Kuweka Pamba kwenye miti ya krismasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuweka Pamba kwenye miti ya krismasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simple, Dec 17, 2009.

 1. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikijiuliza kuhusu utamaduni mzima wa krismasi na jamii yetu ya Tanzania.
  Ni kwanini tunaisheherekea sikukuu hii ya kuzaliwa kwa bwana yesu kwa mapombe, shopping za kuzima moto kwa watoto, na pilau la siku moja, tunafika mpaka kuweka pamba kwenye miti ya krismasi ili mazingara yetu yafanane na yale ya snow za magharibi.
  Brain washing kama hizi tunazaliwa nazo,,tunakua nazo na kuzipitisha kwa watoto wetu bila kujiuliza kimsingi nini lengo la sherehe nzima.

  Krismasi njema wana JF.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  KWA HIYO HOJA YAKO NI NINI SASA?
  brainwashing?
  chrismass?
  pamba?

  hueleweki!kwa hii thread peke yake unaonekana BRAIN-WASHED
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Noeli noeli tuimbe pamoja kwa maana amewajia watu wake na kuwakomboa.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sasa hizo brainwashing unazozizungumza ni nini, kama ni pombe, shopping, pilau la siku moja ni sikukuu zote iwe Iddi, maulidi, pasaka sasa hapa tatizo ni nini,

  kwa kuweka pamba kwenye hiyo miti we kinakuuma nini kama hauna imani na hivyo vitu?

  hebu kuwa wazi tukuelewe misimamo yako
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Haulewi msingi wa X-mass, au hauelewi kwa nini watu wanaweka pamba( jibu umeshalisema) au hutaki watu watumie pamba a

  Kama haujui lengo la sherehe tutakusaidia.Ila kama unalaumu kwa nini pamba zinatumika, hilo ni swala lingine katika mengi sana tuliyorithi kutoka kwa waleta hizi dini, sidhani kama kuna dini hapa Tz iliyokosa athari za kitamaduni.

  wazee wetu walivaa vibwaya tu(unazima mbele na nyuma sehemu za siri, leo hii tunavaa nguo tulizoiga kutoka kwa wageni(hata wewe humo) sasa ukija kwenye kwa nini tunaiga, jibu lake haliishii kwenye miti ya pamba, karibu kila kitu tumeigam kuanzia tamaduni, elimu, teknolojia,mavazi, etc. Hili la pamba ni dogo mno na maskini kwa Tz tunasherehekea siku mbili tu, wakati wenzetu mwezi wote wa 12 ni X-mass.

  Life is short cherish it,ili mradi haumuathiri mtu!
   
Loading...