Kuzaa Kwa Upasuaji V/S Kuzaa Kwa Njia Asilia

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF Wasalaam Aleykhum!

Kuna habari miongoni wa Wanawake hasa wenye uwezo wa Kiuchumi kwamba wao hawapendi kuzaa kwa njia ya asili ili kuepuka maumvivu na uchungu wa uzazi. Pia wakizaa kwa njia ya upasuaji, wanadai kuwa maumbo yao yanaendelea kuwa "Bomba".

Lakini wengine wanapingana na hilo na kuwa kuzaa kwa "Mkasi" kunamfanya mama asijue thamani ya mtoto kupitia uchungu wa mwana na hivyo kumwondolea upendo. Kwa mtazamo wao uzazi wa namna hiyo "Mkasi" uwe ni kwa wale tu walio katika hatari kuwa wakizaa kwa njia ya kawaida wanaweza kupoteza maisha.

Wadau, hii chaguo mbili zimekaaje?
 
- Hawa ni wavivu tu wa kusukuma.

- Pia kunakosekana strong bond kati ya mama na mwana . . ule msemo wa "Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi" unakosa maana.

- Sijui dini zetu zinasema nini. Inawezekana ikawa ni kinyume cha maagizo ya Mungu kuwa "Utazaa kwa Uchungu"?
 
kuzaa kwa njia ya kawaida ni bora zaidi kwa mama mtoto kwani mwili unakuwa unafanya changes flani baada kujifungua kwa njia hii kama kuandaa maziwa mwilini kwa ajili ya mtoto.wanawake wengi wanajifungua kwa mkasi huwa saaa nyingine utoa maziwa kidogo sana kwa ajili ya mtoto mpaka hapo baadae kidogo mwili uzoee.na kuzaa kwa mkasi nadhani ina limit ya watoto wakati ya kawaida unaweza kuzaa wengi tu.madaktari wengi ushauri kuzaa kwa njia ya kawaida labda pale tu mtoto anapokuwa katika hatari flani ndio wanashauri kutumia njia ya mkasi.
 
Du, hii ya uvivu wa kusukuma ni kali. Inawezekana kwa uhakika hii ikawa ni sababu?

Sina uhakika kisayansi kama kuna uhiusiano wowote kati ya kuzaa kwa njia ya asili na bond. Wanaojua watusaidie.

Hili la dini liko wazi, lakini je kwa walio na matatizo ya kuzaa kwa njia ya kawaida, nao wako restricted na vitabu vitakatifu?
 
Mimi kwa mawazo yangu ni kwamba M/Mungu huwa ana makusudi yake kwa kila alichokipanga na kukiweka kwa wanadamu. Sijazaa bado ila nimekuwa nikisikia tu kwamba uchungu unauma. Ila kwa kudra zake M/Mungu baada ya zoezi la kujifungua kumalizika, maumivu yanaisha na mtu anasahau. Na ndio maana most of wamama baada ya miaka michache ana beba mimba nyingine.

Swala la kwamba kuzaa kwa kawaida kunaharibu mwili sidhani kama lina ukweli. Mwili utaharibika kwa uvivu wa mtu mwenyewe na kujibwetesha. Wadada wangapi wana watoto hata 4 na mtu unaweza ukaambiwa ukabisha jinsi walivyo na miili mizuri. Na wangapi wamejifungua kwa scissor na miili yao ipo tipwa tipwa. Offcourse kwa mwanamke anaependa afya nzuri ya mwanae kipindi cha kunyonyesha inabidi ale sana ili amnyonyeshe mtoto ipasavyo hence lazima atagain (kwa wengi) then baadae ndio mambo ya kurudi kwenye mwili mzuri (kama mtu hakuwa mnene) ndio yataendelea.

I believe mtu akizaa kwa njia ya kawaida akafeel uchungu atakuwa na mapenzi zaidi kwa mwanae... Na pia ni njia natural ukilinganisha na mkasi. Yeah, ni technology but nahisi ingekuwa kwa special cases sio kwa luxury. Madaktari wao si wanataka pesa so atakupasua tu lakini nahisi yaweza kuwa na baadhi ya madhara. Sijui....

Mawazo tu lakini....
 
Kitaalamu mkasi huwa unatumika tu endapo wakati wa kujifungua ikaonekana mama hawezi tumia njia ya asili au kuna uwezekano wa kupoteza maisha yake na ya mtoto au mmoja kati yao, utumiaji wa mkasi kwa sababu za kukeep figure na mambo mengine ya kiurembo ni matakwa ya watu binafsi.
 
If u knoe something called CP (Cerebral palsy) you would never allow ur wife to deliver per vaginally. Data zinaonyesha kuwa ongezeko la watoto taahira linasababishwa kwa kiasi kikubwa na birth asphyxia. C/S is the best in terms of outcome! Take it or leave it, that is the reality!
 
kuzaa kwa njia ya kawaida ni bora zaidi kwa mama mtoto kwani mwili unakuwa unafanya changes flani baada kujifungua kwa njia hii kama kuandaa maziwa mwilini kwa ajili ya mtoto.wanawake wengi wanajifungua kwa mkasi huwa saaa nyingine utoa maziwa kidogo sana kwa ajili ya mtoto mpaka hapo baadae kidogo mwili uzoee.na kuzaa kwa mkasi nadhani ina limit ya watoto wakati ya kawaida unaweza kuzaa wengi tu.madaktari wengi ushauri kuzaa kwa njia ya kawaida labda pale tu mtoto anapokuwa katika hatari flani ndio wanashauri kutumia njia ya mkasi.

Mkuu;

Kuna dada ana watoto wanne na wote amewazaa kwa kisu. Hii nayo imekaaje kama kuna limit?

Kuhusu kutoa Maziwa mengi au kidogo. Kuna maelezo yoyote ya Kisayansi ya tofauti hiyo?
 
Unaweza kuzaa hata marakumi kwa kisu, issue ni kwamba kila unapofanya oppearation ndo unavyoongeza risks na complication km kupasuka mfuko wa uzazi (uterine rupture),kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua ( APH na PPH), shinikizo la damu (PIH) na mengine mengi.
Kwa msingi huo, wataalamu wanashauri upasuaji usizidi mara tatu.
Wanawake wengi wanaojifungua kwa upasuaji hupata tatizo la uhaba wa maziwa kwa sababu zifuatazo:
Kitendo cha upasuaji uliopangwa ( Elective C/S) hufanyika kabla mama yajatoa oxytocine homone ya kutosha, hiyo homone ni muhimu sana kwa uanzishaji wa uzalishaji wa maziwa.
Sababu nyingine ni pale ambapo hawa kinamama wanapofanyiwa upasuaji inabidi wakae karibu masaa 24 bila kula, ukilinganisha na mama aliyesukuma ambaye anaanza kula imediately baada ya kujifungua.
 
- Hawa ni wavivu tu wa kusukuma.

- Pia kunakosekana strong bond kati ya mama na mwana . . ule msemo wa "Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi" unakosa maana.

- Sijui dini zetu zinasema nini. Inawezekana ikawa ni kinyume cha maagizo ya Mungu kuwa "Utazaa kwa Uchungu"?

Kuhusu bond hii nakupinga kwa sababu kuna akina mama wamezaa kwa njia ya kawaida na wanatreat watoto wao kama vinyago!!!

Kuhusu la maagizo ya mungu, sina hakika... ila je wanaozaa kwa operesheni huwa hawapati uchungu?
 
If u knoe something called CP (Cerebral palsy) you would never allow ur wife to deliver per vaginally. Data zinaonyesha kuwa ongezeko la watoto taahira linasababishwa kwa kiasi kikubwa na birth asphyxia. C/S is the best in terms of outcome! Take it or leave it, that is the reality!

Thanks Obhusegwe,

Its good to deliver naturally, lakini with all teh current developments and lifestyle challengs... nakwambia fanya unachodhani kitawasaidia wewe na mkeo;
wale wenye kuzaa wachache au with any potential risks during labor and delivery, wanaweza ku-opt ili kumuokoa mama na mtoto

  • Nimeona baadhi ya watoto wakipotea au hata baadhi ya akina mama wakipotea
  • Pia nimeona akina mama kuharinika kabisa viungo vya uzazi kwa sababu mbalimbali during uzazi
  • Baadhi ya watoto azaliwao na wamama wenye maumbo madogo hupata deformities nyingi, za ndani [kama palsy] au hata kwa nje kama vichwa kupinda, mikono kuwa na defects [vikono] au kunywa maji ya mama hivyo kuharibu mapafu nk.]

Kama mungu alitupa innovative minds za kupunguza shida, basi mie nikipata chance ya kuepuka risk kwa mke wangu au mtoto, ntachoose the easier way!! I have done it and i dont regret,
 
Nadhani hapa ndipo kwenye matatizo makubwa katika matumizi ya sayansi, kwa kweli sasa sayansi inatumika hata katika vitu ambavyo viko natural
kiukweli mwili wa binadamu ni computer iliyotimia kabisa, mwanamke aanapokuwa na mimba mwili wote unajua kwamba kuna kitu kigeni ndani ya mwili na hivyo unajiamdaa kwa njia mbalimbali ili kkwenda sambamba na mabadiliko hayo, sasa wakati wa kujifungua ukifika kunakuwa na mawasiliano kati ya ubongo na viungo vya uzazi kwamba kile kitu ambacho kiliingia muda wake wa kukaa ndani umekwisha hivyo ni lazima kitoke, sasa nadhani hapa tatizo linakuja pale viungo vya uzazi vinaposhindwa kufanya kazi yake pale mtoto anapotolewa kwa njia ya operesheni, hivyo viungo vina adapt ile tabia, na uwezekano wa kuzaa tena kwa operation ni mkubwa sana
ni kama kama mwanamke anayetoa mimba, kama alitoa mwezi wa nne wa mimba, basi mwili unajua kwamba kila mimba ikiingia after 4 months lazima itoke, bas kunakuwa na matatizo makubwa ya misscarriage hapo
MWILI NI COMPYUTA ACHA UFANYE KAZI YAKE NATURALLY
 
Wana JF Wasalaam Aleykhum!

