maliyamungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 564
- 412
Mimi ni kiongozi wa Kanisa hapa Dar Leo nafungua Vyombo vya Habari nakuta unasema mikusanyiko ya Mkesha wa Mwaka Mpya kwenye viwanja Vya wazi marufuku.
Leo tarehe 31/12/2020 narudia Leo unatoa Tamko wakati sisi tumepanga jambo tokea Novemba. Tumekodi vyombo vya muziki, tumelipia Eneo, tumelipa watu wa vyakula, tumelipa waimbaji wa Injili n.k. Leo unatoa tamko, kweli ni sawa masaa kadhaa kabla ya mkesha?
Hebu tuoneeni huruma kama Watanzania wenzenu. Mkipata madaraka msiwe washamba, mnamkwamisha Mh. Rais. Watu tunajenga chuki sababu ya ujinga wenu mawaziri, matamko kila siku; ubabe tu na kutishiana. Mnataka tufe kwa presha ndio muwe na Amani ya mioyo yenu? Sio sawa jamani, tusiishi kwa kukomoana.
Madaraka yana mwisho kuna siku mtakuja makanisani kutubu dhambi zenu. Acheni ushamba wa madaraka.