Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,678
119,311
Wanabodi,

Kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na panapostahili ushauri au angalizo tutoe.

Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, ni kitendo cha kizalendo na kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, na madini mengine mengi kwa kiwango kidogo ila yana thamani kubwa, tena ili kutuibia bila sisi kushtuka, mchanga huo wanauita copper concentrate, wakati in reality ni gold concentrate.

Nimekiita ni kitendo cha kizalendo na kishujaa kwa sababu kinagusa maslahi ya wakubwa, hivyo tutatikiswa na kupewa misukusuko na wakubwa hawa. Inahitaji uzalendo wa kweli kuingilia kati utekelezaji wa mikataba ya kinyonyaji iliongiwa na watangulizi wake au kwa ujinga wa kutojua tunaibiwa, au kwa maslahi ya matumbo yao.

Kisingizio cha kuibiwa huku ni hoja kuwa Tanzania hatuna uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba, fedha, na madini mengine toka katika mchanga huo.

Tena sio tu ni Tanzania pekee ndio tumeelezwa kuwa hatuna, uwezo huo, bali wakoloni mamboleo hawa na mabeberu, wametengeza mfumuko kuhakikisha mitambo hiyo haipo bara zima la África lenye dhahabu, kisha kwenda kusimika mitambo hiyo nchini Japan ambako hawana hata tone la dhahabu.

Wenye smelter za uwezo huo ni wale wale mataifa makubwa kiuchumi, the big 5. Marekani, Japan, China Urusi na Ujerumani ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor. Mfano kuna kanchi kadogo sana kanaitwa Uswiss hakana hata tone la dhahabu lakini kanazo smelter 5.

Irani ilipotaka kutengeneza reactor iliipata, Sadam Husein wa Iraq nae aliipata na kwa nchi za Afrika, Muamar Gaddafi alishungulikiwa, hivyo wakubwa hawa wakisikia Tanzania tuna mpango wa kununua smelter ili angalau mchanga wa Afrika uchenjuliwe Africa, wakubwa hawa hawatakubali, hivyo kwa uamuzi huu, Magufuli anahitaji sala zaidi ya pongezi tuu ili aweze kuyaweza yote katika YEYE amtiaye nguvu.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe tuu mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kabisa kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo wa ndani wa kuyachimba, bahati mbaya Nyerere alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata just a peanut huku wenye migodi wakikomba kila kitu na kuishia na faida yote huku wakituachia mashimo! .

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania kwa hivi tulivyo sasa, bado hatuna uwezo huo rais wetu Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo nchi kama za Ghana na África Kusini ambazo ziko kwenye top 10 bora za uzalishaji wa dhahabu, bado hazijawa na uwezo wa kuwa na smelter hizo, what are the chances kwa Tanzania kujenga smelter kwa sio kwa uwezo gani bali kwa mchanga gani wa kuutengenezea smelter.

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.

Wachumi wa sekta ya madini humu JF, hebu tusaidieni kwenye hili, je kwa umeme huu, wa gridi ya taifa na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo je Tanzania tunaweza? Unless tununue vile vi smelter vidogo tuuchenjue wenyewe mchanga wetu kidogo kidogo na vi smelter vidogo, huwezi kuchenjua kila kitu. Ukichenjua mchanga kidogo, the economics of scales inaingilia kati kwa the cost of extraction kuwa ni kubwa kuliko the byproducts za kitakachopatikana.

Piga ua galagaza, tumezua mchanga kwa mbwembwe nyingi, lakini tukilambishwa tuu asali, mtashuhudia tutaendelea kusafirisha mchanga na tutaendelea kuibiwa unless tuvunje mikataba!.

Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu?

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, tende kabisa kwenye mikataba yenyewe ya madini, ni mikataba ya kinyonyaji, na tusiishie kwenye madini tuu, kwanini tusiende hadi kwenye gesi asili maana huko nako nako tunaibiwa kweli kweli kwa vile hatuna hili wala lile.
Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa kisingizio hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu cha gesi, what are the chances ya kumiliki smelter.

Sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yetu yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu cha gesi, what are the chances ya kumiliki gold smelter la kiwango cha nuclear power reactor?

Niliwahi kushauri
Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. ..