Kuna habari miongoni wa Wanawake hasa wenye uwezo wa Kiuchumi kwamba wao hawapendi kuzaa kwa njia ya asili ili kuepuka maumvivu na uchungu wa uzazi. Pia wakizaa kwa njia ya upasuaji, wanadai kuwa maumbo yao yanaendelea kuwa "Bomba".

Hamna lolote, wameshaathiriwa na mchezo mchafu wa kufanya mapenzi kinyume na maumbile hivyo wanaona wakizaa kwa njia ya kawaida wataumbuka.
 
Hivi mwanamke akizaa kwa operation mzao wa kwanza, ni lazima azae kwa operation watoto watakaofuata?
 
du, kupasuliwa kitu cha kuogopa kumbe kuna watu wengine wanapenda, kweli dunia hadaa
 
Nadhani hapa ndipo kwenye matatizo makubwa katika matumizi ya sayansi, kwa kweli sasa sayansi inatumika hata katika vitu ambavyo viko natural
kiukweli mwili wa binadamu ni computer iliyotimia kabisa, mwanamke aanapokuwa na mimba mwili wote unajua kwamba kuna kitu kigeni ndani ya mwili na hivyo unajiamdaa kwa njia mbalimbali ili kkwenda sambamba na mabadiliko hayo, sasa wakati wa kujifungua ukifika kunakuwa na mawasiliano kati ya ubongo na viungo vya uzazi kwamba kile kitu ambacho kiliingia muda wake wa kukaa ndani umekwisha hivyo ni lazima kitoke, sasa nadhani hapa tatizo linakuja pale viungo vya uzazi vinaposhindwa kufanya kazi yake pale mtoto anapotolewa kwa njia ya operesheni, hivyo viungo vina adapt ile tabia, na uwezekano wa kuzaa tena kwa operation ni mkubwa sana
ni kama kama mwanamke anayetoa mimba, kama alitoa mwezi wa nne wa mimba, basi mwili unajua kwamba kila mimba ikiingia after 4 months lazima itoke, bas kunakuwa na matatizo makubwa ya misscarriage hapo
MWILI NI COMPYUTA ACHA UFANYE KAZI YAKE NATURALLY

Thanks mkuu, nimejifunza mengi toka kwako.... computer inaenda hedhi, inapata flu, inatunga mimba, inakata magogo nk.

from now on, i will follow your advice
 
'Madaktari' wa JF kiboko. Ngoja nihamie kwenye mada nyingine maana hapa naona makundi makubwa 2 yenye nguvu sawa, wamchao Mungu na waichayo sayansi
 
Thanks mkuu, nimejifunza mengi toka kwako.... computer inaenda hedhi, inapata flu, inatunga mimba, inakata magogo nk.

from now on, i will follow your advice
Pia inapata virusi na minyoo na wakati mwingine inaaboti
 
Kuhusu bond hii nakupinga kwa sababu kuna akina mama wamezaa kwa njia ya kawaida na wanatreat watoto wao kama vinyago!!!

Kuhusu la maagizo ya mungu, sina hakika... ila je wanaozaa kwa operesheni huwa hawapati uchungu?

Ahsante sana MTM, kuzaa kwa mkasi pia kuna uchungu mkubwa tu na pia hili la kusema wanaojifungua kwa C-Section hawana bond na watoto wao halina ukweli wowote.
 
Hivi mwanamke akizaa kwa operation mzao wa kwanza, ni lazima azae kwa operation watoto watakaofuata?

Hapana Nemesis siyo kila mwanamke aliyejifungua ujauzito wake wa kwanza kwa C-Section ataendelea kujifungua kwa njia hiyo. Inategemea sana operation ya kwanza ilikuwa ni kubwa kiasi gani, pia inategemea ujauzito uliofuata kama una complications au la na pia inategemea recomendations za daktari.

Kuna akina Mama ambao mimi nawafahamu ujauzito wao wa kwanza wote walijifungua kwa C-Section na wote walishauriwa na madaktari wao katika mimba zao za pili wafanyiwe tena C-section wote walikataa mmoja alijifungua salama salmini na mwingine uterus ilipasuka na alikaribia kupoteza maisha.
 
Back
Top Bottom