Kuzuiwa kwa mikusanyiko mwisho wa Mwaka: Kilio kwa Waziri Simbachawene

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
557
500
Mimi ni kiongozi wa Kanisa hapa Dar Leo nafungua Vyombo vya Habari nakuta unasema mikusanyiko ya Mkesha wa Mwaka Mpya kwenye viwanja Vya wazi marufuku.

Leo tarehe 31/12/2020 narudia Leo unatoa Tamko wakati sisi tumepanga jambo tokea Novemba. Tumekodi vyombo vya muziki, tumelipia Eneo, tumelipa watu wa vyakula, tumelipa waimbaji wa Injili n.k. Leo unatoa tamko, kweli ni sawa masaa kadhaa kabla ya mkesha?

Hebu tuoneeni huruma kama Watanzania wenzenu. Mkipata madaraka msiwe washamba, mnamkwamisha Mh. Rais. Watu tunajenga chuki sababu ya ujinga wenu mawaziri, matamko kila siku; ubabe tu na kutishiana. Mnataka tufe kwa presha ndio muwe na Amani ya mioyo yenu? Sio sawa jamani, tusiishi kwa kukomoana.

Madaraka yana mwisho kuna siku mtakuja makanisani kutubu dhambi zenu. Acheni ushamba wa madaraka.
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
624
1,000
Mpaka uambiwe kuna korona na mikusanyiko ya aina hio haikubaliki, jaribuni kuyafahamu kwa kina baazi ya mambo.

Kiswahili sanifu ..Jiongezeni...tunasema Tanzania hakuja korona lakini sio kama kweli hakuja idadi ya mwisho watu 500 walikuwepo hospitali hadi hii leo hawajatolewa tamko wapo wapi,
 

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
557
500
Mpaka uambiwe kuna korona na mikusanyiko ya aina hio haikubaliki,jaribuni kuyafahamu kwa kina baazi ya mambo.
Kiswahili sanifu ..Jiongezeni...tunasema Tanzania hakuja korona lakini sio kama kweli hakuja idadi ya mwisho watu 500 walikuwepo hospitali hadi hii leo hawajatolewa tamko wapo wapi,

Nimekuelewa sana tena sana Mtumishi.
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,496
2,000
Mimi ni kiongozi wa kanisa hapa Dar Leo nafungua vyombo Vya habari unasema mikusanyiko ya Mkesha wa mwaka mpya kwenye viwanja Vya wazi marufuku, Leo tarehe 31/12/2020 narudia Leo unatoa Tamko wakati sisi tumepanga jambo tokea November tumekodi vyombo Vya mziki tumelipia Eneo tumelipa watu wa vyakula tumelipa waimbaji wa injili Nk Leo unatoa tamko kweli ni sawa masaa kazaa kabla ya mkesha....
Kamshtakie Mungu!

Unapataje hasara kwenye Kazi ya Mungu..!? We kuandaa tamasha la bure na lisifanyike unaona hasara wewe..!? Na wanaotoa sadaka kila siku na hawaoni faida!? Majirani zao wanakufa kwa njaa, kando ya Kanisa kuna bibi na mama mjane hawana hata uwezo wa kupata chakula, kuna watoto wanasali kanisani hawana ada...! Na sadaka twatoa kila siku ili kuwafikia wasiojiweza bila mafanikio...

Happy new year..
 

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
557
500
Kiongozi wa kanisa unatumia maneno kama ushamba, ujinga, kufa kwa presha!!?? wewe ni Dj mzee acha kuzuga
Kiongozi wa dini hujui kusamehe Saba mara 70

Ok ngoja nijibu unavyotaka Sababu sina Roho

Ok simbachawene kafanya vizuri sana
Hasara niliopata Safi sana
Bwana Yesu msamehe
 

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
557
500
Kamshtakie Mungu!

Unapataje hasara kwenye Kazi ya Mungu..!? We kuandaa tamasha la bure na lisifanyike unaona hasara wewe..!? Na wanaotoa sadaka kila siku na hawaoni faida!? Majirani zao wanakufa kwa njaa, kando ya Kanisa kuna bibi na mama mjane hawana hata uwezo wa kupata chakula, kuna watoto wanasali kanisani hawana ada...! Na sadaka twatoa kila siku ili kuwafikia wasiojiweza bila mafanikio...

Happy new year..

Bwana Yesu akuponye na Pepo la kuhukumu.
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,801
2,000
Mtumishi ebu soma tangazo hili kwanza

2652614_DC3CBBCD-5DAC-417A-9C7E-858578EF3DD4.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom