Kuweni Makini na Tigo

Kuweni Makini na Tigo

Miss k

Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
11
Reaction score
1
Mimi ni mjasilia mali nafanya biashara ya kuweka na kutoa pesa I.e Tigo pesa,M-pesa,airtel money
Leo amekuja mtu ametaka toa pesa 3k nimemtolea baada ya sms kuingia kwenye simu yangu na salio kuongezeka lakini baadae nikagundua nimepigwa !!!nikawapigia tigo kuwaeleza kwamba sms imeingia kutoka tigo pesa wakasema hii haikutoka kwao baada ya kuichunguza sms nikaona center # inaanzia +46707990020
Chakushangaza namba yangu aliijuaje? Hadi sms kunifikia?
Naomba wezangu muwe makini lakini bado sina imani na baadhi ya wafanyakazi wa tigo kwa namna moja lazima watakuwa wanausika ,hamna anayeweza kujua salio lililopo kwenye simu!!!!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mimi binafsi siwaamini hata kidogo hawa wafanyakazi wa mitandao kutokana maelezo yako hapo juu Miss K inaonekana kuna mtandao ndani ya wafanyakazi wa tiGo sio waaminifu!!
Nenda Polisi katoe taarifa then uende tiGo ofcn kucheck nao watakusaidiaje
Pole sana
 
Hao jamaa ndio kazi yao wakiona unatoa na kuweka pesa nyingi wanakuibia fasta, na ukienda makao makuu hakuna wanachokuambia zaidi ya kwenda polisi wakati hiyo michezo wanaicheza wenyewe! Nina kesi mbili za wazi kabisa ambapo namba ya simu iliyosajiliwa ilikuwa swapped na nilipouliza wakasema hawajui chochote, nani mwenye mamlaka ya KUSWAP line za simu?! Mi sitaki kusikia hiyo habari ya TIGO Pesa......
 
Kweli hawa Tigo wamekua ni wezi sana mara mbili nimekua nikipoteza pesa zangu, unakuta password yangu inagoma kabisa ukifuatilia utapewa kalenda week 3 wanakuzingua tu mara jaribu baada ya masaa 8, mara baada ya masaa 24.. mpaka unaamua kuacha na pesa unakuta inapotea tu..wanavyofanya sio uungwana kabisa
 
Siku hizi wafanyakazi wa bank hasa NMB na hawa wa Tigo - Pesa ni wezi sana na kwa sababu hiyo ndiyo maana M - Pesa itawaacha mbali sana.
 
kuna siku nilisikia kesi moja ya mfanyakazi wa benki.alikuwa anachukua sh.2000 kwa kila account ndani ya mwezi mmoja kwa kila mteja nikaona hii sasa hii balaa.wanasema tusiifadhi pesa majumbani lakini ukiweka benki wanaume wanakula kiulaini
 
Mimi ni mjasilia mali
nafanya biashara ya kuweka na kutoa pesa I.e Tigo pesa,M-pesa,airtel
money
Leo amekuja mtu ametaka toa pesa 3k nimemtolea baada ya sms kuingia
kwenye simu yangu na salio kuongezeka lakini baadae nikagundua nimepigwa
!!!nikawapigia tigo kuwaeleza kwamba sms imeingia kutoka tigo pesa
wakasema hii haikutoka kwao baada ya kuichunguza sms nikaona center #
inaanzia +46707990020
Chakushangaza namba yangu aliijuaje? Hadi sms kunifikia?
Naomba wezangu muwe makini lakini bado sina imani na baadhi ya
wafanyakazi wa tigo kwa namna moja lazima watakuwa wanausika ,hamna
anayeweza kujua salio lililopo kwenye simu!!!!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Hii imemkuta jamaa yangu, ila yeye ni kwa Mpesa, jamaa kaibiwa laki 8, mawakala wa hizi huduma muwe makini manake hawa jamaa ni nooma
 
Kweli tukimbilie wapi? Ila inakuwaje mtu aingie accoung ya mpesa, tigo au aritel money aibe hela wakati hajui password yangu? So sad!! Ila ni lazima kuna ushirikiano wa watumishi kama ilivyo katika ATM za mabenki.
 
Hivi Tanzania tuna sheria za kusimamia hizi mobile banking and internet banking?
 
Hizo ndizo baadhi ya faida na hasara za mobile banking technology. Ni rahisi kutuma na kupokea pesa, lakini pia ni rahisi kulizwa.
 
Kila kona wezi...sijuinchi itakuwaje baada ya miaka 5 ijayo
 
Tanzania sasa si mahali salama pa kuishi binadamu! Maana tunasikia wizi kwenye ATM, mara wizi wa mizigo uwanja wa ndege, mara uuaji wa tembo, mara wanyama hai wanasafirishwa, hatujatulia mabilioni yatafunwa TANESCO, mara oooh mabilioni ya uswisi, sasa na makampuni ya simu na yenyewe yameingia kwenye wizi huu? Mmmh, hata kama Mkapa alitoka na kashifa ya EPA, na hisi Kikwete hali yake ni mbaya kushinda ile ya Mkapa. Kama wakati wa Mkapa ziliibiwa bilioni 150, this time hadi anaondoka Kikwete madarakani tutakuwa tumepoteza matrioni.

Hivi ina maana security system ya Tanzania ipoje? Kama watu wanachora dili mbaya za kuiba kiasi hiki, hadi kuna watu wanatengeneza ATM card na kuiba fedha benk watu wanaohusika na usalama wa nchi hawana habari, hivi haiwezekani watu kuunda kikosi cha uasi kwa lengo la kushambulia msafara wa Rais? Au hata kupindua nchi? Ukishaona kuna loopholes za mambo ya kijangiri mengi kufanyika nchini, basi ni dhahiri kwamba nchi haipo salama. Ni vema wenye mamlaka watambue huu ukweli kwamba hata wao hawapo salama kama hali ya nchi ipo hivi.
 
Tongs bana! Mbona hiyo maana uliyoidhania iko mbali sana na biashara ya kuweka na kutoa pesa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom