Pole sana ndugu, naheshimu sana mawazo yako,.lakini pia sijaona sababu ya kutokwa na maneno makali sana, how you respond tells alot about you
Turudi kwenye mada, nadhani inategemea kila mtu anatumiaje mtandao na aina ya magroup anayojiunga, binafai siwezi kujiunga kwenye groups ambazo sielewi nia na dhumuni la group au siwezi kukuta tu group linatangazwa mtandaoni basi nikajiunga, hayo mambo wanafanya wanawake wahuni
Pili, groups ni nzuri kama utazitumia kwa nia njema, kwa mfano kuna groups za wazazi ambazo zinaanzishwa na walimu wa madarasa kwa ajili ya kupeana taatifa za shule za watoto
Kuna groups za jumuiya kwa ajili kupeana taarifa mbalimbali za kanisani
Kuna groups za alumni, ambazo zinawakutanisha collage mates au school mates, kuna groups za familia nk
Ila kumeibuka wimbi mtu anatangaza tu group instagram au faceboo na watu wanajiunga, usitegemee mambo mazuri kwenye hizo groups, character yako ndio inayopelekea wewe kujiunga aina fulani ta group