kuzalisha tu bila kuoa

KIDHEHA

Member
May 21, 2012
51
14
asalam aleikuuum
mi ni kijana wa miaka 30...nina watoto wawili na wanawake tofauti...hivi nikiamua kulea watoto tu bila kuoa mwanamke mwingine jamii itanichukuliaje?
 
jipime 1.ulilelewaje? 2.Unatakaje? Halaf jibu utapata
 
kwani jamii ikikuchukulia negative au positive wewe unachubuka?

Usiishi maisha yako kwa kutazama macho ya watu ishi vile nafsi yako ipendavyo.....tunza wanao vileunavyoona inafaa
 
Kwani plan yako ya maisha umepanga iweje..unataka uzalishe tuuu bila kuoa au.... Kama ulitegemea kuoa mpaka sasa hijafika 30 una watoto wawili nje mama tofauti. je ukifika 45 sijui utakuwa na wangapi. Ila kwa ujumla maisha yako hayapangwi na jamii bali wewe mwenyewe kuangalia plan zako. ila jipange!!!!!
 
asalam aleikuuum
mi ni kijana wa miaka 30...nina watoto wawili na wanawake tofauti...hivi
nikiamua kulea watoto tu bila kuoa mwanamke mwingine jamii
itanichukuliaje?

Ulipowapata hao watoto wawili bila ndoa kwa wanawake wawili tofauti jamii ilikuchukuliaje?
 
Mbona wengine wakibebesha mimba wanasepa na bado wanafit katika jamii? Si bora wewe uliyeamua kulea watoto wako?
 
asalam aleikuuum
mi ni kijana wa miaka 30...nina watoto wawili na wanawake tofauti...hivi nikiamua kulea watoto tu bila kuoa mwanamke mwingine jamii itanichukuliaje?

Wewe ni mwanachama katika jamii. Si unaendelea nalo hilo na hakuna aliesema?
 
Watu tunajitahidi sana kuupinga ukweli. Hivi kuna mtu asiyejali jamii inamchkuliaje???

Tukirudi kwenye mada; mimi nimekuelewa ni kwa nini unaona ngumu kuoa; kwani kuwa na watoto wawili toka kwa mama tofauti si mchezo. Wasiwasi wangu unaweza pata wa tatu na wa nne kwani inaelekea unatembea na wanawake wanaopenda kuzaa na wewe. Na wewe kama mwanaume itakuwa ngumu kuepuka mtoto wa tatu na kuendelea. Na sijuhi utawaleaje hao watoto wawili maana ukisema uoe shida, mama wa kambo; ukisema usioe utazaa wengine nje ya ndoa. Mtihani kwa kweli.
 
Kwanza una hakika gani kuwa hao watoto ni wako? Pamoja na kuwa hata wazazi wawili wanaweza kufa kwa pamoja, lkn ikikutokea ume-rip wakiwa wadogo bado unawarithisha nani, hao watoto wakiwa wakubwa na waanze kuzaa kama panya na kuleta watoto home utajisifia? Hii misemo kuwa ishi unavyoona inakufaa bila kujali jamii ndiyo inayowapa haki wasagaji, mashoga na wengine wa aina yao. Shetwani @ work.
 
asalam aleikuuum
mi ni kijana wa miaka 30...nina watoto wawili na wanawake tofauti...hivi nikiamua kulea watoto tu bila kuoa mwanamke mwingine jamii itanichukuliaje?

Ishi uwezavyo usiishi watakavyo. Ila kumbuka kuna KUFA.
 
Kuoa au kutokuoa ni hiari yako; lakini kulea watoto uliowazaa mwenyewe ni wajibu wako kama mzazi. Si hiari.
 
Kuhusu hilo maamuzi hasa yako kwako mwenyewe, lakini umewapa wakati mgumu sana hao watoto watatu ambao wanakosa ukaribu wa mama zao.
 
Back
Top Bottom