Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,767
- 29,721
Wadau,
Jana Kijana wa jirani yangu kwenye Kibanda cha M-pesa ametapeliwa kwa style ambayo ningependa muifahamu na muwatahadharishe na wengine.
Alikuja mteja akiwa na Tshs 10,000/= na alitaka kumtumie mtu alieko mbali na hapo kibandani. Mhudumu akamjibu kua akitaka yule anaetumiwa apokee Tshs 10,000/= basi ato na ziada ya Tshs 1,000/= yaani jumla Tshs 11,000/=. Yule mteja (Tapeli) akampa mhudumu hiyo Tshs 11,000/= na kumtajia namba ya kutuma hela.
Utapeli ulianza pale kila Mhudumu anapoweka ile namba aliotajiwa kwenye simu yake na kutaja jina, yule Mteja (tapeli) anasema hilo Jina lililotokea silo lenyewe hivyo Mhudumu ameweka wrong number. Walirudia kama mara nne hivi kila jina linalotokea baada ya kutajiwa namba yule mteja/tapeli anasema silo lenyewe.
Mwishowe Mteja/tapeli akamwambia mhudumu ni heri aiweke mwenyewe hiyo namba kwenye simu, mhudumu akampa simu mteja/tapeli (kosa). Alichofanya yule tapeli ni ni
1) Kuangalia kwenye inbox SMS ya mwisho ya salio lililopo (lilikua 890,000) kwenye simu
2) Kujisevu namba yake yeye tapeli kama TIGOPESA na
3) Kubonyeza namba anakotaka hela iende.
Baada ya kubonyeza namba akamrudishia mhudumu simu aendelee kisha nae akaondoka. Baada ya nusu saa Ikaingia meseji kwenye simu ya Wakala kutoka TIGOPESA "feki" kua kuna hela imewekwa kimakosa kiasi cha 800,000/= hivyo balance ni Tshs 1,690,000/= kisha ikafuatia na kupigiwa simu kua Kuna hela imeingia kimakosa hivyo aitume kwenye namba aliotajiwa. Mpigaji alijitambulisha kua ni Mfanyakazi wa Tigo na alimtaka asichelewe.
Wakala alikuja kushtuka kua ametapeliwa baada ya kuona kua alivyotuma ile Tshs 800,000/= inayodaiwa kutumwa kimakosa, balance haikua 890,000/= yake iliyokuwepo kabla, bali ilibaki tshs 90,000/= tu. Kupiga Tigo ili wazuie hela isitolewe ikawa too late, pengine tapeli alikua kwenye kibanda kingine cha tigopesa standby anaisubiria iingie tu aitoe.
Nime-share nanyi ili muwasaidie wengine, waweza kumtumia mtu ambae unajua anamiliki Kibanda cha tigopesa ampe mfanyakazi wake, Ni hayo tu wadau