Kuzuia mchanga wa madini na kuzuia madini yasitoke kipi kianze?

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Najiuliza sana sina majibu... hivi kama kilo moja ya dhahabu ina gharama kubwa kiasi hicho (wajuvi mtanijuza thamani halisi kwa sasa ya 1kg ya Aurum _Ag _dhahabu), kwa nini tusizuie kwanza hii mambo isitoke mpaka tujiridhishe tunapata benefit kiasi gani kwa dhahabu kutoka kabla hatujahamia kwenye mabaki yake? ni sawa na kuzuia chupa tupu za maji zisikusanywe wakati maji yashanywewa... nashauri mlalahoi mimi tuzuie kwanza madini ndiyo mchanga ufuatie... Ag (gold) inapanda ndege mabaki yanapanda meli...tunahangaika na offols, hatushangai?
 
Mkuu nchi yetu ni kichwa cha Mwendawzimu. Wameshupalia mchanga lakini mikataba ya madini bado hawataki kuiweka hadharani ili Watanzania tuone jinsi ambavyo haina maslahi kwa Watanzania. Hata kama hawataki kuiweka hadharani basi waipeleke Bungeni ili Wabunge wakaichambue na kuijadili.

Najiuliza sana sina majibu... hivi kama kilo moja ya dhahabu ina gharama kubwa kiasi hicho (wajuvi mtanijuza thamani halisi kwa sasa ya 1kg ya dhahabu), kwa nini tusizuie kwanza hii mambo isitoke mpaka tujiridhishe tunapata benefit kiasi gani kwa dhahabu kutoka kabla hatujahamia kwenye mabaki yake? ni sawa na kuzuia chupa tupu za maji zisikusanywe wakati maji yashanywewa... nashauri mlalahoi mimi tuzuie kwanza madini dniyo mchanga ufuatie... Ag (gold) inapanda ndege mabaki yanapanda meli...tunahangaika na offols, hatushangai?
 
01042017kp-jpg.490469

Najiuliza sana sina majibu... hivi kama kilo moja ya dhahabu ina gharama kubwa kiasi hicho (wajuvi mtanijuza thamani halisi kwa sasa ya 1kg ya Aurum _Ag _dhahabu), kwa nini tusizuie kwanza hii mambo isitoke mpaka tujiridhishe tunapata benefit kiasi gani kwa dhahabu kutoka kabla hatujahamia kwenye mabaki yake? ni sawa na kuzuia chupa tupu za maji zisikusanywe wakati maji yashanywewa... nashauri mlalahoi mimi tuzuie kwanza madini ndiyo mchanga ufuatie... Ag (gold) inapanda ndege mabaki yanapanda meli...tunahangaika na offols, hatushangai?
 
Attachments

  • 01042017kp.jpg
    01042017kp.jpg
    30.9 KB · Views: 104
Mh! kwan ukikosoa serikali si wanaweza kukukamata? Mi naogopa ila nimewahi kufanya kazi kwenye kampuni moja inayohusika na mambo ya madini, jamaa wana hela hao hatari, yaani dhahabu inasafirishwa inaenda kusafishwa ile wanaita refinment sijui, nje huko halafu ndo inaenda kuuzwa, ukiambiwa bei ya carat moja utachoka halafu carat ni kipimo kidogo sana, ukija kwenye kilo moja, bei ni nzuri sana we acha tu, acheni dhahabu iitwe dhahabu
 
Nchi ya kichwa cha mwendawazimu hii! Badala ya kungangamara na mikataba ya madini ili ifumuliwe upya kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wako busy na kelele za mchanga! Madini yanachukuliwa bure kabisa bila manufaa yoyote kwa nchi wako busy wanashupalia mchanga!

Kuzuia mchanga ni sawa na Kuzuia mabaki ya chakula mezani.
 
Nchi ya kichwa cha mwendawazimu hii! Badala ya kungangamara na mikataba ya madini ili ifumuliwe upya kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wako busy na kelele za mchanga! Madini yanachukuliwa bure kabisa bila manufaa yoyote kwa nchi wako busy wanashupalia mchanga!
sasa sijui tatizo ni watawala au ni wananchi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo kubwa la nchi yetu Mkuu ni hawa waliojivalisha ngozi ya uongozi wakati hawana dhamira ya kweli ya kutuongoza kwa faida ya Tanzania na Watanzania.
Ni kweli mkuu lakini upande wa raia nako kuna tatizo, yaani ukianza kufanya reasoning ndogo tu kama hii kuhusu mchanga na dhahabu, jamii nzima inakuona mpinzani, watakuita majina yote na wanaoweza kureason huko mitaani ni wachache sana, mabadiliko lazima yaanze kwa mtu mmoja mmoja then hata akitokea wa kupaza sauti, anakuwa na watu wanaomuunga mkono... nafikiri illiteracy ya wengi ndiyo mtaji wa hawa watawala
 
Nchi ya kichwa cha mwendawazimu hii! Badala ya kungangamara na mikataba ya madini ili ifumuliwe upya kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wako busy na kelele za mchanga! Madini yanachukuliwa bure kabisa bila manufaa yoyote kwa nchi wako busy wanashupalia mchanga!
Wanahangaika na moshi badala ya kuzima moto.
 
Back
Top Bottom