Kuzimwa kwa Siasa uchwara Vyuo Vikuu, Wanafunzi wengi wapata nafasi za ajira Serikalini Awamu ya Rais Magufuli

Huliza

JF-Expert Member
May 5, 2017
392
982
Wanajukwaa, Miaka ile wakati baadhi ya watu tukishiriki kwenye elimu ya Tanzania ilikuwa ni migomo kabla hujaingia chuo,ukiingia mpaka siku unaondoka chuo. Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 habari za migomo vyuoni imebaki historia

Migomo inachelewesha wanafunzi kusoma na kuwa na mawazo mbadala. Taifa hili leo hii limeweza kuajiri maelfu ya vijana kutoka na umahiri na udhibiti mzuri wa JPM vyuoni tangu mwaka 2015

Huduma bora zimeimalika vyuoni kwa upande wa ada na pesa za kujikimu kuongezeka zaidi baada ya mfumuko wa bei kudhibitiwa,Wakati wa migomo watu walitumia pesa hovyo kutafuta sehemu za kuishi lakini sasa Wanafunzi wamejikita kwenye elimu

Ajira elfu nane za walimu wa msingi na sekondari ni uthibitisho kuwa sasa Wanafunzi wetu wanapikwa na kupikika na hawakushiriki migomo vyuoni,

Baada ya kugundua migomo haifai na haijengi Halima Mdee na wenzake wameamua kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo

Ukipita maeneo mbalimbali vijana wenye umri wa miaka 21 mpaka 27 wameajiriwa kwa maelfu tangu 2014 mpaka sasa katika kila sekta, Ushahidi ni walimu zaidi ya elfu nane walioajiriwa kwa mkupuo na hii haijawahi tokea kwa wakati mmoja kuajiri idadi kubwa namna hii

Kila mtu mtaani mwenye mtoto aliyepata nafasi hizi ni Furaha kubwa sana hata Raia wa kawaida wana furaha na raha isiyo ya kifani kutokana na maendeleo makubwa ya huduma yaliyofanyika chini ya Magufuli

Hasira na Povu linaruhusiwa lakini povu liwe la kiasi katika kuchangia uzi huu kwani povu ni sehemu ya kupunguza stress

Viva CCM Viva CCM,
 
Wanajukwaa, Miaka ile wakati baadhi ya watu tukishiriki kwenye elimu ya Tanzania ilikuwa ni migomo kabla hujaingia chuo,ukiingia mpaka siku unaondoka chuo. Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 habari za migomo vyuoni imebaki historia...
Viva vijana vivaaa.

Viva Magufuli vivaaa
 
Hata mjinga hujiona ana akil
Hata mjinga hajioni kuwa mjinga bali hujiona mwerevu. Anaweza akaponda kila jema linaloelezwa na wenzake kwa kujiona mwerevu bila kujua anachoeleza kupinga ni ujinga.

Kwa vile hajitambui kuwa ni mjinga anaendelea kuwa mjinga na amezungukwa na wajinga wenzie
 
Nimeandika nikafuta,nikaandika nikafuta,ninaandika ninafuta na nitaandika nitafuta maana chochote nitakachoandika kinauwezo kudhuru ubongo wako
 
Back
Top Bottom