Elections 2010 Kuzomewa kwa CHADEMA wakitoka bungeni

agwedegwede

Member
Jan 12, 2011
42
24
Ndugu wana jamii wenzangu, jana wakati Chadema wanatoka Bungeni kupinga mabadiliko ya kanuni kuhusu tafsiri ya neno KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI wabunge wengine waliwazomea, kwa mimi nilisikia mwishoni wakati wabunge wanatoka Sauti ya Spika wa Bunge nae alizomea au kutoa neno la kejeli kwa Chadema, sikumbuki vizuri hapo, ila ilinishtua kusikia sauti ya Spika nae kwenye mkumbo wa kuzomea.

Mnalionaje hili wana Jamii wenzangu, naomba tulijadili na kama kuna mmoja wetu ana hiyo Clip naomba aiweke ili tuisikilize kwa makini, ila mimi nilisikia kuna sauti ya Spika pia akitoa kejeli kwa wabunge wa CHADEMA.

Naomba kutoa Hoja.
 
Spika =ccm=cuf=udp=nccr=hamad rashid=kafulila.
kwa hiyo kama naye alizomea majibu ni hayo juu,ila wajue yanamwisho hayo.
 
YANGA vs SIMBA

Zomea zomea haiepukiki toka upande wowote unaofurahishwa na jambo linalotokea wakati ule
 
hapana mimi nilisikia wabunge wakishangilia kwa nguvu wabunge wa CDM wakiongozwa na mwenyekiti mbowe wakati wakitoka nje, bunge liliwapongeza kwa uamuzi wao wa busara sana...bwaha hahaha
 
YANGA vs SIMBA

Zomea zomea haiepukiki toka upande wowote unaofurahishwa na jambo linalotokea wakati ule

Lakini kwa SPIKA kuzomea kama kweli alifanya hivyo alifanya kosa. Ni sawa na refa wa mechi ya mpira wa miguu kushangilia timu moja ikifungwa. Lazima kuwe na kasora hapo
 
Nilisikia nikaishiwa nguvu sikutegemea wabunge wanaweza behave vile kwani hata watoto wa nursery wangekuwa na some ustaarabu...
 
nilisikia nikaishiwa nguvu sikutegemea wabunge wanaweza behave vile kwani hata watoto wa nursery wangekuwa na some ustaarabu...
kwani wabunge wa ccm kunamtu pale na ndo maana huwa wanatoa maamuuuzi hovyo sana!
 
Kuna vijimbe kadhaa vilisikika ambavyo vina ukweli ndani yake! Aidha hata hao wabunge wa Chadema walionekana kufurahia hatua yao!
 
CCM kwa ushamba wao wanaipandisha chati CDM, kama kuna mtu alikuwa ana wasi wasi kuwa vyama vya CUF, TLP & NCCR- Mageuzi ni matawi ya CCM, sasa amepata uthibitisho
 
Lakini kwa SPIKA kuzomea kama kweli alifanya hivyo alifanya kosa. Ni sawa na refa wa mechi ya mpira wa miguu kushangilia timu moja ikifungwa. Lazima kuwe na kasora hapo

Kwani wewe huoni spika akipinga ama akitaka kumkataza kitu mbunge wa chadema anavyoongea kwa jazba..; hata anahema kwa tabu.. anaonekana wazi kuwa na hasira na wabunge wa cdm... tuendelee kuangalia tutaujua mwisho wake tu... Aghhhhh nimechoka ngoja nikapumzishe kichwa..:roll:
 
Lakini kwa SPIKA kuzomea kama kweli alifanya hivyo alifanya kosa. Ni sawa na refa wa mechi ya mpira wa miguu kushangilia timu moja ikifungwa. Lazima kuwe na kasora hapo
Nina wasiwasi kama huyu mama atamaliza miaka yake mitano
 
Ndugu wana jamii wenzangu, jana wakati Chadema wanatoka Bungeni kupinga mabadiliko ya kanuni kuhusu tafsiri ya neno KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI wabunge wengine waliwazomea, kwa mimi nilisikia mwishoni wakati wabunge wanatoka Sauti ya Spika wa Bunge nae alizomea au kutoa neno la kejeli kwa Chadema, sikumbuki vizuri hapo, ila ilinishtua kusikia sauti ya Spika nae kwenye mkumbo wa kuzomea.

Mnalionaje hili wana Jamii wenzangu, naomba tulijadili na kama kuna mmoja wetu ana hiyo Clip naomba aiweke ili tuisikilize kwa makini, ila mimi nilisikia kuna sauti ya Spika pia akitoa kejeli kwa wabunge wa CHADEMA.

Naomba kutoa Hoja.
Spika ni mbunge wa sisiem , na yaliyokuwa yakizungumzwa pale ni kwa maslahi ya sisiem, kuona ushindi umepatikana alipandwa na mzuka pia akijua wazi kuwa atapongezwa na chama kwa kazi nzuri.
 
Nilisikia nikaishiwa nguvu sikutegemea wabunge wanaweza behave vile kwani hata watoto wa nursery wangekuwa na some ustaarabu...

Ndugu yangu hili Bunge limejaa usanii wa hali ya juu. Wanachojali wengi wa Wabunge wa CCM na CCM B wanaojiita nao wapinzani ni kuweka mbele maslahi yao na yale ya CCM badala ya Tanzania na Watanzania. Kwa hiyo usishangazwe na chochote kile kitakachofanyika ndani ya Bunge hili.

Tulivyo waambia kuwa wabunge wa CCM si makini hata mpirani kuna staha kidogo
je hili ni bunge au kilabu cha pombe na siku hizi hata vilabuni watu wanazungumzia vitu
vya msingi.Ubunge sio fadhila za watawala ni uwakilishi wa wananchi.
 
Kama mtu babaye na mamaye wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya na umasikini uliosababishwa na ufisadi,halafu yeye anashangilia mafisadi kupata nafasi ya kuua shangazi yake na mjomba wake pia ujue huyo hana tofauti na ling'ombe. Ndivyo ninavyoanza kuwaona baadhi ya waheshimiwa wetu pale mjengoni.
 
Nilimsikia sista du mmoja akisema "cheap politicians" wakati yeye mwenyewe kaingia mjengoni kwa viti maalum.
 
Walichotaka ccm ni kufanya tafsiri ya kambi rasmi ya upinzania ili waweze kudhoofisha upinzani bungeni kwa kuingiza vibaraka wao kuwa wenyeviti wa kamati za bunge hilo wamefanikiwa. so lazima tuwapongeze CDM kwa kulitambua mapema njama zao ingawa wengi hawakulijua hilo!
 
Lakini kwa SPIKA kuzomea kama kweli alifanya hivyo alifanya kosa. Ni sawa na refa wa mechi ya mpira wa miguu kushangilia timu moja ikifungwa. Lazima kuwe na kasora hapo
Kweli kabisa!hiki ni kichekesho cha mwaka 2011!!
 
Back
Top Bottom