ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,556
Nimemsikia Waziri mkuu akiongea majuzi hapa kuwa walisha amua toka bungeni kuwa gari zilizotengenezwa nyuma ya mwaka 2010 zisiingie nchini.
Tungeomba bunge letu na serikali kupitia tena kulitazama jambo hili ki undani vinginevyo sie wanyonge hatutokuja agiza gari toka nje hadi dunia hii inaisha nchi yetu bado tuko nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo.
Watanzania tulio wengi tunaishi katika hali duni kimaisha,hizo gari za miaka ya karibuni bei zake ni juu na mwananchi mimi sina msamaha wa kodi kama ilivyo kwa mbunge.sijajua hili liliwekwa kwa lengo gani.
Vijijini bado hali za usafiri ni tete ..wananchi wachache sehemu nyingine bado wanatumia punda kwa usafiri wao,wagonjwa,maji na mizigo...huko nje unazawadiwa Land lover 109 model ya 1984. Unashindwa kuichukua kwa katazo hili...pengine gari kama hili..gumu,imara madhubuti lingesaidia sana kule kijijini kwetu ndani katika kuhudumia wagonjwa,mazao ya kilimo na pembejeo nk.
Kwa ujumla zuio hili linatuumiza mno sisi watu wa hali ya chini na kufubàza maendeleo..
Tuwaombe wabunge msomapo jumbe kama hii hebu jengeni hoja bungeni kuondoa zuio hili ikiwa pamoja na kushusha ushuru wa magari ili kuwe na uwiano mzuri wa kodi kati ya pesa ya manunuzi ya gari na ushuru tukumbuke gari si chombo cha anasa bali ni nyenzo muhimu ya maendeleo!
Magari yakiongezeka hadi vijijini kutachagiza maendeleo ya nchi kwa ujumla wake..tuombe wabunge litazamwe upya jambo hili.pamoja na ushuru wa magari.
Nawasilisha.