kulipa ili kutunza diplomatic cosmetic.

Kabla ya kuwaburuza mahakamani jaribu njia zote mbadala kwanza!!!!
 
Back
Top Bottom