Kuweni makini na mafataki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuweni makini na mafataki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, May 4, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  “ mama husna mbona unatoa mimba ?” ahh hii mimba sio ya mume wangu

  Hiyo ni kauli kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa kampuni moja ya mambo ya mawasiliano , hapo rafiki wa mama husna alikuwa akimuuliza kwanini anatoa mimba mara kwa mara – huyo rafiki toka amejuana na mama husna inasemekana ametoa mimba zaidi ya 3 .

  Mama husna ameolewa mumewe aliachishwa kazi hana kazi maalumu anamtegemea mama husna kwa kila kitu , yeye mama husna ni mtoa huduma kwa wateja katika kampuni moja ya mambo ya mawasiliano – kinachoendelea ndani ya kampuni hiyo kati ya wafanyakazi wenye vyeo na hawa wachini wenyewe wanakijua .

  ……………………………………………………………………….

  Ni saa 4 za usiku , kijana yuko na mkewe ndani wanataka kupumzika ghafla anapigiwa simu na mmoja wa mabosi wake wa kazini anaambiwa anatakiwa kurudi kazini “ gari la kazini litakuja kukufuata hapo kituoni au nyumbani dada ngu “

  Mumewe hajui afanyaje mkewe kaitwa kazini wakati alitoka kazini saa 12 jioni tu muda ule ulikuwa ni wake sasa wa kupumzika , kijana wa watu hakuwa na la kufanya mkewe anatakiwa kwenda kazini amepigiwa na bosi

  Yule kijana kaamua kumsindikiza mkewe mpaka kituo cha gari , kufika huko ni kweli gari ya kazini ikaja lakini sio kibasi anachokijua yeye bali ni gari binafsi la mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ile ndio lilifika kumchukuwa yule dada .

  Kijana wa watu akarudi zake nyumbani – mkewe kumbe alikuja kuchukuliwa na bosi wake kwenda kula starehe kwa kisingizio cha kuitwa kazini na aina hii ya kazi imeashiri vijana wengi sana haswa dada zetu wanaofanya kazi katika kampuni hizi .

  ………………………………………………………………………….

  Katika chumba cha mawasiliano mmoja wa wasimamizi wa idara hiyo anatambulika kwa jina la FATAKI yuko amekaa pale kazi yake ni kusimamia wafanyajazi wote wanaotoa huduma kwa wateja wale wageni wanaojiunga mwanzo bila kujua ndio huwa halali yake kabla ya kuanza kuzoea maisha ya chumba hicho cha huduma .

  Siku ya kazi imefika mmoja wa wadada amechelewa kuingia kazini mlangoni amekutana na fataki , anaitwa pembeni kuchombezwa kwa sababu amechelewa kuingia kazini akakubaliana na fataki muda wa kazi ukiisha basi wakutane waende wote nyumbani .

  Mdada wa watu akakubali kukutana na yule baba baada ya muda wa kazi akaondoka nae kuanzia siku hiyo wakawa wapenzi na mapenzi moto moto – fataki ameacha mke na watoto nyumbani huyu dada ndio kamaliza form 6 tu na amepeta majibu mazuri katika matokeo yake lakini amekuja kukutana na fataki

  Sasa fataki akikaa tu kazi kuchungulia katika mitambo kuona sms zinazotumwa na kupokewa toka katika simu ya yule dada pamoja na kusikiliza mazungumzo mengine binafsi ya yule dada , fataki alimshika pabaya dada yule

  Fataki akishamaliza hamu zake huwa anaanzisha tena ishu zingine ili dada akasirike au wavurugane dada aache kazi au aachishwe kisha atafute msichana mwingine au wengine halafu aendeleze mchezo ule ule

  Kwa mtindo huo Fataki ameadhiri watu wengi sana wenye ndoa na wasio na ndoa ila wale tu wanaotaka maisha rahisi na vitu vya haraka haraka

  WAKINA DADA KUWENI MAKINI
   
 2. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Shy,

  Je, hakuna mafataki wa kike hapo? Mimi nawatafuta wa aina hiyo, maana wana vichenge!
  Kama yupo unayemjua tafadhari ni - PM.
   
Loading...