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu tuu, huku tunaendelea kuibiwa kwenye dhahabu zenyewe!. Watanzania tunaibiwa kwenye Tanzanites, tunaibiwa kwenye gesi, tunaibiwa kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa migodini huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.

To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo wa ndani kwa Watanzania kukopa na kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
 
Nadhani walioruhusu mchanga kuondokana wangali HAI na mmoja wao ni Mh Benjamin Mkapa. Hebu asijifanye yeye ni "Alfa na Omega"

Na kama ana NIA ya DHATI ya kuuzuia mchanga basi asitumie mabavu. Dunia ya Leo ni ya watu wenye maarifa na weledi, "misuli" haina nafasi. Achukue ushauri wa Mh Tundu Lissu.
 
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Hala hala na hizi zisije kuwa ni siasa! .

Paskali

Siyo kweli kwamba AK hawana huo uwezo na wala AK hasafirishi mchanga nje ya kama hapa Tanzania, bali AK anaexport processed products na ndiyo iliyojenga Johannesburg na Uchumi wa AK kwa ujumla ambao ni first world economy vile vile Johannesburg Stock exchange ipo kwenye Top ten Duniani kwa thamani hivyo jielimishe tena Mzungu wa AK hawezi kukubali huu ujinga!

Unaijua historia ya madini ya Platini AK ambayo yana thamani klk dhahabu? Ni kwamba walianza kwa lengo la kuchimba dhahabu lkn baada ya kuchunguza ule mchanga wakagundua una madini mengi ya Platini klk dhahabu wakabadilisha na kuanza kuprocess Platin, na AK ndiyo mmoja kati ya number one exporter wa Platini Duniani, khs matumizi ya Platin nakuachia ujitafutie ...

Ngoja nikuulize swali dogo sana, Tanzania ni ya 3/4 kwa kuzalisha dhahabu, Je tunaexport kwenda nchi gani? Ni nchi ipi inayonunua dhahabu yetu? Hii ni lazima tuwe tunajua kwamba dhahabu ya Tanzania inakuwa exported to countr xyz!
 
Ivi mnawezaje kuzuia wakati mna mikataba na wawekezaji???.. Acacia wanalalamika wamepata hasara ya 40b kwa 2 wks toka order imetolewa...
Kesho wakienda mahakamani tunawalipa hela nyingi kwa kuvunja mikataba.
Kwa nini kama serikali wasikae hao wawekezaji waone wanachaweza kupata na mwisho kuboresha maslahi ya wa Tanzania kwenye kupata ajira...
Hii awamu italeta kesi nyingi saana na tutashindwa wote kwenye mahakama za kimataifa!.
Kikwete alipoingia alikuta mrahaba wa madini ni 3%..ila mbona hakufunga migodi zaid walikaa na kuangalia kuwa tunapunjwa.
Kufunga/kuzuia bado hujatoa suluhisho maana watu wamewekeza saana kwenye hizi shughuli!..
Sheria za kimataifa zinaruhusu kupitia upya mikataba.hiyo ndo best way.
Maana kama kuzuia ilishawahi kuzuiliwa
Tuwe na sera na sio kukulupuka kufanya maamuzi bila kuangalia athari zake!.
 
Hii nchi ina maeneo mengi yenye mashaka..kumbuka tumepita awamu nne na tatu ni miaka kumi kumi..jumla 30..makosa mengi yalifanyika na ilionekana kawaida..sababu wanasiasa wenyewe walikuwa wanufaika wa kwanza..yaani familia zao kwanza nchi badae..
JPM ameanza kubadili upepo maeneo mengi likiwemo hilo la madini..lakini huwezi Fanya kila kitu kwa siku moja kama ambavyo akili za watanzania wenzetu wengine wanavyodhani..
La msingi ni kuunga mkono hizi jitihada maana magufuli kabla haujamuambia yeye anajua na kufikiria and beyond..
Ndani ya kipindi cha miaka minne hakuna kitakachosalia..mwaka wa tank atakuwa anaziba ziba viraka tu..akisubiri nngwe nyingine ya urais..
Kinachoendelea kwa sasa ni jungu kuu tu..
 
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Hala hala na hizi zisije kuwa ni siasa! .

Paskali
Na siku tunalipa mabilioni ya dola kama fidia kule ICSID ushangilie hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom