Kuweni makini na vifurushi vya Airtel

Kuweni makini na vifurushi vya Airtel

kingine kwa siku unruhusiwa kutuma sms 300 tu hata kama una sms za kutosha , zikishafika 300 unasubiria kesho

Aiseeh!! Dunia pana SMS 300 unakuwa unachati na baby au za kazi.

..........Nimetumia line za aitel, tigo,vodacom na halotel ila Airtel ni bora kuliko zote ukiunga bando na salio likabaki hawakati salio lako na bando likiwa linaenda kuisha lazima wakutumie sms kukushtua kabla hawajaanza kula salio, Shughuli ipo na hao wengine ukibakisha salio baada kuunga bando wanaanza kwanza na salio ndio wake na bando.
 
Wenye mitandao wajanja sana. Mfano wana watu 200, 70 wanawafanyia uhuni wa kuwaibia salio na wengine hawaibiwi. Sasa kinachofanyika hapo, hawa 70 wakianza kulalamika, hawa 130 wanaanza kuwajibu hawa 70 kuwa siyo kweli mbona wao hawafanyiwi huo uhuni. Inaonekana hawa 70 wanamatumizi mabaya ya vifurushi. Nilishawahi kuunganishwa na vifurushi vya hadithi kwenye tigo ambacho sijawahi kujiunga, nilishawahi kununua salio mpesa kwenda tigo salio hata halikufika na juzi kati niliweka vocha 1000 Haloteli wakapita kama na 310 hivi. Kuwauliza nilichoka na majibu. Sasa hivi salio naweka Halopesa tu. Hawa kwenye mitandao wanapiga hela sana za wizi.
Kwangu mi airtel haina hayo manjanginjangi. Mb 500 tu unaweza cheza na youtube mbaka simu ikachemka
 
Wacha nkendelee kutamba na ttcl japo wao ktk kifurushi cha bandika bandua huwez jiunga mara mbili kwa pamoja...
 
Halotel siku hizi mwenyew siwaelewi.. Nawahesabia siku tu nirudi ttcl
 
Aiseeh!! Dunia pana SMS 300 unakuwa unachati na baby au za kazi.

..........Nimetumia line za aitel, tigo,vodacom na halotel ila Airtel ni bora kuliko zote ukiunga bando na salio likabaki hawakati salio lako na bando likiwa linaenda kuisha lazima wakutumie sms kukushtua kabla hawajaanza kula salio, Shughuli ipo na hao wengine ukibakisha salio baada kuunga bando wanaanza kwanza na salio ndio wake na bando.

kitu nachowapendea airtel, mfano ukiunga bundle ya siku alafu kabla ijaisha ukaongeza, zinajumlishwa, hata mda ukipita unakuta umeweka bundle za siku mara 3 ndan ya wiki zote znakua combined: ingawa bado wana mapungufu kama slow internet na coverage lakini wanapiga hatua
 
Airtel kwa bundle za internet wanajitahidi sana. Ukiona wanakwambia limeisha angalia salio unakuta lipo sawa. Ulichosema ndugu ni sawa kabisa
GB1 ni siku tatu sio wiki na ni elfu moja.
Niliweka bundle la 1GB siku tatu saa tano usiku dakika 3.Kufika saa 6 usiku napata message bundle lako la siku 3 limekwisha.Nikachanganyikiwa.
Nikaamua kuuliza salio kupitia *149*81# then salio nikaona salio liko sawa.
Nikapata reason kuwa ni autoreply message saa sita usiku simu ina assume ni siku mpya.
Nawashauri airtel rekebisheni hili based on 24hrs×3=72hrs ndio ije msg bundle limeisha.
Otherwise airtel is best msiwapake matope.
Nilitaka kufungua uzi kwa hili lakini kupitia hapa nimeona nitoe ushahidi wangu
 
Cjafahamu line zenu zina shida gani ila airtel yangu inafanya kazi vizuri sana kila aspect mda wa kuongea na internet vinafanya kazi vizuri sana ni network coverage sio nzuri ila all things wako fire
 
Habarini za jioni,

Asubuhi ya kuamkia jana nilipata mshtuko kidogo. Jana yake jioni niliweka bundle la wiki la GB 1 nikachat na JF na WhatsApp kidogo, usiku nikajibishana kidogo na wifi yenu nikalala.

Na nimezima data, nawasha simu asubuhi nijibu message naambiwa bundle lako la GB1 la siku limeisha. Aisee nikawapigia wakasema ni kweli inaonyesha bundle limeisha GB1, nauliza mbona nimechukua cha wiki na sija-download ama kufanya kazi ya kutumia data? Na je, mbona naambiwa bundle lako la siku limeisha na sijajisili la siku?

Dah Japh boy akanijibu kaka naomba watakupigia kujua shida iko wapi ndani ya masaa 24.

Ghafla nikatumiwa tiketi nitapigiwa simu, hivi sasa inaelekea masaa 48 aisee!

Leo nikamua kujiunga tena nikawapigia inasoma GB ngapi, wakataja nikasema jana mmenifanyia uhuni ngoja tumoniter na hizi kama zitaondoka.

Nawatakia wote matumizi mema wanaotumia Airtel.

Nilishawahi walalamikia huko nyuma naona imeisha hii tabia.

Ukiwa una 2100 unajiunga kifurushi, inagoma na ni kifurushi cha 2000. Ukiwapigia wanakwambia hawaelewi tatizo, embu ongeza za 500.

Kweli nikiongeza kinakubali cha 2000 na salio linabaki, sijui why. Tigo kama una 2000 unaweza jiunga cha 2000 kama una 10000 unaweza jiunga haitaji addition yoyote.

Kituo kinachofuata Serikali za Mitaa.

Tukutane 2 Nov.
Mimi Nina mawili

1.nilikua na salio la vocha 15000 nikapata tatizo nikipiga 100 huduma kwa wateja kma mnavojua ni bure lakn nimemaliza kubonga nao Salio LA. Vocha ni 0

2.nilishawahi kosea kutuma ela kwa mtu nikapiga huduma kwa wateja wakasema imezuiliwa baada ya 24 saa itakua isharud,kufika mda naona kimy napiga kuuliza naambiwa ela ishatolewa yaan Airtel mtandao Bomu kbs
 
NIMESEMA.AWA JAMA.N.MATAPELI
NIMEJIUNGA..ANA LEO.NKAINGIA KANSANKWA.MWAMPOSA.NKAZIMA DATA NAWASHA USIKU HUU NAAMBIWANIMETUMIA.ASILIMIA.90% YÀ GB 1
Screenshot_20191117-235248.png
Screenshot_20191117-235254.png
Screenshot_20191117-235301.png
AISEE ..ANAWAONA NAFIKIRI.MDA.MUFAKA.KUHAMA.KABISA HUU MTANDAOOO
 
Airtel kwa bundle za internet wanajitahidi sana. Ukiona wanakwambia limeisha angalia salio unakuta lipo sawa. Ulichosema ndugu ni sawa kabisa
SIO KWELI KUNA GB 1 SIKU SABA MUACHE USHAMBA KUWAZA N SIKU TATU NIMEMWONYESHA ATYCHMENT AONE KAMA HUJUI NIKUELEKEZE PENGINE NDIPO WANAPOPIGA WANANCHI WANASEMA SIKU SABA WANATUMA MSG GB ZIMEISHA SIKUTATU AMKENI
 
Back
Top Bottom